Yanga tumeshinda ila kwa Aziz Adambwile kocha umetudanganya

Wote mnaobisha humu mnapenda timu na sio mpira, huyo andambwile amepita na upepo tu , ila akijichanganya kwa waangola akamuweka lazima tuchezee chuma za kutosha, Simba zaidi ya mara 4 wamewafikia mabeki wetu wa mwisho in one against one situations,na mara mbili wamemfikia diarra.. holding midfielder sio kupiga vipasi tu ,nikuziba mashimo, kutembea right and left..nasio kusubiri mpaka mpira uchezwe eneo lako, holding midfielder hauwezi kupress, af tunakaa kumsifia??lakini pia , why Kocha alimruhusu mudathir acheze juu zaidi na sio kupartner na abuya katikati ya kiwanja??kulikuwa na gep kubwa baina Yao.. anyway jumapili sio mbali
Ni ukweli mtupu uliosema hapo
 
Yanga ikikaa pamoja miezi miwili na kocha akajua kuwatumia wachezaji wote kama nabi.
Huyu Simba tutafunga sana, na ubingwa tutachukua sana
 
Kuna mechi ya umuhimu tarehe 19 ya klabu bingwa pengine kocha kaamua ku save energy kwaajili ya hiyo mechi. Simba wao ratiba yao imekaa vizuri ya kupumzika hadi tarehe 21.
Nakubaliana na wewe 90%. Sema ni dharau sana kuwapangia Simba kikosi kile.
 
Coaches hamna paleee

Yanga poor performance huyo andambwile ndio hamna kitu kabisa eneo la kati kati limekufa kabisa halifai hata robo

Waliwaza nini kumuachia AUCHO !? Hata kama Alikuwa amechoka hawakupaswa kumuachia mazima wangekuwa Wana mtumia hata Kwa kutokea sub
 
Nikweli tumepata ushindi, lakini ukiangaliaa namna huyu Kocha wetu Folz alipanga timu , na namna alivyofanya substitution zake , ni wazi HAJUI kitu anafanya ..Aziz Andambwile alikuwa chanzo cha matatizo mengi ya Yanga sc, na kama isingekuwa ubora wa diarra tungekuwa matatizoni..

AZIZ Andambwile ni mzito sana, passing yake ni mbovu pia , lakini cha zaidi jamaa hatembei eneo kubwa la uwanja na anaganda tu kama pumbu ..pili timu ilikuwa inacheza bila mpango hasa kipindi cha kwanza , yote sababu ya andambwile..Kocha arudi nyuma ajitafakari tofauti na hivyo simuoni akifika November. Andambwile sio CAF champion league material, nakataaa katakata
Holding midfield unataka atembee eneo kubwa la Uwanja ?hapo tu hujui unachokitaka
 
Nimeangalia mpira kwa mara ya pili nikiwa nipo concentrated na adabwile hamna maajabu yoyote aliyofanya ni basi tu kocha amemwamini, Hana coverage kubwa, slow sana anatembea sana uwanjani na anapitwa sana na baadhi ya matukio,

Mabeki wetu wamefikiwa sana Jana basi tu walikuwa solid.
 
Coaches hamna paleee

Yanga poor performance huyo andambwile ndio hamna kitu kabisa eneo la kati kati limekufa kabisa halifai hata robo

Waliwaza nini kumuachia AUCHO !? Hata kama Alikuwa amechoka hawakupaswa kumuachia mazima wangekuwa Wana mtumia hata Kwa kutokea sub
Kocha hamna je amecheza michezo mingapi? Kwanzia apewe timu ana muda gani? Kocha ni mgeni na yupo katika hatua ya awali kabisa ya kuandaa timu mnakuja kuhukumu kama vile ana miezi mitatu na timu. Tujifunze kuwa wavumilivu, waliopo pale wote ni wachezaji wa Yanga hivyo ni kazi yake kuangalia ni nani atakayefaa kwenye mfumo upi na mbinu ipi. Bado yupo kwenye kujifunza juu ya wachezaji alionao hivyo inahitaji muda kutengeneza anachotaka. Ndio mechi ya kwanza hii ya mashindano na ameshinda dhidi ya opponent mgumu ambaye kikosi chake ni cha gharama na kocha wake ni mzoefu na timu na ni mzoefu na soka la Tanzania. Hilo tu ni jambo kubwa kwake
 
