Wewe unafikiri Yanga hawajui ukomo wa madai wewe ndio unajua sana? Au kwamba wewe ni mwerevu kuliko management ya Yanga na kitengo cha fedha?
Labda nikupe wazo dogo tu. Kwenye uongozi wa taasisi yoyote lazima ujue uimara na udhaifu wa sheria na kanuni zinazowaongoza. Hii itakusaidia kwenye maamuzi wakati gani ulipe ama usilipe.
Mfano kwenye kesi nyingi timu inafungiwa kusajili mpaka madai ya wachezaji walipwe. Na unakuta mwezi inapotoka statement hiyo ni September dirisha la usajili liko January. Kwa nini ukimbilie kulipa wakati hizo pesa zinaweza kutumika kwenye shughuli nyingine za uendeshaji wa team then mwishoni mwa mwezi December kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa zinalipwa then unaendelea na usajili?
Fikiria madai haya yaliyoletwa hapa. Yanaitaka Yanga kulipa kiasi chote au kwa vipindi vitatu vinavyofuatana. Kwa nini usitumie udhaifu wa sheria hiyo kuanzisha taratibu za malipo mwezi December ili vipindi vingine vya malipo vianze mwaka mwingine na pesa zikatumika mahali pengine?
Kila kitu lazima kifanywe kwa manufaa ya taasisi si kwa manufaa ya watu nje ya taasisi.
TRA wanatoa nafasi ya kulipa corporate Tax kwa mkupuo au by Installments za hadi nne. Asilimia kubwa ya walipa kodi wanalipa kila robo ili pesa nyingine waizungushe izalishe pesa ya malipo mengine ya kodi. Uongozi sio kufanya payment kila muda . Viongozi wa Yanga wanajua wanachofanya. Lazima watafute fursa za kunufaika na udhaifu wa sheria na kanuni za FIFA au chama chochote cha mpira.