Tetesi: Yanga sc Kushusha Mbadala wa Aucho

Smart codetz

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2023
Posts
218
Reaction score
875
Klabu ya Yanga imeripotiwa kuwa ukingoni kukamilisha dili la kumsajili kiungo mkata umeme kutoka Ivory Coast, Djire Abdoulaye kutoka klabu ya Racing Club Abidjan. Young Africans SC inahitaji kiungo mwingine mkabaji haraka iwezekanavyo ikiwa ni pendekezo la kocha Miguel Gamondim

Abdoulaye (17) anatazamiwa kukubaliana pia masharti ya kibinafsi na Young Africans licha ya msururu wa vilabu kadhaa vikiwemo ASEC Mimosas na TP Mazembe vinavyowania saini yake.

Yanga SC inatarajia kuwasilisha ofa hivi karibuni ambapo zaidi dola 120,000 zinatarajiwa kuwatoka kwa ajili ya kuinasa saini ya kinda huyo anayefananishwa na Mohammed Zougrana ambaye alitimkia MC Algiers baada ya Wananchi kuzidiwa kete.

20231112_185607.jpg
 
Nilikuwa shabiki mkubwa wa Aucho ila utovu wa nidhamu awapo uwanjani umenivunja moyo.

Anafanya makosa ambayo huwezi kuyategemea kutoka kwa mchezaji pro kama yeye, mbadala wake sio mjadala tena... anahitajika haraka.
 
Nafasi ya kiungo mkabaji ni ngumu uwanjani
Tuliocheza mpira tunajua ugumu wake
Aucho ni bonge la kiungo akili kubwa

Kadi kwa kiungo ni za kufikia
Angalia akina na casemiro, kante, bosquet, Rice, xhaka, partey kumaliza mechi bila kadi ni ngumu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo hapati kadi za "kazi"ila ni za utovu wa nidham mf tukio la juzi dhidi ya Ajibu halikuwa na umuhimu kiasi Cha kupata kadi na hata Ile ya mwaka Jana
Anapaswa kurekebisha muenendo mbona Akaminko anajitahidi kuzuia hasira
 
Nafasi ya kiungo mkabaji ni ngumu uwanjani
Tuliocheza mpira tunajua ugumu wake
Aucho ni bonge la kiungo akili kubwa

Kadi kwa kiungo ni za kufikia
Angalia akina na casemiro, kante, bosquet, Rice, xhaka, partey kumaliza mechi bila kadi ni ngumu

Sent using Jamii Forums mobile app
Okay, ngoja tuchukulie mfano wa mechi iliyoniuma zaidi nusu fainali ya pili kule S.A Vs Marumo... Ile kadi ya kujitakia kwa kumbabua mchezaji vile na mpira tena nje ya uwanja ndio ugumu wa kiungo mkabaji?

Unajua pengo la Aucho ndilo lililotunyima kombe kwa kupoteza ile mechi ya kwanza hapa nyumbani?
Aucho hatufai tena, naunga mkono hoja ya kuletwa mbadala wake yeye atupishe.
 
Hii inaitwa mihemko... Umewahi kucheza hata mpira wa pete?, Unajua joto linapompanda mchezaji?. Yanga itachukua miaka 10+ kupata kiungo wa karba ya Aucho!!.
 
Okay, ngoja tuchukulie mfano wa mechi iliyoniuma zaidi nusu fainali ya pili kule S.A Vs Marumo... Ile kadi ya kujitakia kwa kumbabua mchezaji vile na mpira tena nje ya uwanja ndio ugumu wa kiungo mkabaji?

Unajua pengo la Aucho ndilo lililotunyima kombe kwa kupoteza ile mechi ya kwanza hapa nyumbani?
Aucho hatufai tena, naunga mkono hoja ya kuletwa mbadala wake yeye atupishe.
Kufaa bado anafaa ila akipata mbadala itakua poa zaidi
 
Back
Top Bottom