Yanga SC kushuka daraja mwakani!

Yanga SC kushuka daraja mwakani!

Quality Group Limited is Tanzania's largest conglomerate with 17 companies in the automotive, engineering products, international trade, logistic solutions and warehousing, real estate development, food processing, consulting, transport, aluminiumand fisheries sectors...Kawadanganye wanywa kahawa wenzako..kama ulikuwa hujui Manji ndio tajiri namba moja Tanzania... Quality Group ina thamani ya 13 Billion's... Tigo peke yake Manji anamiliki 99% ina thamani ya $ 1.4billion...Muulize Mo anavyomuogopa Yusuf.....alafu kuna jitu lingine lingine linaitwa Shubhash Patel hatari...wote wanarudi kundini 10 June....alafu Chirwa mchukueni hana hata footwork nzuri...Tshitshimbi hamuwezi kuvunja mkataba wake...
Kwenye list ya mabillionea wa africa Manji anashika nafasi ya ngapi?
au ndio hapendi kujionyesha.
 
ukiona MTU anatukana hana facts..
Yusuf Manji, the CEO of Quality Group Tanzania and one of the richest men in Africa, was born into a life of privilege. Highly intelligent and educated in the US he took over his family business and grew it into one of the most successful businesses in Tanzania

As a highly intelligent man, Yusuf Manji has been unable to refrain from going overboard, taking his family with him..Manji hawezi kuwekwa Forbes maana ni family business wewe kilaza...niambie kampuni moja ya Mo yenye thamani ya Tigo...... Ingia YouTube Mkasi ya Salama mwenyewe Mo alisema alienda kukopa bank South Africa $250m..billionaire anakopa????Mzee Dalali alilia Simba kuchukuliwa kwa 20B akatoa mfano wa Manji kuivalue Yanga 40 B..

Hujui biashara mkuu acha kupiga soga!
matajiri wengi hawatumii pesa kutoka mifukoni mwao kwaajiri ya kufanya uwekezaji.
 
Baada ya Azam FC kumalizana na Donald Ngoma na muda si mrefu wanaenda kumalizana na akina Thabani Kamusoko na Kelvin Yondani taarifa zilizonifikia hivi punde zinasema kwamba muda wowote Kiungo Papy Tshishimbi na Mshambuliaji Obren Chirwa wanasaini kuichezea Simba SC.

Je Yanga SC itakuwepo mwakani?

Poleni sana Yanga. Mlianza sasa tunamaliza kudadeki.

Mpaka mje mtuombe radhi Simba SC ndipo tunaweza kufikiria kuwasamehe ila nina uhakika kwa kuondoka kwa Ngoma, Kamusoko, Yondani, Tshishimbi na Chirwa tayari Yanga SC imeshashuka daraja rasmi katika Ligi Kuu ya msimu ujao wa 2018 / 2019.

Kama ambavyo mlitutesa Simba SC kwa akina Kelvin Yondan na Mbuyi Twite kupitia ' Tajiri ' wenu Yusuph Manji sasa nasi Simba SC kupitia si tu Tajiri bali ni ' Bilionea ' Mohamed Dewji sasa tumeamua kulipiza Kisasi na najua kuwa kwa taarifa hii ya Tshishimbi na Chirwa kusaini Simba SC muda wowote kuanzia sasa litakuwa ni ' Pigo ' moja takatifu kwa Yanga SC huku niamini kuwa muda wowote ule ' Bakora ' zitaanza kutembea pande za mitaa ya Twiga na Jangwani.

Wana Simba SC popote pale mlipo kaeni tayari kuwapokea hawa Wachezaji wawili akina Tshishimbi na Chirwa kwani tayari ' almost done deal ' na mliokuwa leo maeneo ya Posta karibu na Ofisi ya ' Bilionea ' kuna mambo mliyaona. Simba SC sasa hivi hatutanii na tunatumia Pesa kwa raha zetu na mtatutambua mwakani.

Simba SC 2018 / 2019
  1. Aishi Manula
  2. Shomari Kapombe ' Kiraka '
  3. Asante Kwasi
  4. Paul Bukaba
  5. Erasto Nyoni
  6. Jonas Mkude
  7. Haruna Fadhil Hakizimana Niyonzima ' Niyo Fabregas '
  8. Papy Kabamba Tshishimbi
  9. Obren Chirwa
  10. John Raphael Boko ' Adebayor '
  11. Emanuel Okwi
Kwa Kikosi chetu hiki Kipya cha Msimu ujao niwaombe tu TFF watukabidhi mapema Kombe letu kwani kuna uwezekano mkubwa sana Simba SC tukachukua ' Ubingwa ' zikiwa zimebaki mechi 15 huku idadi ya magoli yetu ya Kufunga yakiwa 203 na ya kufungwa yakiwa ni 0.

Nawasilisha.
Ok tusubirie tutaona
 
Kwa kikosi hicho lzm mfungwe tu

Papy ni kiungo mkabaji na mchezeshaji ni pure namba 6 mkimpa 8 ni kumtesa ila timu itakuwa slow kwa kuwa hana speed, mkude ni kiungo mchezeshaji hana uwezo wa kukaba sana na hana speed, niyonzima ni kiungo mchezeshaji hana uwezo wa kukaba na hana speed kwa hiyo itakuwa ni timu ya kizee maana haitakuwa na speed

Mkikutana na timu yenye speed mtafungwa sana
 
Sasa yanga ikishuka daraja utafaidika nini MKUU

Tunajua mlifanya figisu kwa kumtumia MKUU wa mkoa kummaliza jamaa

Sasa jiandaeni kumchangia si muda mrefu maana jamaa kashinda kesi

Vikaragosi nyie
 
wewe una akili sana, Gents n'a Manara akilimu zao zinafanana kumbe ? Sikulijua hilo.
Ila sio kikosi cha kushondana afrika hiki. Hakuna haja ya kuchukua wa yanga na umri umeenda. Uvuke boda na kuchukua majembe ya kushindana afrika.
 
