Mwenendo wa Yanga tangu msimu mpya uanze unafurahisha. Wamecheza mechi mbili kwenye Ngao ya jamii (vs Azam na Simba) bila kuruhusu goli (ndani ya dk 90), wakaja kucheza mechi ya awali ya ligi ya klabu bingwa Afrika (vs ASAS) bila kuruhusu goli, na hatimaye wamecheza na KMC kwenye mechi ya NBC premier league na kumaliza bila kuruhusu goli.
Kwa upande mwingine, Yanga imeweza kufunga magoli katika mechi tatu kati ya hizo nne. Kwa ujumla timu hii ya Wananchi imeuanza vema msimu huu mpya wa mashindano
Kwa upande mwingine, Yanga imeweza kufunga magoli katika mechi tatu kati ya hizo nne. Kwa ujumla timu hii ya Wananchi imeuanza vema msimu huu mpya wa mashindano