Yanga na Simba unazi wa zamani: Kisa cha Mzee Mangara Tabu na Ayubu Kiguru

Yanga na Simba unazi wa zamani: Kisa cha Mzee Mangara Tabu na Ayubu Kiguru

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
YANGA NA SIMBA UNAZI WA ZAMANI: KISA CHA MZEE MANGARA TABU NA AYUBU KIGURU

Nina rafiki yangu anaitwa Kazua leo asubuhi kanipa kisa cha Mzee Mangara Tabu na Ayubu Kiguru. Wakati wa ujana wake Kazua alikuwa mkoba, yaani "centre half," wa Dundee United.

Leo mimi na sahib yangu Kazua akitutokea simba ghafla tumeliwa. Miguu hainyanyuki ardhini haitaki inatukatalia sharti tuibembeleze.

Mzee Mangara Tabu alikuwa President wa Yanga na Ayubu Kiguru alikuwa shabiki mkubwa sana wa Sunderland na unaweza kusema ndiyo Haji Manara wa enzi hizo.

Haji mwanafunzi kwa Ayubu.
Ayubu alikuwa na kipaji cha ajabu.

Mtu wa vibweka lukuki.

Sunderland ikichukua kikombe asubuhi anakujanacho sokoni anakiweka mbele ya ubao wake washabiki wa Sunderland wakija sokoni wanatunza.

Hapo Ayubu kavaa jezi no. 6 ya Hamisi Kilomoni. Jioni soko likifungwa anahesabu fedha zilizotunzwa anapeleka club Congo na Mchikichi.

Soko zima lile limejaa wanazi wa Yanga basi Ayubu peke yake anapambananao na mwisho wa siku wanasalimu amri wanafunga virago hao wanaondoka.

Ayubu alikuwa ana ubao wa biashara Kariakoo Market. Siku hiyo Mzee Mangara kenda sokoni kununua mahitaji yake.

Ayubu kumuona Mzee Mangara akamuamkia kisha akamwambia, "Mzee Mangara kanunue hiliki tu basi. Vingine vyote vilivyobakia njoo uchukue kwangu bure."

Yanga ilikuwa imefungwa na Sunderland. Mzee Mangara akamshukuru Ayubu kisha akamwambi, "Tutakutana Ilala Stadium."

Ayubu akamjazia vitu Mzee Mangara kwenye jumu lake, Mzee Mangara akimshukuru Ayubu akashika njia kwenda nyumbani kwake ambako hapakuwa mbali na sokoni.

Hapo chini soko la Kariakoo kama lilivyokuwa enzi hizo.

1625373115140.png
 
Shikamoo.

Ulivyoanza na Dundee United nikafikiria kumbe wazawa walishaanza kucheza nje zamani ila ulipoitaja na Sunderland nikajicheka.

Ila Mwalimu wangu alinikata maksi kwa kuandika 'Kutunza' akisema ni 'kutuza' ikitokea kwenye 'tuzo'. Nilifikiri yupo sahihi kwa miaka yote.
 
Castr...
Marahaba.
Ni hivi.

Mimi nazungumza Kiswahili cha pwani na kwetu ni kutunza.

Huenda huyu mwalimu ni mtu kutoka bara yeye kwao wanasema "kutuza."

Sote tuko sawa.
 
Shikamoo.

Ulivyoanza na Dundee United nikafikiria kumbe wazawa walishaanza kucheza nje zamani ila ulipoitaja na Sunderland nikajicheka.

Ila Mwalimu wangu alinikata maksi kwa kuandika 'Kutunza' akisema ni 'kutuza' ikitokea kwenye 'tuzo'. Nilifikiri yupo sahihi kwa miaka yote.
Kutuza? He labda hicho ni kiswahili cha bara.
 
Nikiona picha za aina hii, moyo unaingia ganzi. Hakuna kinachodumu kwenye haya maisha yetu. Kila wakati mambo yanabadilika. WEatu wanakuja na kwenda.

Tujifunze kuishi maisha ya uadilifu maana sisi ni wapitaji na haya tunayodhani yanadumu, nayo yanabadilika. Hilo jengo sijui ni jengo gani. hakika haliko kama lilivyo kwenye picha sasa hivi.
 
nikiona picha za aina hii, moyo unaingia ganzi. Hakuna kinachodumu kwenye haya maisha yetu. Kila wakati mambo yanabadilika. WEatu wanakuja na kwenda.
Tujifunze kuishi maisha ya uadilifu maana sisi ni wapitaji na haya tunayodhani yanadumu, nayo yanabadilika. Hilo jengo sijui ni jengo gani. hakika haliko kama lilivyo kwenye picha sasa hivi
Tangawizi,
Hilo ni Soko la Kariakoo kama lilivyokuwa hapo zamani.
 
Kwa wale wasiojua, ule uwanja wa Karume yalipo makao makuu ya TFF ndio ulikuwa unaitwa "Ilala Stadium." Ingependeza sana iwapo uwanja ule ungeboreshwa zaid kufikia kiwango cha kimataifa pia kusudi dar iweze kuendesha michezo miwili au mitatu ya kimataifa kwa mpigo, hasa ukizingatia uzito wa jina la uwanja wenyewe.
 
Kiswahili fasaha ni kutuza. Angalia kamusi. Kutunza ni jambo lingine. To care. Wakati kutuza ni to reward
Kwenye taarabu, ngoma au michezo ni kwamba unatunza (pesa au kitu), sijawahi kusikia mtu akisema anakwenda kutuza.
 
nikiona picha za aina hii, moyo unaingia ganzi. Hakuna kinachodumu kwenye haya maisha yetu. Kila wakati mambo yanabadilika. WEatu wanakuja na kwenda.
Tujifunze kuishi maisha ya uadilifu maana sisi ni wapitaji na haya tunayodhani yanadumu, nayo yanabadilika. Hilo jengo sijui ni jengo gani. hakika haliko kama lilivyo kwenye picha sasa hivi
Soko hilo pichani bado lipo sema Matangazo ya Biashara yanaficha mengi
 
Back
Top Bottom