Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,725
Nitawalaumu kwa umakini mdogo mlioonyesha leo kufumania nyavu, nafasi 4 za wazi zingetosha kuwafanya muondoke na ushindi Leo hii, huwezi kupoteza nafasi kama hizo halafu ukategemea eti usonge mbele kwenye michuano mikubwa Kama hii, ukichezea nafasi basi ujue utaadhibiwa tu, pia sikuona mantiki ya kocha kumpeleka nje Makambo na kumuacha Mukoko ndani, ambae eneo lake na Mauya lilikuwa dhaifu sana.
Palikuwepo na haja ya kumuingiza Bangala kuituliza safu ya kiungo cha ukabaji, yote kwa yote nafikiri kocha amepata kipimo sahihi kinachomuonyesha ni kitu gani anatakiwa afanye kwenye mechi ya marudiano, hakuna kinachoshindikana Kama wamepata matokeo hapa basi hata yanga wanao uwezo wa kupata matokeo Nigeria pia, kilichopo ni kujipanga ipasavyo, makosa ya umakini na upangaji wa kikosi vinatakiwa kuchukuliwa kwa umakini mkubwa, kila la kheri!