Yanga SC wanastahili kupata ushindi wa mezani kwa huu ujinga wa TFF.

denooJ

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2020
Posts
18,509
Reaction score
68,228
Salaam.

Kama Yanga wakiamua kudai haki yao ya pointi za mezani naona wana kila sababu ya kupata pointi tatu na magoli mawili.

Hii ni kwasababu walikidhi matakwa ya kanuni inayotaka wapeleke timu uwanjani Kanuni ya 15 (10) ya Ligi Kuu; muda wa mchezo uliopangwa, wakae dakika thelathini, kama mpinzani wao akiwa bado hajatokea basi waondoe timu yao uwanjani.

Simba SC hapa wameingizwa chaka na TFF, wamefuata tamko la TFF/ bodi ya ligi kuahirisha muda wa mchezo bila kuangalia kanuni zinasemaje, naamini Simba wakiulizwa kwanini hawakupeleka timu uwanjani watadai ni kutokana na tamko la TFF.

Lakini kwa bahati mbaya hilo tamko la TFF limekosa weledi wa kanuni za soka, wameahirisha muda wa kuanza mchezo bila kusema wametumia sheria/kanuni ipi kufanya hivyo.

Natumai hili tukio la leo litakuwa fundisho tosha kwa soka letu na wote wanaoliendesha, ni vyema kanuni na sheria za mpira zifuatwe kuamua hatma ya matukio ya uwanjani badala ya mamlaka husika kukurupuka tu na kujiamulia mambo pasipo kufuata sheria.
 
Kiukweli Mpira wa Tanzania na watanzania wenyewe hawajaamua kutumia weledi japo mie naipenda Simba Ila yanga niwapongeze kwa kutumia weledi wao vizuri.

Sitarajii kusikia Simba wakilalamika kupigwa adhabu Kali na kunyang'anywa point 3 na magoli 3.

Tuanze kufanya vitu kwa weledi Kama taifa ili twende mbali kimafanikio
 
Hapa anayeweza kupata point 3 ni Simba kama Yanga watasusa hiyo saa 1

Sheria za Mpira za kipuuzi sana. Ukifanyiwa rough then ukaretaliate vibaya, wanadeal na wewe uliyelipiza
 
Kuipa Yanga ushindi wa mezani itakuwa sio haki kwa Simba. Pia kama Yanga wasipoingiza team saa moja kuipa Simba ushindi wa mezani itakuwa sio haki kwa Yanga.

TFF pamoja na bodi ya ligi wanatakiwa wapigwe fine na FIFA kwa kukubali kupelekwa kisiasa kinyume na taratibu za FIFA.

Tunahitaji mtu awajibishwe iwe funzo siku nyingine.
 
Uwe na akil japo kdgo. Football la Tanzania liko mikonon mwa nan?
 
Daah wameharibu muda wa watu bure sidhan kwa ujinga huu kama Kuna mtu atahangaika Tena kwenda uwanjan
 
Bora yule jamaa yetu alikuwa anajipanga kitu kinakuwa planned Sasa huyu anataka awepo sehemu zote ona sasa.

Naomba tuwe tunashauriana kulingana na tararibu eti

Wizara ya habari imepelekea taarifa tff kuhusu kusogezwa kwa muda game ya Simba na yanga alafu tff ikawapa bodi ya ligi taarifa iwajulishe vilabu kuwa muda umebadilika alafu Sasa body ya ligi ndo ipeleke taarifa kwa klabu na kabla ya kupeleka taarifa bodi ya ligi Kama bodi sio mtu mmoja wanatakiwa kukaa na kutafsiri kanuni je Ni sawa ndo wawaite viongozi wa klabu wakae nao wote wakubsliane kwa sauti moja ndio waamue.

Kosa limefanyika hvyo kuanzia tff bodi yaligi wote wanatakiwa kujipima weledi wao kuwa bado wanafaa kuendelea kusimamia Mpira wa miguu Tanzania
 
Kanuni ya 15 (10) ya Ligi Kuu; muda wa mchezo uliopangwa, wakae dakika thelathini, kama mpinzani wao akiwa bado hajatokea basi waondoe timu yao uwanjani.
Ha ha haaa! Utopolo unachekesha! Kanuni gani inaitaka timu iondolewe uwanjani! Sio kwamba refa ndio atamaliza mchezo baada ya kumsubiri mpinzani kwa dakika thelathini? Je, hii mechi refa alikuwapo anawasubiri Simba wafike? Refa mwenyewe kwanza yupo uwanjani? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Sema sehemu kama hiz mwenda zake alikuwa anajua nini tunataka utasikia
"hiki kitabu mzee wangu kipo wacha kwanza wanachi wapate raha..."
 
Hawawezi kupewa kwa kuwa Kamisaa wa mchezo ataandika ripoti ya saa moja jioni na yanga wataonekana hawakuja uwanjani.
 
Faini n timu ya taifa ya Tanzania na vilabu vyake kutoshiriki michuano yoyote kwa miaka isiyopungua mitano na kuwafungia wote waliohusika kwani FIFA ilishaweka bayana kuwa serikali na Mambo ya Mpira ijitenge ya Mpira wawaachie wanampira Ni kwa maana njema Sana sema weledi wa watanzania wengi imekuwa finyu kuhusu hili
 
Nyie utopolo kama mmeshindwa kushiriki kimataifa kaeni pembeni sio mlazimishe timu zifungiwe kimataifa
 
Hapa hoja ni moja tu. Huyo aliyetoa maamuzi ya game kuhairishwa unless awe na mamlaka na sio mwehu mmoja tu.
 
Utopolo akili zenu zinafanana mmekimbia kipigo mnajua kabisa timu yenu ni mbovu mmenda kulobby serikalini kwani wanaohangaika na serikali ni nani ai nyie mnaojiita wananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…