denooJ
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 18,509
- 68,228
Salaam.
Kama Yanga wakiamua kudai haki yao ya pointi za mezani naona wana kila sababu ya kupata pointi tatu na magoli mawili.
Hii ni kwasababu walikidhi matakwa ya kanuni inayotaka wapeleke timu uwanjani Kanuni ya 15 (10) ya Ligi Kuu; muda wa mchezo uliopangwa, wakae dakika thelathini, kama mpinzani wao akiwa bado hajatokea basi waondoe timu yao uwanjani.
Simba SC hapa wameingizwa chaka na TFF, wamefuata tamko la TFF/ bodi ya ligi kuahirisha muda wa mchezo bila kuangalia kanuni zinasemaje, naamini Simba wakiulizwa kwanini hawakupeleka timu uwanjani watadai ni kutokana na tamko la TFF.
Lakini kwa bahati mbaya hilo tamko la TFF limekosa weledi wa kanuni za soka, wameahirisha muda wa kuanza mchezo bila kusema wametumia sheria/kanuni ipi kufanya hivyo.
Natumai hili tukio la leo litakuwa fundisho tosha kwa soka letu na wote wanaoliendesha, ni vyema kanuni na sheria za mpira zifuatwe kuamua hatma ya matukio ya uwanjani badala ya mamlaka husika kukurupuka tu na kujiamulia mambo pasipo kufuata sheria.