Mnao mshambulia
Nifah nadhani hamuelewi au mnajilazimisha kutokuelewa kwa ajili ushabiki maandazi uliowajaa. Msiwe na akili kama makolo bana, Aucho hana nidhamu na ni mwepesi kujaa upepo kitu ambacho sio sahihi kwa mchezaji wa level yake na umuhimu alionao kwenye timu yetu. Alikosa fainal ya pili dhidi ya USMA kwa ajili ya tukio la kipuuzi ila pia juzi kati dhidi ya Coastal almanusura ale umeme kwa ajili ya upuuzi. Badala acheze rafu zinazookoa timu anaenda kuwapiga watu viwiko mpira ukiwa umesimama, huyu ni proffessional au mswahili tu flani wa mpira wa vichochoroni?