Yanga rasmi yamtangaza mbelgiji luc Eymael kuwa kocha mkuu

Yanga rasmi yamtangaza mbelgiji luc Eymael kuwa kocha mkuu

Yaani vituko havi kosekani tayar makocha wa Simba na yanga washapewa a.k.a 😊

Wasimba-kishingo
Wayanga-trump
 
Huyu Ajiandae Kufukuzwa kwa Zengwe

Huo ujinga Umenunua Duka Gani?
 
Klabu ya Yanga ikifanya kazi karibu na mdhamini wake GSM imemtangaza kocha Luc Eymail kuwa kucha mkuu atakaechukua mikoba ya mwinyi Zahera

Luc anauzoefu na soka la Africa na akiwa ametwaa mataji kadhaaa na vilabu tofauti.
Ametwaa ubingwa akiwa na AS Vita ya DRC Congo

Kocha huyo atatua Saa 8:30 mchana kiwanja Cha ndege Zanzibar kuungana na timu moja kwa moja kwenye michuano ya mapinduzi
View attachment 1316820
=====
Mfahamu Kocha Mpya Yanga Kwa Ufupi | .
:
✓ 26 August 2010, aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa AS Vital ya Congo .
:
✓ Msimu wake wa kwanza aliisaidia AS Vita kumaliza Juu ya Tp Mazembe na kuisaidia pia kushinda Super Coupe du Congo 2011. Pia aliisaidia kuifikisha Raundi ya pili ya michuano ya CAF Champions league. Aliweka Rekodi ya mechi 23 bila ya kufungwa na baadae 2011 April alijiuzulu kufundisha timu hiyo
:
✓ 2011, 1 Julai alijunga na Missile ya Gabon kama kocha mkuu, na aliisaidia timu hiyo kushinda taji lao la kwanza la ligi katika historia yao, pia akaisaidia timu hiyo kufika Raundi ya 16 CAF Confederation Cup na kupoteza goli kwa penati 0-3 dhidi ya JS Kabylie baada ya Aggr ya 3-3.
:
Timu Nyingine alizo zifundisha Luc ni
2013 - Leopard, 2014 - Rayon Sport, 2014/15 - Js Kairouan, 2015 - Al Nasr, 2015/16 - Al Merrikh, 2016/17 - Polokwame City, 2017/18 - Free state Star, 2018/19 - Talae's El Gaish, 2019 - Black Leopard.


Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee Luc ...y! 🙂 🙂
 
Kwa mtizamo wangu Charles Boniface mkwasa ni Kocha mzuri anaye wajua wachezaji wa kitanzania. Mkwasa ni Kocha msomi ambaye kwa bahati mbaya hajapata timu ya kufundisha nje ya nchi katika miaka ya hivi karibuni.Sidhani kama Yanga wamemfanyika sawa Kocha Boniface Mkwasa.



