Yanga SC vs Coastal Union

Hahahahaa. Kazi kweyi kweyi.

Kwani alikuwa anacheza Yanga au Simba mie sijawaelewa ujue?
Mkuu.. alikua anacheza Yanga SC dhidi ya Coastal Union. Yanga SC kashinda goli 1 (la offside tena ikiwa ni kwa taaabu sana).
Imagine hadi mpira unaisha, Yanga SC kapiga mashuti 2 tu katika lango la Coastal.. Umiliki wa mpira coastal kaongoza kwa 76% dhidi ya 24%.. Kwa kifupi jana timu nzima ya Yanga lazima watakua walilala na viatu.

NB: Mna bahati King Kiba alipata majeruhi katika mazoezi, lasivyo mlikua mnalala.
 
Hahaaaa. Hizi zako porojo tu Mkuu.

Sababu mwisho wa siku hazina nafasi katika msimamo wa ligi zaidi ya Point na magoli. Nadhani wanielewa Mkuu.
 
Hahaaaa. Hizi zako porojo tu Mkuu.

Sababu mwisho wa siku hazina nafasi katika msimamo zaidi ya Point na magoli. Nadhani wanielewa Mkuu.
Hahaha.. Labda nikuambie kitu, mi mwenyewe nafurahi sana hizi kauli zenu za cha muhimu point. Mmeshambuliwa dk karibia 70 alafu mnashangilia ushindi, kweli? Ingekua sisi masaa 48 baada ya mechi tungekua tunaomboleza.
Ila mnachokifanya kitatusaidia sana 30/09/2018. Palqe timu imara kabisa katika ligi ya msimu huu, Simba SC itakapokutana na timu dhaifu iliyokua ikipambwa na mashabiki + magazeti, Yanga SC.
 
Hahaaa. Sasa ulitaka tufanyeje Mkuu wakati point tatu tunazo kibindoni.

We tulia Mkuu haya unayoyaandika uje kuyaandika hiyo Septemba 30 na ndio naeza kwa mbaali nikajilazimisha kukuelewa sababu ntakutana na weye unayejiona una timu ya maana ambayo mpaka Ndada kakutoa kijasho. Teh teh teh
 
Hahahaaa. Kwani kwenye ile chart ya msimamo wa ligi kuna sehemu ya kujaza mpira mbovu Sesten? 😜😜😜
Yaani wewe waangalia magoli tu hutaki kuona ubovu wa timu yako, shauri zenu. Msije kusema hatukuwaambia siku ya siku halafu mkaanza kushikiana bakora mgogoro ukaanza upyaa
 
Baada ya matokeo ya Ndanda.. Tuliomboleza na kujiuliza sana kwa mda wa masaa 48. Ndani ya huo mda tulipata majibu, na leo tunayaleta kwenu mda wa saa 1 kamili usiku katika uwanja wa CCM Kirumba pale tutakapokua tukiwapa somo Mbao FC.

ANGALIZO: Refa atakapoanzisha mpira jitahidi uwe mbele ya TV yako.. maana kuna hatari baada ya dk 20 Mbao wakagoma kuendelea na mpira.
 
Yaani wewe waangalia magoli tu hutaki kuona ubovu wa timu yako, shauri zenu. Msije kusema hatukuwaambia siku ya siku halafu mkaanza kushikiana bakora mgogoro ukaanza upyaa
Sasa ndio timu tuliyonayo tufanyeje Sesten maana ndio tulipojikuna tukafikia hapo mnapopadharau.

Hahaaa. Kushikiana bakora si rahisi sababu timu inazidi kuimprove kila uchwao maana Yanga ya mwisho wa msimu uliopita si sawa na hii ya jana hivyo ni step tumepiga mpaka sasa na nina imani huko mbele itaimarika zaidi.
 
Hahahaaa. Unajua kujikaza kweli weye.

Hiki unachokiandika nitakicopy kama kilivyo after hiyo mechi sababu hapa umeandika kiushabiki na sio kiuhalisia wa game ya Simba na Mbao inavyokuwa Mkuu.

Vipo vitimu vya kusema vinaweza goma kuendelea kucheza ila sio Mbao Mkuu. Chukua hiyo. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Haya Hajar yetu macho tuombe uzima tu

Hebu usikilize moyo wako, ukiikumbuka tarehe 30.09.2018 haulipuki na kwnda mbio kwa hofu? Nahisi kama watamani isifike vileπŸ˜€
 
Hahaha.. Sawa Mkuu tukutane hapa saa 1 na dk 30 baada ya Mbao kuweka mpira kwapani.
 
Ulikuwepo taifa swahiba?
 
Hahaha.. Sawa Mkuu tukutane hapa saa 1 na dk 30 baada ya Mbao kuweka mpira kwapani.
Hahahaaa. Mie utaniona asubuhi sababu saa hizo nakuwa busy na mambo ya nyumbani ila usiache kunitag ili asubuhi cha kwanza nije kwenye huo uzi nikuone ulivyokimbia kivuli chako.

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ msalimie Ghazwat maana ulijua kumtag. πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Halafu mbona siwaelewi? Kipindi Simba ikishinda goli moja mnasema haitoshi. Leo (Jana) mmeshinda goli moja na mkawa mnapumua kwa mashine huku mkiomba gemu iishe mnasema muhimu pointi 3, inamaana umuhimu pointi 3 ni kwenu Yanga na sio kwa Simba? Au kwavile Simba SC ni Big Brand? [emoji123][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Unatumia nguvu nyingi kumwelewesha mtu anayejifanya haelewi wakati ukweli anaujua sana!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…