Yanga sasa imechokwa kwa kuombaomba.

Yanga sasa imechokwa kwa kuombaomba.

wazunguwawili

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2019
Posts
3,984
Reaction score
4,132
Huko mwanza hali sio shwari kwa wanajangwani. Sare dhidi pamba sio habari sana maana uwezo wa timu bado tia maji tia maji.

Hapa nazungumzia kuchangisha fedha taslimu tshs milioni 4 na ahadi za milioni 6.

Jumla ikiwa ni tshs milioni kumi.

Idadi ya watu wanaotajwa kuhudhuria ni takribani watu mia sita ( 600).

Kwa uwiano huu inaashiria huko kanda ya ziwa hasa kwa mashabiki wa yanga vyuma vimekaza hivyo hamna namna ya kubadili matokeo ama la mashabiki wamechoka na hii tabia ya omba omba.

Cc: vodacom na red logo yetu.
 
Hizi Club zinaweza kuishi bila michango hasa hasa zikitumia jezi vizuri na hata kuingia mkataba na makampuni ya nguo na bidhaa. Sema kwa sababu hapa ni Bongo ,basi sawa
 
Walioandaaa hiyo sherehe ni wanachama wa Yanga na sio uongozi. Hata timu kwenda Mwanza imepelekwa na wanachama wenyewe.
 
Hizi Club zinaweza kuishi bila michango hasa hasa zikitumia jezi vizuri na hata kuingia mkataba na makampuni ya nguo na bidhaa. Sema kwa sababu hapa ni Bongo ,basi sawa
Wameshajaribu huko na kuona kua sio rahisi kama tunavyofikiria.. Unahitaji kuwa na mipango na mitazamo hasi. Sio wasomi wazima wanakuja na argument ya Rangi za nembo. Kama plan ndio hizo hata Mzee wangu Akilimali angaweza kuongoza team bila ya shaka
 
Ivi kama ahadi zitatimia unadhani kwa timu ya Yanga mil 10,ni pesa ndogo?kumbuka hiyo milion kumi cash ukoo wenu mzima mnaweza kuchangishana hadi mkachawiana kisa mil.10.Mil 10 ukiamua kuilipa wachezaji kama posho inatosha sana.
Hao ni washabiki wachache tu wa Yanga mwanza.je,kila mkoa Tanzania wakitoa mil 10 ni milioni ngapi jumla.?
Yani mashabiki wa simba pesa za Mo zinawachanganya utadhani simba ndo inazalisha hizo pesa.
 
Wameshajaribu huko na kuona kua sio rahisi kama tunavyofikiria.. Unahitaji kuwa na mipango na mitazamo hasi. Sio wasomi wazima wanakuja na argument ya Rangi za nembo. Kama plan ndio hizo hata Mzee wangu Akilimali angaweza kuongoza team bila ya shaka
Nakupa mfano nadharia

Yanga wakiorganize na kampuni nzuri ya jezi zikatengenezwa jezi bora wakapanga bei ya laki na nusu kwa jezi nina uhakika Uhakika wa kuuza jezi laki mbili kwa kila mwaka upo

Hapo wakiwa wamekubaliana na mtengeneza jezi kuwa pasu mapato yanakuwa 75,000 *200000=15,000,000,000

Mapato ya Shilingi bilioni 15 kutoka kwenye jezi kila mwaka
 
Huko mwanza hali sio shwari kwa wanajangwani. Sare dhidi pamba sio habari sana maana uwezo wa timu bado tia maji tia maji.

Hapa nazungumzia kuchangisha fedha taslimu tshs milioni 4 na ahadi za milioni 6.

Jumla ikiwa ni tshs milioni kumi.

Idadi ya watu wanaotajwa kuhudhuria ni takribani watu mia sita ( 600).

Kwa uwiano huu inaashiria huko kanda ya ziwa hasa kwa mashabiki wa yanga vyuma vimekaza hivyo hamna namna ya kubadili matokeo ama la mashabiki wamechoka na hii tabia ya omba omba.

