Yanga na teams zote za ligi kataeni huu upuuzi

Yanga na teams zote za ligi kataeni huu upuuzi

kukiwa na viporo umerahisishiwa
Yanga aliwahi kucheza home and away uwanja wa Taifa. Hamkulalamika. Yanga akacheza mechi 11 uwanja wa nyumbani na hamkulalamika. Ili malalamiko yako yawe ya msingi hutakiwi kukaa kimya unapokuwa kwenye advantage na kulalamika Iinapokuwa kinyume chake katika premises hizohizo.
 
Anzeni nyie Yanga kujitoa... Uone Kama kuna watakaowafuata. Mlizoea enzi za Malinzi na Manji basi mnajiamanisha kuwa hata TFF ya sasa inafanya madudu ya TFF ya Malinzi.
 
kwa ufatiliaji wako wa soka umewahi sikia timu ina viporo 12

ama timu kucheza kila baada ya siku 2

ama backpass kuwa offside

ama mpira kuendelea ikiwa golikipa kaumia
dah nakumbuka ratiba ile yanga anacheza na coastal kisha anaenda singida usiku tena anarudi kucheza na mgambo kisha leo anapumzika wiki mbili bila game
 
nmeandika kwa kifupi sababu hamna mpenda soka wa TZ ambaye hajui madudu ya ligi yetu...kuanzia bodi ya ligi, upanga fixture na kubadili fixture...waamuzi rushwa plus uwezo mdogo nk
Ok, madudu ninayoyaona mimi ni TFF kuibeba Yanga, waliipangia mechi nyingi rahisi rahisi za zote zikachezwa Dsm, huku wakikwepesha mechi ngumu kama vile ya Azam, lengo lilikuwa Yanga aongoze ligi mapema ikibidi atangaze ubingwa kabla hata hajakutana na mechi ngumu, wewe unaonaje?
 
Mkuuu wewe ungeshinda mechi zako zote hivyo viporo vya mnyamaa vingekuathili nini? .
Anza kumwuliza Haji Manara, kuna wakati Yanga ilikuwa na viporo viwili Manara aliongea bi Hindu cha mtoto. Uzuri mashindano yajayo Simba hatafika mbali kimzimu mzimu kama alivyopita mwaka huu.
 
Viporo 12 angefungwa 6 ungesemaje? Anacheza kila baada ya siku 2 angefungwa mechi zote unhetoa jibu gani?
kwa ufatiliaji wako wa soka umewahi sikia timu ina viporo 12

ama timu kucheza kila baada ya siku 2

ama backpass kuwa offside

ama mpira kuendelea ikiwa golikipa kaumia
 
Mlipaswa kushinda mechi zenu zote kama mliavyoanza ligi,

Lakini mkajipa moyo kuwa hawawezi kushinda viporo kumi na 12 hata mechi sita.

Mwigulu Nchemba alijipa moyo kwa kusema msimu huu simba msitarajie mteremko, ligi itakuwa ngumu!

Matokeo yake vipi sasa?
Miaka yote yanga wamebeba ndoo hakukua na ujinga huu

Wamejidhalilisha tu
 
Tumia muda huu kutafuta pesa, siku familia yako ikilala njaa Yanga hawatoweza kukupa hata dagaa wa buku maana hawana.
Mpaka leo hujui njaa haina mbabe? Yanga kuna njaa hiyo sio siri msitegemee miujiza.
 
maandalizi ni kitu kimoja na ubingwa ni kitu kingine...chukulia mfano wa leister city ilivyotwaa ndoo ya uingereza...tunataka
kuwe na fairness teams kama Kagera shuga au lipuli ziwe na uwezo wa kuwa bingwa
Acha ujinga bro.wakati Leicester ciru anatwaa ubingwa unawajua wachezaji wake?

Usiongelee kutwaa ubingwa tu unajua UEFA walimaliza hatua gani?

Alafu jiulize ile Leicester city ya wakati ule sawa na leo?

Rudi bongo. Hivi Yanga walifanya usajili gani hasa wa maana zaidi ya Makambo na Fei Toto. Ukiacha hao timu nzima mlikuwa na vilaza wangapi na spana mkononi wangapi?

Rudi pale msimbazi, kaangalie walifanya nini kabla ya ligi kuanza na walisajili wachezaji gani?
 
Ndio maana tukienda kukipiga Na watu kweli tunakula hamsa hamsa hamsa tunakuwa km tumesimama vile!!!! Kwa mambo km hayaaa!!!
 
