Tupo vizuri,maboresho tuliofanya dirisha dogo hili yamelipa vizuri.
Sasa shida tuliyonayo ni washambuliaji wa pembeni,ni wazi wamekua wakipoteza nafasi nyingi..
Kocha Nabi style ya sasa ya kutumia washambuliaji wawili ni nzuri,hii itatusaidia sana hata katika upatikanaji wa magoli mengi na nafasi zaidi.
Kumtumia Mayele peke yake kunafanya timu iwe na kazi kubwa katika kufunga kwa tabia ya mabeki wengi nchini kumzingira Mayele kila aendapo
Tupongeze uongozi kwa jitihada zote za kuimarisha kikosi na kweli tunazidi kuwa bora kila iitwapo leo
Sasa uongozi itumieni michuano hii ya CHAN inayoendelea huko Algeria kutuletea vijana wawili tu waje dirisha kubwa litakapofunguliwa...kule kuna vipaji vingi na kizuri wachezaji wale wote wanacheza ndani.
Nawasilisha.