Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Walikuwa Academy moja na Babu OnyangoUmri wake tafadhari!
Upuuzi mtupu kwani mnasajili kwaajili ya kucheza na Yanga tu?Kiingereza
Tanzania's Giant Club and VPL Champions Simba SC have lined up Kaiser Chiefs and Kenyan international midfielder Anthony Teddy Akumu as the perfect replacement of Brazilian Gérson Fraga Vieira who was ruled out of the season after sustaining an injury.
The Tanzania champions are currently in contact with Amakosi to sign the former Zesco United man in the January transfer window.
Kizanaki
Klabu Kubwa Tanzania na Bingwa wa Ligi Kuu Simba SC iko mbioni Kumsajili Mkabaji na wa Kimataifa Raia wa Kenya anayecheza katika Klabu Kubwa nchini Afrika Kusini ya Kaizer Chiefs kama mbadala sahihi wa Kiungo wa Brazil anayeenda Kuachwa kutokana na kuwa na Majeruhi Gerson Fraga.
Mabingwa hao wa Tanzania ( yaani Simba SC ) sasa wako katika Mazungumzo na Amakhosi ( Kaizer Chiefs ) ili Kumsajili Mchezaji huyo wa zamani wa Zesco United katika Kipindi cha Usajili cha dirisha dogo Mwezi January.
Chanzo: African Sports Today
Kama kuna Usajili ambao GENTAMYCINE nitaufurahia Simba SC wakiukamilisha basi ni wa huyu 'Kiungo' kwani anajua hadi anakera katika Kiungo.
Wadaawa FCCSubiri 'akishakufunga / akishawafunga' Yanga SC utawekwa hadharani Mkuu.
Kwan objective ya YANGA si kumfunga simba tu. Acha simba wasajili WACHUKUE MAKOMBEHuo usajili wenu hatusumbui kabisa mkuu sisi teacher Mukoko anatutosha!
Simba wasihangaike kusajili hii nafasi Fraga anatosha na alishazoea timu. Sehemu pekee ya kuumiza kichwa ni beki na strikerUONGOZI wa klabu ya Simba umefunguka kuwa, hauna pingamizi lolote la kumrudisha aliyekuwa Mkata umeme wao raia wa Brazil, Gerson Fraga Vieira ikiwa tu kocha mkuu wa timu hiyo, Didier Gomes atapendekeza usajili wake.
Mkata umeme huyo aliyehudumu ndani ya kikosi cha klabu ya Simba kwa msimu mmoja wa 2019/20 alipata majeraha ya goti mwanzoni mwa msimu huu na kulazimika kufanyiwa upasuaji wa goti Novemba 25, mwaka jana, ambapo Jumatano iliyopita alitakiwa kufanya vipimo vya mwisho vya MRI, kwa ajili ya kutoa ripoti ikiwa tayari amepona kabisa au la.
Licha ya kumalizana na Simba, Fraga ameendelea kuonyesha mapenzi na sapoti kwa klabu hiyo hususani kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram.
Baada ya Simba kutolewa na Kaizer kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Fraga aliwatumia ujumbe wachezaji wa Simba uliosomeka: “Tugange yajayo, najua marafiki zangu wamejitoa kwa asilimia 100 najisikia fahari kuwakilishwa na kila mmoja wa kaka zangu.”
Akizungumza kuhusu uwezekano wa kumrudisha mkata umeme huyo mkuu wa maudhui wa klabu ya Simba, Ally Shatry amesema: “Kuhusiana na Fraga tayari tulifikia makubaliano ya pande zote mbili ya kusitisha mkataba kutokana na sababu mbalimbali.
“Lakini hii haimaanishi kwamba hatuwezi kumsajili, kwa kuwa yupo katika hatua za mwisho za kupona anaweza kusajiliwa na kurejea Simba, kama tu atakuwa pendekezo la bendi la ufundi kupitia ripoti ya kocha mkuu, Didier Gomes kwa kushirikiana na kamati ya ufundi ya klabu yetu.
“Ni wazi Fraga mwenyewe bado anaonekana kuwa na mapenzi makubwa na klabu hii na ndiyo maana mara kwa mara amekuwa akitutumia ujumbe wa kututakia kheri na hata kuchapisha picha kwenye mitandao yake ya kijamii akiwa na jezi ya Simba.”
Source : SIMBA WAFUNGUKA ISHU YA KUSHUSHA KIUNGO MBRAZILI