Kama hamkufungwa kihalali kwa nini msikate rufaa? Tena rufaa mngepeleka fifa kabisa maana tff imejaa wanasimba!
...vile vile vipi kuhusu FA, mlivyofungwa na lipuli haikuwa halali?
Kumbuka lipuli waliwafunga kwenye ligi pia!
Hahah mkuu hapo ulipotaja FIFA umenikumbusha mbali sana. Vipi mrejesho wa ile Barua ya Haji Manara kukata rufaa kule FIFA?!
 
Nimeikuta mahali
1b00cc553e5f247b29724400faade16c.jpeg
 
kwa ufatiliaji wako wa soka umewahi sikia timu ina viporo 12

ama timu kucheza kila baada ya siku 2

ama backpass kuwa offside

ama mpira kuendelea ikiwa golikipa kaumia
Vyura nyie mmesahau fadhila za TFF na bodi ya ligi kuwabeba masimu ulipoanza mkapangiwa ratiba ya kucheza Taifa mechi zaidi ya kumi nyumbani ili mpate fedha za kujibust??? Umewahi kuona wapi ligi moja timu inakuwa na ratiba ya kucheza nyumbani mechi zote hizo mfululizo??? Hapo ndipo mlipopatia points za kupata kiburi cha kudhani kwamba mngeweza kuchukua ubingwa na kujilinganisha na simba. Ile ratiba ya awali iliwasaidia sana kupata points na fedha za kujiendesha nyie watembeza bakuli alafu ikaathiri timu ndogo akina Alliance unakuta timu ina gemu musoma, next wk mbeya, then dar kukutana na yanga mnajipigia tu mkiwa mmetulia! Yaani vyura kwa akili zenu mngeweza kuchukua ubingwa mbele ya simba ya Mwaka huu??? Mna miaka mingine mitano ya kusubiri. Suala la viporo ni kawaida kwa Afrika hata mazembe na al ahly bado wanaendelea kumalizia viporo japo walikwishatolewa nusu fainali, yanga nyie mlikuwa mnapata viporo vile vile sema vilikuwa vichache coz mlikuwa mnatoka raundi ya pili tu! Aliyekuzidi kakuzidi tu acheni kulalamika! Yaani mmefikia mahali hata mkifungwa na lipuli mnasema tumefungwa sababu ya simba! Malalamiko Fc
 
Ushabiki tuweke kando, ligi yetu ya Tanzania bara ipo corrupted, kuanzia daraja la kwanza ndiyo madudu kabisa, ligi kuu bingwa anaandaliwa kabla ligi kuchezwa

Tatizo lipo TFF, nachelea kusema bodi ya ligi au chama cha marefa....sababu TFF wanajua kabisa madudu ya hizi idara na wana mandate ya kuzivunja wapo kimya.

Ushauri wangu kama hakutatokea mabadiliko kwenye hizo sehemu hapo juu...tutegemee simba kuchukua ubingwa misimu yote mpaka mabadiliko ya uongozi wa TFF, chama cha waamuzi na bodi ya ligi vipo corrupted.
We shabiki wa yanga tuu, misimu mi3 yanga alichukua kombe na alikuwa na mechi za viboro kutokana na mechi za kimataifa kama simba msimu huu. Mnaumia nini sasa. Ebu kuweni na kumbukumbu.
Achilia mbali hivyo viporo alivyokuwa navyo simbo, angalia quality ya wachezaji wa simba then fananisha na timu nyingine za ligi kuu.
Sio unakuja hapa na kimada chako afu unazuga ushabiki tuweke pembeni.
 
Hoja ya kibaguzi
Ushabiki tuweke kando, ligi yetu ya Tanzania bara ipo corrupted, kuanzia daraja la kwanza ndiyo madudu kabisa, ligi kuu bingwa anaandaliwa kabla ligi kuchezwa

Tatizo lipo TFF, nachelea kusema bodi ya ligi au chama cha marefa....sababu TFF wanajua kabisa madudu ya hizi idara na wana mandate ya kuzivunja wapo kimya.

Ushauri wangu kama hakutatokea mabadiliko kwenye hizo sehemu hapo juu...tutegemee simba kuchukua ubingwa misimu yote mpaka mabadiliko ya uongozi wa TFF, chama cha waamuzi na bodi ya ligi vipo corrupted.
 
Back
Top Bottom