Yanga na Ushirikina:Mliberia afichua Maji ya Kichawi, Mrwanda ayanywa

Yanga na Ushirikina:Mliberia afichua Maji ya Kichawi, Mrwanda ayanywa

Freeland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
14,481
Reaction score
10,227

sherman.jpg

MASTRAIKA wawili wa Yanga wamekumbana na uchawi wa aina yake. Kpah Sherman ambaye ni Mliberia amedai kuyabaini maji ya ushirikina yaliyokuwa uwanjani, lakini mwenzake Danny Mrwanda akayachukua akayanywa huku kipa aliyeyaweka akiwashangaa.

Kpah ambaye si mzungumzaji sana, alifichua tukio hilo lililotokea kwenye mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo timu hizo hazikufungana.

Lakini mlinda mlango wa Ndanda, Wilbert Mweta, ambaye ni kipa wa zamani wa Simba, aliposikia maneno ya Sherman akashangaa. Katika mchezo huo, washambuliaji wa Yanga; Sherman, Mrwanda na Simon Msuva walikosa mabao ya wazi wakiwa peke yao mbele ya lango, kila walipopiga mipira ilipaa na kutoka nje hali ambayo iliwashangaza wapenzi wa soka na mashabiki waliofika uwanjani hapo. Hata hivyo kocha wa Yanga, Hans Pluijm, amepuuza madai hayo na kusema ni uzembe tu wa wachezaji wake.

Sherman ameiambia Mwanaspoti kwamba kwenye goli la Ndanda kulikuwa na maji ya ushirikina na aliyatoa kwa mikono yake baada ya kugundua kwamba kipa huyo aliyanyunyizia kwenye goli na baadaye akayabakiza mengine na kuyaweka pembeni ya mlingoti wa lango.

Baada ya Mliberia huyo kuyatoa maji hayo na kuyatupa nje, bado yalikuwa magumu kwao kisha Mrwanda aliyafuata na kuyanywa. Hata hivyo haikusaidia chochote kwani ndio kwanza wapinzani wao walizidi kukaba huku wakijiangusha kupoteza muda.

Sherman aliiambia Mwanaspoti akisema: "Mimi ni Mwafrika moja kwa moja naamini maji yale yaliwekwa vitu tu vya kishirikina ikawa sababu ya kutukosesha mabao, ndiyo maana niliamua kuyatupa nje, haiwezekani mtu na goli unapaisha.

"Pia nilimwona kwa macho yangu yule kipa, yale maji aliyamimina (anaonyesha kwa ishara) kuanzia mwanzo wa goli hadi mwishoni kwa nini alifanya vile ndio yalikuwa kikwazo kwetu,"alisema Sherman ambaye Yanga wanamchukulia kuwa ndiye straika namba moja wa timu yao.

Ingawa Mrwanda hakupenda kufafanua hilo, kipa Mweta alijitetea akisema: "Ule ni mpira ndiyo maana tunafanya mazoezi, hakuna ushirikina wala nini.

"Nimeshangaa sana kuona mchezaji mkubwa kama yule kuamini mambo hayo ya kishirikina badala ya kucheza mpira, anajua kiwango chake ni kidogo?"

Kocha Pluijm alisema hawezi kuwalaumu washambuliaji wake kutokana na kitendo cha kushindwa kufunga mabao na badala yake anaulaumu mfumo wa makuzi ya soka waliyokulia wachezaji hao tangu utoto wao.

Pluijm alisema suala la kufunga ndiyo jambo kubwa alilokuwa akiwaelekeza katika kipindi chote cha mazoezi yao na walikuwa wanafanya vizuri mazoezi. Alisema aligundua tatizo hilo katika michezo waliyocheza na Polisi Morogoro na Ruvu Shooting.

"Hatufungi, sina wasiwasi na safu ya ulinzi lakini kwa washambuliaji tatizo lao ni ufungaji, nimekuwa nikilifanyia kazi kwa siku zote kwenye mazoezi yetu na wachezaji walikuwa wanafanya vizuri," alisema kocha huyo.

