Wakati wa Sakata la Feisal Salum nilipata wasaa wa kumsikiliza Wakala wa Dickson Job Bwana George Job. Kwenye interview ile George Job alisema hakuna Klabu yoyote ya mpira wa miguu Duniani inayopenda kumlipa mchzaji fedha nyingi. Kinachofanya timu kukubali kumlipa mchezaji fedha nyingi ni negotiation kati ya Wakala wa Mchezaji na Management ya Timu. Tatizo wachezaji wengi wa Tanzania hawana Mawakala wenye ujuzi wa negotiation. Utakuta mchezaji msimamizi wake ni baba, mama au mjomba ambaye hana ujuzi wa negotiation. Ukiacha hilo, Bacca amekuwa alivyo kiuchezaji kutokana na kuwa sehemu ya Kikosi cha Yanga na amekuwa branded na Yanga. Je, angeendelea kuwa JKU angefikia kiwango alichonacho? Ni sawa na Kibu Dennis angeendelea kuchezea Mbeya City angekuwa na mafanikio aliyo nayo sasa? Klabu zina mchango mkubwa kwenye maendeleo ya Wachezaji. Mchezaji akitaka alipwe vizuri basi awe na uwezo mkubwa wa kunegotiate vinginevyo ataishia kulalamika tu.