mwenyekiti wa bodi ya ligi simba au hujui ndio makamu mwenyekiti wa yanga we jamaa acha upotoshaji
 
Wameshachelewa Mkuu. Hao ' Wapuuzi ' Yanga SC walitutesa na kutunyanyasa mno wakati wa Awamu ya mwana Yanga SC mwenzao na yule ' Tajiri ' uchwara wao wa Kihindi sasa na Sisi Simba SC huu ni wakati wetu ' Kuwatesa ' na kulipiza ' Kisasi ' hasa ukizingatia kuanzia Mzee Mzima wa Magogoni mwenye Awamu yake sasa, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge na Naibu wake, Waziri wa Michezo, 75 ya Baraza la Mawaziri la sasa ni Mnyama Mnyamani bila kusahau Rais wa TFF, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu nao wote ni wana Simba SC ( Mnyama Mnyamani )

Hapo nyuma nilikuwa siuelewi huu msemo wa Kizungu usemao " a one who laugh later laughs better " kwamba " achekae mwisho hucheka zaidi " ila kupitia hiki ambacho Simba SC imemua kukifanya na kujibu ' mapigo ' sasa nimeuelewa rasmi huo msemo.

Tutaheshimiana chini ya Awamu hii ya Tano na Uongozi huu wa sasa wa TFF Kudadadeki.

This is Simba!!!!!!!

Haya maandishi niyasome kikarismatiki au ninayasomesome tu....!
 
adui yako mwombee njaa....yanga mpigieni magoti mzee Mengi aje kuwaokoa....
Mengi Hana ufisadi?? Huwa hakwepi Kodi kweli?? Mnataka kumtia matatani mzee wa watu!

Simba tutatumia njia zote za kimafia kuhakikisha hi yanga inakufa in natural death au ishuke daraja kabsa!
 
hapo kwa yanga sion wa kuchukua,

tutulie simba, tuchukue damu changa, ina maana zile sampo za kina samatta hakuna hapa bongo?

hao tunao wachukua kutoka yanga wamefikia mwisho wa uwezo wao,,

hivi hamuon mambo ya TP mazembe wanavosajili?

pale simba bado sijaona wa kumshauri MO,
Hayo tutafanya mwakani, mission ya mwaka huu NI kuiua yanga kabsa, ikiwezeka tuinunue hiyo alafu tuishushe daraja kabsa, shenzy, huu NI umafiaaa!
 
Ila sio kikosi cha kushindana afrika hiki. Hakuna haja ya kuchukua wa yanga na umri umeenda. TUvuke boda na kuchukua majembe ya kushindana afrika.
Hawa tunawachukua ili kuiua yanga to basi ili mwakani washuke daraja! Huu NI umafiaaa
 
Kwa kikosi hicho lzm mfungwe tu

Papy ni kiungo mkabaji na mchezeshaji ni pure namba 6 mkimpa 8 ni kumtesa ila timu itakuwa slow kwa kuwa hana speed, mkude ni kiungo mchezeshaji hana uwezo wa kukaba sana na hana speed, niyonzima ni kiungo mchezeshaji hana uwezo wa kukaba na hana speed kwa hiyo itakuwa ni timu ya kizee maana haitakuwa na speed

Mkikutana na timu yenye speed mtafungwa sana


Hata Kikosi chetu cha Msimu huu kilichomaliza Ligi na kuwa Mabingwa mlikikosoa na kukiita cha ' Kihenga ' je matokeo yake yakawaje? Nasubiri majibu yangu tafadhali.
 
Kwa icho kikosi una maanisha kichuya hana nafasi tena ?

Kwani Mchezaji akianzia ' Sub ' huwa anakua mbaya? Hivi yule Mchezaji wa zamani wa Manchester United Ole Guna Solkjier alikuwa akianza au alikuwa akiingia akitokea Benchini? Na je alipokuwa akiingia kutoka Benchi alikuwa akifanya nini? Tatizo lenu msiojua mpira mnadhani Mchezaji kukaa au kuingia akitokea Benchi / Sub ni mbovu. Hebu jifunzeni ' modern football and style of play ' inavyokuwa na acheni Kukariri kama Uchezaji wa kizamani mliouzoea tafadhali.
 
Kwani Mchezaji akianzia ' Sub ' huwa anakua mbaya? Hivi yule Mchezaji wa zamani wa Manchester United Ole Guna Solkjier alikuwa akianza au alikuwa akiingia akitokea Benchini? Na je alipokuwa akiingia kutoka Benchi alikuwa akifanya nini? Tatizo lenu msiojua mpira mnadhani Mchezaji kukaa au kuingia akitokea Benchi / Sub ni mbovu. Hebu jifunzeni ' modern football and style of play ' inavyokuwa na acheni Kukariri kama Uchezaji wa kizamani mliouzoea tafadhali.
Mchezaj anapo anzia sub ina maanisha yey ni mbadala tu wa yule alieanza.
Ikitokea alie anza aka perform vizur basi uyu alie bench uwezekano wa kusugua bench unakua mkubwa. Mfano mzuri ni pale Santiago Gareth Bel yuko bench muda mwing Kwa kua Isco yuko kweny kiwango kizur . Gareth anapata nafsi pale tu ikionekana game imemshinda Isco au wako mbele kwa goli nyingi, Vinginevyo ana nafas.
Assume msimu ujao inatokea kichuya anagombania namba kama Gareth pale Santiago
Ki bongo bongo msim mmoja tu tunamsahau kabisa.
 
Back
Top Bottom