"Siwezi kuwalaumu wachezaji wangu kwa nini hawafungi, unaona ni tatizo ambalo lilitokana na makuzi yao tangu walipokuwa wadogo, kwa sababu wanafuata maelekezo na wanafika golini, yuko yeye na kipa, anashindwa kufunga, anapiga mpira unapaa juu.

"Lakini umakini nao haukuwepo ingawa natambua pamoja na kufunga mazoezini, hali huwa inakuwa tofauti na mnapokuwa mnacheza mechi."

Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro' aliwataka mastraika wake kuwa makini na kuhakikisha wanafunga mabao kwani kwa sasa hawafanyi kazi hiyo kikamilifu.

"Si mimi tu, hata wenzangu wanashangazwa na hali ya timu kutopata mabao. Naamini hili linatokana na safu ya ushambuliaji kukosa umakini," alisema.

" Binafsi, mimi na safu yangu ya ulinzi tunatimiza kazi yetu ya kuzuia kikamilifu na hilo ni dhahiri kwa kuwa tunajitahidi kutoruhusu mpira kufika kwenye goli letu.

"Lakini Yanga ina washambuliaji wengi ambao wote wameletwa kwa kazi moja ya kufunga mabao. Naamini wanatakiwa kuifanya kazi hiyo wakishirikiana na sisi, lakini wao ndiyo wanalo jukumu la kufunga zaidi yetu, sisi mabeki kazi yetu ni kuzuia."

Beki huyo wa kutegemewa wa Yanga huwa anafunga kati ya mabao matatu hadi saba kila msimu wa Ligi.

Source: Mwanaspoti

Yanga mbona mnakuwa wachawi kiasi hicho....timu zingine zote hazilalamikii uchawi ila nyie tu Makoye Matale Bantu lady mkolaj Deo Corleone sembo Amavubi grafani11 Masuke Sibonike barafuyamoto Revocatus Kashaga

Kwani ile timu iliyotishia kuuhama uwanja wa ccm kirumba kule mwanza kwa madai kuwa wanalogwa na timu ya toto africa na kusababisha kupoteza michezo mitatu mfululizo sio ya ligi kuu!!!!?
 
Acheni kujifariji na huu upuuzi mkuu
Haya ni mambo ya kijinga katika soka
Kama Yanga wanashindwa kubadili mentality ya wachezaji wao kujua kuwa mpira unachezwa uwanjani basi hapo kuna shida kubwa.

Kipa wa ndanda amejibu vizuri sana

Ingawa Mrwanda hakupenda kufafanua hilo, kipa Mweta alijitetea akisema: "Ule ni mpira ndiyo maana tunafanya mazoezi, hakuna ushirikina wala nini.

"Nimeshangaa sana kuona mchezaji mkubwa kama yule kuamini mambo hayo ya kishirikina badala ya kucheza mpira, anajua kiwango chake ni kidogo?
 
Kwani ile timu iliyotishia kuuhama uwanja wa ccm kirumba kule mwanza kwa madai kuwa wanalogwa na timu ya toto africa na kusababisha kupoteza michezo mitatu mfululizo sio ya ligi kuu!!!!?

Kwa hio kwa sababu hiyo timu imefanya hivyo na nyie mfanye hayo.
Nyie si ndio mnasema ni timu bora zaidi tanzania?
Ubora wenu uko wapi?
Kama mnashindwa kujua kuwa mpira unachezwa uwanjani.
 
Kwa hio kwa sababu hiyo timu imefanya hivyo na nyie mfanye hayo.
Nyie si ndio mnasema ni timu bora zaidi tanzania?
Ubora wenu uko wapi?
Kama mnashindwa kujua kuwa mpira unachezwa uwanjani.

