Yanga SC 4-0 Dodoma Jiji | Benjamini Mkapa | Ligi kuu NBC

Yanga SC 4-0 Dodoma Jiji | Benjamini Mkapa | Ligi kuu NBC

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Katika NBC Premier League, leo tunafunga mwaka 2021 kwa mechi baina ya vinara Yanga Sc dhidi ya Dodoma Jiji FC . Yanga wanataka alama tatu ili waendelee kujikita kileleni mwa msimamo wakati Dodoma Jiji nao wanazitaka alama tatu ili wapanda mpaka nafasi ya tatu.

Mechi hi itapigwa katika dimba la Benjamin Mkapa kuanzia saa 1:00 usiku

Je, ni wananchi ama walima zabibu nani kuondoka na alama tatu?

Tuwe hapa Kwa Dakika 90

=======

00' Kabumbu linaanza dimba la Mkapa

01' Saidoo anaachia mkwaju mkali kutoka nje ya 18, mlinda mlango wa Dodoma anaukamata barabara

03' Yanga inapata kona kuelekea Dodoma Jiji, inasababisha madhara kwa mlinda mlango Hussein Masalanga wa Dodoma jiji baada ya kugongana na Fiston Mayele

06' Mayele anampita mlinda mlango wa Dodoma lakini pasi yake inashindwa kuleta matokeo. Yanga inatawala mwanzo wa mchezo.

08' Fei Toto anamuwekea pasi nzuri Fiston Mayele, mlinda mlango anafanikiwa kupangua shambulizi.

13' Dodoma Jiji wanaamka na wanajaribu kulizinga lango la Yanga

15’ Bado ni Bila bila

28' Yanga wanapiga kona ya sita, Mayele anapiga kichwa kinapaa juu ya goli

31' Almanusura Fiston Mayele aandike bao la kwanza, Masalanga anafanya kazi ya ziada langoni.

38' Mayeleee, Masalanga anauweka tena mikononi

40' Dodoma wanajaribu lakini wanashindwa

41' ⚽ Mayeleeeeeeee, pasi maridadi kutoka kwa Saidoo inamkuta Fiston na kuiandikia Yanga bao la kwanza

45+2' Mpira unaenda mapumziko, Yanga SC VS Dodoma Jiji

48' Fei Toto anapata nafasi lakini anashindwa kuitumia vizuri

54' Dodoma jiji wanafanya mabadiliko mawili kwa mkupuo

56' ⚽Jesus Molokoooo, akipokea mpira mrefu kutoka kwa Bangala na kuupanyeza langoni kwa Dodoma jiji Masalanga akishindwa cha kufanya

60' Kadi ya njano kwa Nkosi baada ya kumchezea ndivyo sivyo mchezaji wa Yanga

61' Saidoo anapiga mkwaju wa adhabu ndogo na kufika lango la Dodoma jiji, Masalanga anapangua

62' Mabadiliko tena Dodoma jiji, Karihe anaingia kuchukua nafasi ya Jamal

69' ⚽Mlinda mlango wa Dodoma jiji anajifunga katika harakati za kuokoa mpira usimfikie Fiston Mayele, krosi maridhawa ya Fei Toto

72' Makambo anachukua nafasi ya Fiston Mayele anayeonekana kuchechemea

74' Mukoko anaingia kuchukua nafasi ya Feisal Salum

82' ⚽ Dkt. Aucho anaweka chuma cha nne

84' Yanga inafanya sub za mkupuo akiwemo Sure boy

90+3' Mpira uanatamatika uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga SC 4-0 Dodoma Jiji

Kocha Mbwana Makata wa Dodoma Jiji amesema leo kulikuwa na makosa mengi kwa timu yao ikiwemo eneo la kiungo yaliwaruhusu Yanga kucheza na yamewagharimu.
 
Katika NBC Premier League, leo tunafunga mwaka 2021 kwa mechi baina ya vinara Yanga Sc dhidi ya Dodoma Jiji FC . Yanga wanataka alama tatu ili waendelee kujikita kileleni mwa msimamo wakati Dodoma Jiji nao wanazitaka alama tatu ili wapanda mpaka nafasi ya tatu.

Mechi hi itapigwa katika dimba la Benjamin Mkapa kuanzia saa 1:00 usiku

Je, ni wananchi ama walima zabibu nani kuondoka na alama tatu?

Tuwe hapa Kwa Dakika 90
KILA LA HERI WANANCHI YANGA
 
Anayeongoza ligi ataendeleza ubabe kwa goli 2-0 Feisal na Ntibazokiza
 
Back
Top Bottom