Nimeangalia mpira kwa mara ya pili nikiwa nipo concentrated na adabwile hamna maajabu yoyote aliyofanya ni basi tu kocha amemwamini, Hana coverage kubwa, slow sana anatembea sana uwanjani na anapitwa sana na baadhi ya matukio,

Mabeki wetu wamefikiwa sana Jana basi tu walikuwa solid.
umeongea vizuri, na uko sahihi sanaa
 
Kocha hamna je amecheza michezo mingapi? Kwanzia apewe timu ana muda gani? Kocha ni mgeni na yupo katika hatua ya awali kabisa ya kuandaa timu mnakuja kuhukumu kama vile ana miezi mitatu na timu. Tujifunze kuwa wavumilivu, waliopo pale wote ni wachezaji wa Yanga hivyo ni kazi yake kuangalia ni nani atakayefaa kwenye mfumo upi na mbinu ipi. Bado yupo kwenye kujifunza juu ya wachezaji alionao hivyo inahitaji muda kutengeneza anachotaka. Ndio mechi ya kwanza hii ya mashindano na ameshinda dhidi ya opponent mgumu ambaye kikosi chake ni cha gharama na kocha wake ni mzoefu na timu na ni mzoefu na soka la Tanzania. Hilo tu ni jambo kubwa kwake
Gamond alichukua team akiwa mgeni kabisa lakini ktk mechi yake ya kwanza tu balaa lake tuliliona licha ya Yanga kufungwa na Simba Kwa penalty lakini Mpira waliokuwa wanaucheza Yanga it was extraordinary
 
Nikweli tumepata ushindi, lakini ukiangaliaa namna huyu Kocha wetu Folz alipanga timu , na namna alivyofanya substitution zake , ni wazi HAJUI kitu anafanya ..Aziz Andambwile alikuwa chanzo cha matatizo mengi ya Yanga sc, na kama isingekuwa ubora wa diarra tungekuwa matatizoni..

AZIZ Andambwile ni mzito sana, passing yake ni mbovu pia , lakini cha zaidi jamaa hatembei eneo kubwa la uwanja na anaganda tu kama pumbu ..pili timu ilikuwa inacheza bila mpango hasa kipindi cha kwanza , yote sababu ya andambwile..Kocha arudi nyuma ajitafakari tofauti na hivyo simuoni akifika November. Andambwile sio CAF champion league material, nakataaa katakata
Hata timu ya darasa hujawahi fundisha.... Maumivu yakizidi muone daktari
 
Gamond alichukua team akiwa mgeni kabisa lakini ktk mechi yake ya kwanza tu balaa lake tuliliona licha ya Yanga kufungwa na Simba Kwa penalty lakini Mpira waliokuwa wanaucheza Yanga it was extraordinary
Kwenye mpira unaweza kushinda au kufungwa huku ukiwa na performance bora ama performance mbovu ama performance ya kawaida. Yanga jana ilicheza kwa kipindi kuna muda timu ilikuwa active halafu kuna muda ilipoteana ni ishu ndogo tu ya kuweka sawa upande wa kiungo. Kama itapatikana muarobaini wa hili timu itakaa sawa. Kwenye kuanza kila kocha ana mwanzo wake Gamondi alianza kwa performance nzuri ila hakupata matokeo ila huyu kaanza na matokeo mazuri. Tumpe muda kabla ya kumuhukumu
 
Back
Top Bottom