Mkuu Freeland usijidanganye kwamba klabu yako haijihusishi na mambo ya ushirikina. Mimi ninao ushahidi wa Simba kuchinja kondoo mweusi siku moja kabla ya mechi na Yanga na Simba kuambulia kipigo cha 3-1. Nataka tu ujue kuwa usipende sana kurusha lawama kwa mtani wako wakati hata timu yako ya Simba imebobea kwa ushirikina. Twende kwenye uzi wa updates za leo Mkuu. Huna cha kujivunia kuhusu ushirikina wa hizi timu mbili.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hio kwa sababu hiyo timu imefanya hivyo na nyie mfanye hayo.
Nyie si ndio mnasema ni timu bora zaidi tanzania?
Ubora wenu uko wapi?
Kama mnashindwa kujua kuwa mpira unachezwa uwanjani.
Kwani nalo hilo linahitaji elimu ya juu ili kujua kuwa yanga ndio timu bora tanzania!!!?
0key! hebu turudi kwenye mada husika, Nilichomaanisha hapo ni kwamba kwenye post umekosea unaposema kuwa yanga ndio timu pekee ya ligi kuu inayolalamika kuhusu maswala ya ushirikina.
 
Kwa hio kwa sababu hiyo timu imefanya hivyo na nyie mfanye hayo.
Nyie si ndio mnasema ni timu bora zaidi tanzania?
Ubora wenu uko wapi?
Kama mnashindwa kujua kuwa mpira unachezwa uwanjani.

Ubora wetu upo kwenye msimamo wa ligi na keshokutwa tunacheza shirikisho nyie bakini na kombe lenu la Mbuzi(mapinduzi+ngao ya hisani) sisi tunaenda kimataifa
 
kwanini Yanga wanaamini ktk ushirikina? ndio maana timu haiendelei kamwe asilani
 
Ubora wetu upo kwenye msimamo wa ligi na keshokutwa tunacheza shirikisho nyie bakini na kombe lenu la Mbuzi(mapinduzi+ngao ya hisani) sisi tunaenda kimataifa

Mkuu kombe la NGAO YA HISANI lipo kwa timu ya wananchi dar young africans...Wao wanalo lile la CCM na lile sijui la NANI MTANI MPINI kama sikosei.
 
Kwani nalo hilo linahitaji elimu ya juu ili kujua kuwa yanga ndio timu bora tanzania!!!?
0key! hebu turudi kwenye mada husika, Nilichomaanisha hapo ni kwamba kwenye post umekosea unaposema kuwa yanga ndio timu pekee ya ligi kuu inayolalamika kuhusu maswala ya ushirikina.

Mkuu; don't argue with mbumbumbu people will not know the difference!
 
Acheni kujifariji na huu upuuzi mkuu
Haya ni mambo ya kijinga katika soka
Kama Yanga wanashindwa kubadili mentality ya wachezaji wao kujua kuwa mpira unachezwa uwanjani basi hapo kuna shida kubwa.

Kipa wa ndanda amejibu vizuri sana

Ingawa Mrwanda hakupenda kufafanua hilo, kipa Mweta alijitetea akisema: "Ule ni mpira ndiyo maana tunafanya mazoezi, hakuna ushirikina wala nini.

"Nimeshangaa sana kuona mchezaji mkubwa kama yule kuamini mambo hayo ya kishirikina badala ya kucheza mpira, anajua kiwango chake ni kidogo?

Mbona nyie mnawalalamikia UKAWA au wao ndio wachezaji, tena mwadai wanabadilisha nguo kila kipindi nawasilisha
 
Mbona hata Simba inaamini hayo hayo?

http://millardayo.com/fainim7/

Hivyo unavyosema vinadhaniwa vya kishirikina ni vitendo vipi hivyo?

Tatizo hapa naliona kwa yule anayedhani...yeye ndiye mshirikina....kwa sababu you see what you think.

Yanga ndio mara zote wanadhani...wakifungwa mara gloves..mara taulo....leo maji...hahahahaha
 
Mbona nyie mnawalalamikia UKAWA au wao ndio wachezaji, tena mwadai wanabadilisha nguo kila kipindi nawasilisha

Kuna kauli gani formal imewahi kutoka aidha kwa mchezaji...kocha ,....benchi la ufundi au uongozi wa timu kuwalalamikia ukawa kuwa ni washirikina?