Cc: vodacom na red logo yetu.
Mtoa post mwaka 1989 ulikuwa na umri gani? Nauliza hivyo kwa sababu timu yako ya Simba ilikuwa ishuke daraja na RTC Kigoma ikaokolewa na Yanga. Leo unaibeza Yanga mwokozi wako? Nadhani ulikuwa hujazaliwa.
 
Nakupa mfano nadharia

Yanga wakiorganize na kampuni nzuri ya jezi zikatengenezwa jezi bora wakapanga bei ya laki na nusu kwa jezi nina uhakika Uhakika wa kuuza jezi laki mbili kwa kila mwaka upo

Hapo wakiwa wamekubaliana na mtengeneza jezi kuwa pasu mapato yanakuwa 75,000 *200000=15,000,000,000

Mapato ya Shilingi bilioni 15 kutoka kwenye jezi kila mwaka
Nafikiri unatania... Unazungumzia Yanga au Barcelona mkuu. Hivi kwenye ule ufunguzi waliuza Jezi ngapi? Na kila jezi ni bei gani? Na walipata kiasi gani?. Yanga na Simba hao hao washabiki wao wanaolalamika kiingilio cha Elfu 5 kwenye mechi..Washabiki wangapi wana ambao wanakipato cha laki moja kwa mwezi ambao wanaweza ku-save kununua Jezi bila kuharibu budget ya nyumbani. Hao Yanga ambao walifanya Harambee mwanza na kupata 5milion, na hizo dola 500 kachangia kocha Mwinyi Zahera... Hii ni utterly Nadharia.

Hata huyo Mwenyekiti Prof. Msolwa na Mwakalebela walifikiria hivyo. Ni watu wangu wakaribu, ila jaribu kuwauliza kuhusu mwitikio wa Wananchi katika kununua jezi!! Huu ni utani wa hali juu

Kuna kamari mbili ambazo huwa siwezi cheza. Kufanya biashara ya kwente makaratasi na kulima kwa kutumia simu...
 
Akili hana huyo.......yahn mahesabu yake hajapiga cost za TRA,material,kuwalipa wauzaj,frem na cost nyingne za biashara mpka hapo ishapungua sana tu...bado mahesabu yake ni chenga vilevile ...mauzo jerseys hayawezi endesha team hata siku moja.
Nafikiri unatania... Unazungumzia Yanga au Barcelona mkuu. Hivi kwenye ule ufunguzi waliuza Jezi ngapi? Na kila jezi ni bei gani? Na walipata kiasi gani?. Yanga na Simba hao hao washabiki wao wanaolalamika kiingilio cha Elfu 5 kwenye mechi..Washabiki wangapi wana ambao wanakipato cha laki moja kwa mwezi ambao wanaweza ku-save kununua Jezi bila kuharibu budget ya nyumbani. Hao Yanga ambao walifanya Harambee mwanza na kupata 5milion, na hizo dola 500 kachangia kocha Mwinyi Zahera... Hii ni utterly Nadharia.

Hata huyo Mwenyekiti Prof. Msolwa na Mwakalebela walifikiria hivyo. Ni watu wangu wakaribu, ila jaribu kuwauliza kuhusu mwitikio wa Wananchi katika kununua jezi!! Huu ni utani wa hali juu

Kuna kamari mbili ambazo huwa siwezi cheza. Kufanya biashara ya kwente makaratasi na kulima kwa kutumia simu...
 
Hizi Club zinaweza kuishi bila michango hasa hasa zikitumia jezi vizuri na hata kuingia mkataba na makampuni ya nguo na bidhaa. Sema kwa sababu hapa ni Bongo ,basi sawa
nafikiri CEO mpya wa Simba ameliona ndio maana anasema anataka kuwageuza wanachama wa simba na mashabiki kuwa wateja wa timu hiyo hasa baada ya kuona umati wa watu siku ya simba day
 
Back
Top Bottom