 
HUYU NDIYE CHARLES BONIFACE MKWASA
Mkwasa ni kiungo hodari wa zamani wa kimataifa nchini na mume wa mwandishi wa habari na mtangazaji wa zamani wa Redio na Televisheni nchini, Betty Chalamila Mkwasa aliyeng’ara RTD na baadaye Redio One na ITV.
Charles alizaliwa Aprili 10 mwaka 1955 mjini Morogoro, ambako alipata elimu yake ya Msingi na sekondari.Aliibukia katika timu ya Mseto FC ya Morogoro mwaka 1973 kama beki wa kati na kiungo hodari ambayo aliiwezesha kuwa timu ya kwanza kutoka nje ya Dar es Salaam kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania mwaka 1975.
1976 akahamia Tumbaku pia ya Morogoro aliyoichezea hadi mwaka 1979 alipotua Yanga SC, wakati huo ikiwa imepoteza makali yake kufuatia mgogoro mkubwa wa mwaka 1976 ulioigawa timu hiyo na kuzaliwa Pan Africans.
Baada ya nyota wengi wa Yanga SC kukimbilia Nyota ya Morogoro na baadaye kwenda kuasisi Pan Africans, timu hiyo ya Jangwani ikaanza kujiumba upya kwa kusajili nyota wengine, Mkwasa akiwa miongoni mwao.
Akiwa na chipukizi wenzake wa wakati huo kama Ahmad Amasha, Juma Mkambi ‘Jenerali’, Mkwasa waliiwezesha Yanga SC kurejesha makali na kutwaa tena ubingwa wa Tanzania mwaka 1981 tangu walipotwaa mara ya mwisho 1974.
Alidumu Yanga SC hadi mwaka 1989 alipoamua kutungika daluga zake za kuwa kocha mchezaji wa timu ya Super Stars ya Dar es Salaam. Lakini tayari mwaka 1988 alikwishaanza kupata mafunzo ya ukocha.
Baada ya kozi tatu za awali za ukocha Tanzania, mwaka 1991 Mkwasa alikwenda Brazil alipochukua Diploma na aliporejea akajiunga na Yanga SC kama Msaidizi wa Syllersaid Mziray (sasa marehemu).
Mkwasa ambaye mwaka 2000 alikwenda kusomea tena ukocha Ujerumani na kupata Diploma nyingine, kwa sasa ana leseni A ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) aliyoipata mwaka jana na pia ni Mkufunzi Daraja la Kwanza wa CAF tangu 2014.
Mbali na kufundisha Super Star na Yanga SC kuanzia 1989 hadi 1993, Mkwasa alifundisha pia iliyokuwa timu ya Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC), maarufu kama Sigara kuanzia 1994 hadi 1996 alipokwenda Al Khaboura ya Oman alikodumu hadi 1999.
Alirejea nchini 1999 na kuwa Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons ya Mbeya, ambayo mwaka 1999 aliipa ubingwa wa iliyokuwa Ligi ya Muungano.
Kwa mafanikio, Yanga SC wakamchukua kama kocha Mkuu mwaka 2001, akimrithi Raoul Jean Pierre Shungu kutoka DRC.
Aliifikisha Yanga SC hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika ikatolewa na Mamelodi Sundwons ya Afrika Kusini baada ya kufungwa 3-2 ugenini na kutoa sare ya 3-3 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Mwaka 2002 akahamia Coastal Union, 2003 akarejea Prisons alikodumu hadi 2005 alipohamia Moro United, kabla ya 2006 kuhamia Miembeni ya Zanzibar aliyoipa ubingwa wa Zanzibar na ubingwa wa Kombe la Mapinduzi mbele ya vigogo wa Bara, Mtibwa Sugar, Simba na Yanga SC.
Mwaka 2008 akawa Kocha wa African Lyon kwa msimu mmoja kabla ya kuhamia Ruvu Shooting alikodumu hadi 2013 alipokwenda Yanga SC kama Msaidizi wa Mholanzi, Hans van der Pluijm.
Mwaka jana baada ya msimu, akaondoka na Pluijm kwenda Al Shoolai ya Saudi Arabia, ambako hawakudumu, baada ya takriban miezi mitatu wakaacha kazi kufuatia kukerwa na kuingiliwa na uongozi wa timu juu ya masuala ya usajili.
Desemba mwaka jana yeye na Pluim wakarejea Yanga SC kumpokea, Mbrazl Maximo na mwishoni mwa msimu wakaipa timu ubingwa wa Ligi Kuu pamoja na kuifikisha hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika walipotolewa na Etoile du Sahel baada ya sae ya 1-1 Dar es Salaam na kufungwa 1-0 Tunisia.
Kwa mara ya kwanza kufundisha timu ya taifa ilikuwa ni mwaka 1993 alipoteuliwa kufundisha timu ya vijana chini ya umri wa miaka U17, kabla ya kuteuliwa kikosi cha pili Tanzania Bara, kilichopewa jina Kakakuona mwaka 1992, ambacho kiliwapiku ‘kaka zao’ Victoria 92 kwa kufika Fainali ya Kombe la Challenge, wakati huo akiwa Msaidizi wa Sunday Burton Kayuni.
Mwaka 2001 alikuwa Msaidizi wa Mziray chini ya Mshauri wa Ufundi, Mjerumani Burkhad Pape katika kikosi Taifa Stars kilichotwaa ubingwa wa Kombe la mataifa manne, Castle Cup.