Acheni kuzusha....hizo ni tabia zenu za ajabu yanga

Na kwa mtindo huu...wale Vibonde BDF watawafunga
 
Mkuu Freeland usijidanganye kwamba klabu yako haijihusishi na mambo ya ushirikina. Mimi ninao ushahidi wa Simba kuchinja kondoo mweusi siku moja kabla ya mechi na Yanga na Simba kuambulia kipigo cha 3-1. Nataka tu ujue kuwa usipende sana kurusha lawama kwa mtani wako wakati hata timu yako ya Simba imebobea kwa ushirikina. Twende kwenye uzi wa updates za leo Mkuu. Huna cha kujivunia kuhusu ushirikina wa hizi timu mbili.

Mkuu ...toa ushahidi...sisi tunaongea hapa na tunakupa ushahidi moja kwa moja.

Ushirikina.jpg
Matukio ya hivi karibuni uwanjani, baadhi ya wachezaji na mashabiki wa Yanga wameonekana kuamini katika ushirikina. Picha na Maktaba

ilunga na hirizi ya Neto

Machi 30, mwaka jana Yanga ilijihusisha kwenye moja ya tukio la kushangaza la kishirikina. Yanga ilikuwa nyuma kwa bao 1-0 ndani ya dakika 10 pekee za mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mgambo JKT kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Hakuna mtu aliyeamini kama hilo linawezekana. Wakati mchezo huo unaendelea kiungo wa Yanga, Hassan Dilunga alimfuata mwamuzi wa mchezo huo na kumweleza kuwa mshambuliaji wa Mgambo, Mohamed Neto ana hirizi kwenye bukta yake. Hapa ndipo uchizi ulipoanzia.

Mwamuzi wa mchezo huo alitaka kumkagua Neto ndani ya bukta ili kuthibitisha kama kuna hirizi jambo ambalo straika huyo alilikataa kabisa.

Mtafaruku huo ulipelekea Neto kupewa kadi mbili za njano na kutolewa nje ya wakati huo timu yake ikiongoza kwa bao hilo moja.

Matokeo ya mwisho ya mchezo huo Mgambo ilishinda kwa mabao 2-1 lakini gumzo kubwa lilibaki kwa kitendo cha mchezaji wa Yanga kudai kuwa mwenzake amebeba hirizi. Aliwahi kuiona wapi kabla?

Taulo la Ivo

Huu unaweza kusema ni uvivu wa kufikiri ama kuchoka. Kwenye pambano la watani wa jadi Simba na Yanga msimu uliopita, aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu katika hali isiyotarajiwa aliparamia taulo la kufutia mikono la kipa wa Simba, Ivo Mapunda na kulitupa nje ya uwanja baada ya kukosa mabao ya wazi kwenye mchezo huo. Hisia za Kavumbagu ambaye sasa anacheza Azam FC, kama zilivyokuwa kwa wachezaji wengine wa Yanga na mashabiki wao walioshangilia kitendo hicho zilikuwa kwenye ushirikina.

Waliamini kuwa mabao wanayokosa yalitokana na taulo hilo la Mapunda. Hata hivyo licha ya kuliondoa taulo hilo bado Yanga ilishindwa kupata mabao na mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Msuva na pochi Morogoro

Hii ilikuwa imani ya ajabu kweli. Ni aibu kwa mchezaji wa kiwango cha Simon Msuva ambaye kila mtu anaamini kuwa muda wake kucheza soka la Bongo umekwisha na anatakiwa kutafuta timu kubwa za nje, yeye anaamini katika ushirikina tena wazi. Hii ilikuwa kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi msimu huu dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro, Septemba 20 mwaka jana.

Yanga ilikuwa nyuma kwa bao moja huku washambuliaji wa timu hiyo wakiongozwa na Msuva wakiwa wanalisakama lango la Mtibwa kama nyuki ili kusawazisha bao hilo. Hali ilionekana kuwa ngumu kutokana na umakini wa safu ya ulinzi ya Mtibwa na kipa Said Mohamed kuokoa michomo ya hatari.

