Yanga na Simba SC hamtoboi

ila timu yangu ya Yanga inahitaji kushinda ugenini mara mbili.
Kinachoniuma ni timu yetu pendwa kushika mkia katika CAFCL kwa group lao ilhali katika NBC league wanaongoza, na hivi juzi walipiga mtu mkono wa nyani.

Nikisema tunahujumiwa nitakuwa nimekosea?
 
Dah..😭😭 Kweli mkuu, Yaani Natamani sana turudi kule Shirikisho, kule tulikuwa tunajipigia tu hadi tukavaa na medali
Itabidi mwakani tujilengeshe tucheze Shirikisho, huku kwa mabingwa ni balaa
 
Aisee huku kwa mabingwa kweli kugumu, mwakani turudi tu Shirikisho hakyanani, huku ni kuumbuka
 
Yanga anahitaji kuhinda mechi moja ugenini na mechi mbili za nyumbani. Hatima ya Simba na Yanga zipo kwenye fixture inayofuata
 
Aisee huku kwa mabingwa kweli kugumu, mwakani turudi tu Shirikisho hakyanani, huku ni kuumbuka
Ni kweli kugumu sana maana tokea msimu uanze hakuna hata mechi moja tulioshinda, yaani ni sare ndio ushindi wetu hata kwa vitimu vilivyochini kwenye CAF ranking
 
Wydad anapigika vizuri tu nje ndani, we si unaona vilaza kama akina Jwaneng Galaxy na Asec wanajipigia, Simba atashindwa?
Mechi waliyofungwa ns jwaneng ni bahati tu iliwabeba jwaneng, walizidiwa sana, Wydad sio wabaya , sema wamekosa umaliziaji mzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…