Sio kazi ya TFF, Bodi ya Ligi au Marefarii kuzijengea uwezo baadhi ya timu kuchukua ubingwa. Uwezo unatokana na maandalizi ya kila timu moja moja, kuanzia usajili hadi training. Kumbuka mlivyokuwa mkibeza bajeti ya bilioni 1.3, mnadhani mambo yanajiendea kwa mazoea tu? Watu wamewekeza, viongozi wa timu hizo za Kagera Sugar na Lipuli pia wakitafuta fedha za kutosha maandalizi kama ya Simba, watatoa ushindani hadi wa kubeba ubingwa, na wala sio ajabu. Mbona Azam amebeba ndoo, tena zote ya Bara na ya Kagame Cup? Kwa kuwa aliwekeza katika usajili na uendeshaji. Yanga ilikuwa inagoma kufanya uchaguzi, sasa nani atawapa malezi wachezaji, kocha? Yaani kocha ameajiriwa uje umtegemee ndio awabembeleze wachezaji wasigome? Yanga mkubali kuwa hamkuwa na kikosi kizuri kama Simba, na hamkuwa na viongozi wazuri kama Simba