Mwaka 2002, yeye na Mziray waliifiksiha timu ya Bara fainali ya Kombe la Challenge na mwaka 2007 akapewa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars kama Kocha Mkuu, lakini haikufanya vizuri baada ya kuambulia nafasi ya nne.
Mwaka 2008 akapewa timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars kama Kocha Mkuu ambako huko alipata mafanikio makubwa, ikiwemo kuiwezesha kukata tiketi ya Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2010, Fainali za Michezo ya Afrika 2011 na kuwa washindi wa tatu Kombe la COSAFA pia mwaka huo.
Mkwasa ni mshindi wa mataji ndani na nje ya Uwanja, akiwa anacheza alitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara 1975 na Mseto, 1981, 1983, 1985, 1987 na 1989 na Yanga SC, Ligi ya Muungano 1983 na 1987, wakati pia walikuwa washindi wa pili wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame mwaka 1986.
Huyo ni Mchezaji Bora chipukizi wa Tanzania mwaka 1975 na Mchezaji Bora wa Tanzania mwaka 1981.
Akiwa kocha, Mkwasa ametwaa mataji ya Ligi Kuu ya Bara katika miaka ya 1991, 1992, 1993 na 2015 akiwa na Yanga SC, Ligi ya Muungano 1991 na ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati mwaka 1993 mjini Kampala, Uganda.
Ametwaa pia Ngao ya Jamii mara mbili, mwaka 2001 na 2014 akiwa na Yanga SC- na amekuwa Kocha Bora Tanzania mwaka 1999 na 2005.
Huyo Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ kocha wa kwanza wa Taifa Stars mzalendo baada ya miaka tisa. Je, atarejesha furaha kwa Watanzania? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.
WASIFU WA CHARLES BONIFACE MKWASA;
KUZALIWA: 10 Aprili 1955 (Miaka 64)
ALIPOZALIWA: Morogoro, Tanzania
NAFASI: Beki/Kiungo
TIMU: Tanzania (Kocha Mkuu)
KLABU ALIZOCHEZEA:
Mwaka Timu
1973–1975 Mseto FC
1976–1978 Tumbaku
1979–1989 Yanga SC
ELIMU YA UKOCHA
1988: Kozi ya Awali
1989: Kozi ya Kati
1989: Kozi ya Juu
1991: Diploma (Brazil)
2000: Diploma (Ujerumani)
HADHI ZA KITAALUMA;
Ana leseni A ya CAF (Tangu 2014)
Ni Mkufunzi wa CAF (tangu 2014)
TIMU ALIZOFUNDISHA
1989–1991 Super Stars (Kocha Mkuu)
1991–1993 Yanga SC (Msaidizi wa Syllersaid Mziray)
1994–1996 Sigara (Kocha Mkuu)
1998-1999 Al Khaboura (Oman, Kocha Mkuu)
1999-2000 Tanzania Prisons
2001-2002 Yanga SC
2002 Coastal Union
2003 Tanzania Prisons
2005 Moro United
2006 Miembeni
2008 African Lyon
2008-2013 Ruvu Shooting
2013-2014 Al Shoolai (Saudi Arabia)
2014: Yanga SC
TIMU ZA TAIFA
1992-1993: Tanzania Bara B ‘Kakakuona’ (Msaidizi wa Sunday Kayuni)
1993-1994; Tanzania timu ya vijana U17 (Kocha Mkuu)
2001-2003: Tanzania Bara (Msaidizi wa Syllersaid Mziray)
2007-2008: Tanzania Bara (Kocha Mkuu)
2008-2013; Timu ya taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’, (Kocha Mkuu)
2015- Tanzania 'Taifa Stars' (Kocha Mkuu)
MATAJI TUZO:
WAKATI ANACHEZA; Ubingwa wa Ligi Kuu Bara; 1975 (Mseto), 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, (Yanga SC).
Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati; 1986 (Washindi wa Pili)
TUZO BINAFSI;
1975: Mchezaji Bora chipukizi Tanzania
1981: Mchezaji Bora Tanzania
AKIWA KOCHA;
Ligi Kuu Bara; Ubingwa 1991, 1992, 1993, 2015 (Yanga SC)
Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati; Ubingwa 1993 (Kampala, Uganda)
Ngao ya Jamii; Ushindi 2001 na 2014 (Yanga SC)
Kocha Bora Tanzania; 1999 na 2005
TIMU ZA TAIFA;
Ubingwa Kombe la Castle; 2001 (Taifa Stars)
Tiketi ya Fainali za AFCON; 2010 (Twiga Stars)
Washindi wa tatu COSAFA; 2011 (Twiga Stars)
Tiketi ya Michezo ya Afrika; 2011 (Twiga Stars)
 
Kama kweli Yanga wanahitaji mabadiliko na mafanikio uyu Mkwasa wasiwenaye mbali uhitaji ku pepesa, kila kitu cha mpira anacho katika CV yake. Tff watumieni Mkwasa, Kibadeni n.k kabla hawajawa Waze wa kushindwa kufanya lolote. Hizi ni hazina.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mtizamo wangu Charles Boniface mkwasa ni Kocha mzuri anaye wajua wachezaji wa kitanzania. Mkwasa ni Kocha msomi ambaye kwa bahati mbaya hajapata timu ya kufundisha nje ya nchi katika miaka ya hivi karibuni.Sidhani kama Yanga wamemfanyika sawa Kocha Boniface Mkwasa.



Wewe unajua soka..
 
Mleta Cv umesahau kuweka charles boniface mkwasa alicheza kwenye timu ya taifa iliyofuzu kombe la mataifa ya afrika nigeria 1980


Kwa maoni yangu huyu kocha mbelgiji mpya aliyekuja Hana jipya la kumzidi mkwasa
Muda Ndiyo mwamuzi
 
Back
Top Bottom