SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Yanga wamekuwa na tabia ya kuomba mechi zao ziahirishwe pale wanapokuwa na mfululizo wa mechi . Ni juzi juzi tu hapa tulikuwa tunajadili ni kwa nini mechi ya Yanga vs KMC iliahirishwa ilhali Yanga walikuwa wacheze na katimu kadogo ka ASAS Djibouti kwa mechi zote zilitakiwa kuchezwa Dar es Salaam wakati huo huo Simba akicheza uwanja wa Manungu, Morogoro halafu akarudi kucheza Dar es Salaam na Azam akicheza Dar akaenda kucheza Ethiopia.
Nimeiangalia ratiba ya AFL la kiukweli imebana saaana. Baada ya Simba kucheza mechi ya kwanza na Al Ahly, italazimika kusafiri na kurudiana nao baada ya siku nne tu. Kwenye nusu fainali nako ndiyo usiseme, mechi za marudiano ziko baada ya siku tatu tu. Kutoka mechi ya pili ya nusu fainali hadi mechi ya kwanza ya fainali ni siku 4 tu.
Kwa hiyo nawasihi uto washukuru kikombe hiki wamekiepuka. Kama ulimkimbia timu dhaifu kama KMC kwa kumuogopa timu nyingine dhaifu kama ASAS, ungeweza kweli kutoana jasho na miamba hii kwa ratiba ngumu kama hii? Ila nasikia mganga wenu yuko jikoni amesharusha jini mikwaruzano huko Angola inayotishia kuiondoa Atletico Petroleos de Luanda ili Yanga ichukue nafasi yake.
R.I.P legend, mshindi wa kwanza wa African Ballon D'Or, Salif Keita.