Msuva alishindwa kuliona hilo. Alipoiona pochi ya kike pembeni ya lango la Mtibwa aliamini ndiyo inayozuia mabao yao. Uzalendo ulimshinda winga huyo mwenye kasi nchini na kuamua kuiparamia pochi hiyo na kuirusha nje ya uwanja. Hata hivyo hilo halikusaidia kwani Yanga ilijikuta ikiongezwa bao la pili. Mtibwa ilishinda mchezo huo kwa mabao 2-0.

Chimbua chimbua Kaitaba

Kwa bahati mbaya ama nzuri Yanga imekuwa na matokeo mabaya katika mechi nyingi ambazo wanahusisha ushirikina. Walipokwenda mkoani Kagera kucheza na Kagera Sugar, Yanga walijikuta wakiingia tena kwenye mambo ya kishirikina.

Baadhi ya mashabiki na watu kadhaa wakubwa ndani ya klabu hiyo walionekana wakifukua fukua vitu visivyoeleweka kwenye Uwanja wa Kaitaba ambako mchezo huo ungefanyika kesho yake.

Waliamini kuwa Kagera wameficha madawa uwanjani hapo ili waifunge Yanga. Licha ya fukua fukua hiyo, Yanga ilijikuta ikifungwa bao 1-0 na Kagera.

Shabiki na glovu za kipa

Hii ni ya juzi juzi tu huko Zanzibar katika Kombe la Mapinduzi. Baada ya imani hizi kutanda kwa wachezaji, mashabiki nao wameanza kuonyesha makucha yao baada ya kuamini kuwa timu yao huwa inashindwa kufunga mabao kwa sababu inalogwa.

Hili lilithibitika wiki iliyopita kwenye mechi ya hatua ya makundi ya Kombe la Mapinduzi kati ya Shaba ya Zanzibar na Yanga. Shaba iliaminika kuwa vibonde wa mashindano hayo.

Mashabiki wa Yanga waliamini kuwa timu yao ingeifanyia dhahama Shaba baada ya kuzifunga timu ngumu za Polisi Zanzibar na Taifa Jang'ombe mabao 4-0 kila moja. Waliamini kuwa Shaba ingefungwa mabao mengi zaidi ya hayo.

Hali ilibadilika kwenye mchezo huo na Shaba ilikuja imejipanga. Hadi dakika ya 80 mechi hiyo bado ilikuwa bila bila. Mashabiki wa Yanga wakaanza kuamini ni uchawi baada ya shabiki wake mmoja wa kike kupandisha mashetani na kusema kuna kitu katika lango la Shaba.

Ndipo shabiki mmoja kijana mwenye umri kati ya miaka 24-28 aliamua kuingia uwanjani na kwenda kutoa ‘glovu' za kipa wa Shaba golini na kuzitupa nje. Aliamini kuwa glovu hizo ndizo zilizokuwa zikiwazuia Sherman na Msuva wasifunge.

Kitendo cha Yanga kufunga bao moja baada ya kitendo hicho kilionekana kabisa kuwaaminisha mashabiki wengine kwamba glovu zile zilikuwa na uchawi.
 
Kuna kauli gani formal imewahi kutoka aidha kwa mchezaji...kocha ,....benchi la ufundi au uongozi wa timu kuwalalamikia ukawa kuwa ni washirikina?

Acheni kuzusha....hizo ni tabia zenu za ajabu yanga

Na kwa mtindo huu...wale Vibonde BDF watawafunga

Naona wewe uijui simba kamuulizie mtu mmoja anaitwa Hassan Mbashiri je mkono wake umekuwa mkubwa kwa ajili ya nini...Muulize Hassan Dalali kafukia vitu vingapi yeye na Marehemu mzee Matuga katika makaburi ya Magomeni Mwinyimkuu. Au wakati Simba wanaruka ukuta ulikuwa haupo mkuu...mpira wa Tanzania huo ushirikina ndio unaotawala kila siku mkuu..au Muulize Aveva aliajiri wapenzi wa Simba pale Embassy hotel kwa ajili ya nini?
 
Back
Top Bottom