Yanga na teams zote za ligi kataeni huu upuuzi

Mwamuzi anaruhusiwa kuanzisha mpira kukiwa na wachezaji saba ndani akiwamo golikipa hivyo kwa golikipa wa Singida United kuwa nje ya uwanja na mwamuzi kuruhusu mpira uendelee alikuwa amevunja sheria,nitaitafuta niweke hapa.

Hili la timu kuwa na viporo zaidi ya 12 ni maajabu yanayopatikana tanzania pekee,hakuna maajabu kama hayo duniani kote zaidi unayapata hapa Bongo Darisalama kwenye soko lililojaa kila aina ya ubabaishaji na mkumbuke msimu ambao Yanga anashiriki mashindano ya KImataifa yule msema hovyo wa Simba alilalamika sana Yanga kuwa na viporo ambavyo hata vilikuwa havifiki sita lakini kibao kimegeukia kwao amekuwa kimya kama mbwa kabanwa na mjusi.

Tuendelee kunywa mtori nyama zipo chini
 
Kelele zote hizo ni yanga kukosa ubingwa Lau mngeupata hoja hizi usinge zileta hapa.

Ubovu wa ligi ya bongo sio viporo tuu. yako mengi mnooo sasa yanga kukosa ubingwa sababu mnayo ishikia bango ni viporo .
Umeulizwa ushawahi ona ligi ambayo timu ina viporo 12? Hujajibu
 
Kelele zote hizo ni yanga kukosa ubingwa Lau mngeupata hoja hizi usinge zileta hapa.

Ubovu wa ligi ya bongo sio viporo tuu. yako mengi mnooo sasa yanga kukosa ubingwa sababu mnayo ishikia bango ni viporo .
Maelezo meeeengiiii JIBUNI KAMA MMEWAHI ONA TIMU INA VIPORO 12....
 
Hawajui ndugu yangu , hao wamerishwa matango pori na kocha wao anaejua kila kitu kumbe hamna kitu
Kwa anayejua mpira hakuna mpira kusimama kama mchezaji yupo nje ya touchline. Halafu angalia kipa alivyotoka nje alimwangalia refa kwanza halafu akaendelea kulala. Alikuwa na nafasi ya kurudi uwanjani na kutupa gloves. Wachezaji wanatakiwa kuwa na uelewa wa sheria kadri inavyowezekana.
 
Umeulizwa ushawahi ona ligi ambayo timu ina viporo 12? Hujajibu
Shinda mechi zako uone kama viporo vitamsaidia mshindani wako. Tatizo mliteleza kwa Simba, Lipuli, Stand Utd, na Biashara, na mkatoa sare kadhaa zikiwemo za Ndanda zote mbili, Simba na singida. Hapo umedondosha point za kutosha, ungeshinda hizo mechi hata viporo vya Simba vingekukuta ukiwa bingwa
 
Ahahahahaa mnaendeleza maelezo tu... JIBUNI SWALI LA MSINGI...Mmewahi ona kwenye ligi yoyote duniani eti kuna timu ina viporo 12..?? Mnakimbia HOJA... Si mseme kama mmewahi au la!!
 
kwa ufatiliaji wako wa soka umewahi sikia timu ina viporo 12

ama timu kucheza kila baada ya siku 2

ama backpass kuwa offside

ama mpira kuendelea ikiwa golikipa kaumia
Shadaaaaappp

Subirini mwakani
 
Wana yanga msiilaumu TFF Jilaumuni ninyi wanachama na viongozi wa timu kwa kushindwa kulipa mishahara na posho za wachezaji.

haiwezekani mchezaji hajalipwa mshahara kwa zaidi ya miezi 5 alafu akawa focus uwanjani.

hayo malalamiko yenu ni kama mbuni kujificha kichwa mchangani wakati mwili uko nje. Jipangeni kiuchumi alafu tukutane uwanjani.
 
kwa ufatiliaji wako wa soka umewahi sikia timu ina viporo 12

ama timu kucheza kila baada ya siku 2

ama backpass kuwa offside

ama mpira kuendelea ikiwa golikipa kaumia
Yaani washkaji TFF wamekuwa bwabwa kabisa kwa Mo.
 
Moira hauchezwi bila kipa.
 
Unamkumbuka yule aliesema simba haitakuja chukua ubingwa akiwa ye madarakani pale TFF?

Mbona hukulalamika
 
Mkuuu wewe ungeshinda mechi zako zote hivyo viporo vya mnyamaa vingekuathili nini? .
unazungumzia soka ama kabumbu, psg,liva,baka na ubora wao wanategjemea matokeo 3, kumtaka Yanga ashinde tu bila suruhu wala kupigwa hilo sio SOKA ni KABUMBU

kama ungepewa nafasi ya kuongoza soka ukaja na mawazo kama haya ni ajabu sana
 
Mimi sipendi kutoa ushauri wa bure bure tu ila nashauri Yanga au Azam au timu yeyote inayotaka kuuchukua ubingwa wajifunze kushinda kila mchezo mbele yao. Viporo vya wenzako havita kuumiza tumbo kwani weye huli kiporo
 
Kwahiyo kuhusu viporo ulitaka simba wanyanganywe asicheze au? Maana walikuwa wanacheza kimataifa hakukua na namna nyingine, unasema hujawahi kuona je ni sheria ya mpira inakataza au ni haijatokea tu?
kimataifa alicheza peke yake vp tp,vital,j.s soura kwenye ligi zao wallikuwa na ivo viporo 12
 

Hivi yanga kwanini hamkushinda mechi zenu zote
 
kufungwa siyo tatizo, tatizo je ulifungwa kihalali....kuna figisu za kupangiwa matches za mbali mfululizo..mfano Tanga to singida then Tanga tena ukitoka hapo Lindi...makusudi tu..magoli halali kukataliwa...kunyimwa penalt za wazi nk
Je ungepangiwa ratiba ngumu ungesemaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…