Yanga tuna la kujivunza kutokana na mafanikio ya timu ya Simba

Yanga tuna la kujivunza kutokana na mafanikio ya timu ya Simba

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
Ushindi wa mabao 2-1 walioupata Simba jana dhidi ya Vita Club umewapeleka robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Hakika wanastahili pongezi kwa mafanikio hayo

Watani zetu wametufundisha jambo kubwa sana, ili kuweza kufanikiwa tunahitaji uwekezaji wa fedha, akili, muda, hali na mali pasipo kukata tamaa

Kama Simba wangekata tamaa baada ya kupigwa zile dozi za tano tano sidhani kama wangekuwa na ubavu wa kushinda michezo yao miwili waliocheza nyumbani dhidi ya vigogo wa soka Barani Afrika.

Lakini pia nyuma ya mafanikio hayo yupo mwekezaji wao Mohammed Dewji 'Mo' ambaye alimwaga fedha za kutosha kutengeneza kikosi ambacho leo kimewafanya waweze kutembea kifua mbele.

Simba ndio klabu pekee kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya ligi ya mabingwa.

Wana Yanga yatupasa kupambana juu chini kuhakikisha nasi tunafanya mabadiliko katika timu yetu ili tuweze kuwavutia wawekezaji walete fedha.

Mpango huu wa kuchangia uliopendekezwa na kocha Mwinyi Zahera sio wa kudumu, utaisaidia Yanga kusimama wakati ikijiweka sawa.

Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji ndio kila kitu, kwani mabadiliko waliyofanya Simba tumeona jinsi yalivyokuwa na faida kwao.

Uwekezaji aliouweka Mo katika kipindi cha misimu miwili kwenye klabu ya Simba umekuwa na faida kubwa kwake na kwa Simba pia.

Kwa kutinga hatua ya robo fainali tu Simba itavuna zaidi ya Bil 1.5 fedha ambazo ni zaidi ya fedha walizotumia kukijenga kikosi chao(bil 1.3)

Ukiongeza na fedha walizovuna kupitia mashabiki ambao waliujaza uwanja wa Taifa katika michezo yote mitatu waliocheza jijini Dar es salaam pamoja na mauzo ya jezi, timu hiyo itakuwa imetengeneza fedha nyingi sana.

Simba wametuonyesha kumbe haya yote yanawezekana, ukijipanga vizuri na ukafanya uhamasishaji wa kutosha unaweza kufanya mambo makubwa kuliko wengi tulivyokariri.

Nani alitegemea kama Simba itaweza kuifunga Al Ahly, mabingwa mara nane barani Afrika? Al Ahly ambayo ilicheza fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu uliopita.

Nani alidhani kama Simba itapata ushindi dhidi ya Vita jana? Hawa Vita walicheza fainali ya kombe la shirikisho msimu uliopita.

Simba haikupewa nafasi ya kupenya katika kundi D lililozijumuisha JS Saoura, Al Ahly na Vita lakini wamepita.

Hivi kuna atakayeshangaa tena kama Simba itatwaa ubingwa wa Afrika? kwani hatua waliyofikia lolote linaweza kutokea.

Jambo la muhimu kwa Wana Yanga ni kupata somo kutokana na mafanikio haya. Kama hatua hazitachukuliwa, Yanga haiwezi kushindana na Simba katika nyanja zote.

Ni wazi msimu ujao huenda ukawa mgumu zaidi kupambana na Simba kwani watakuwa bora mara dufu kuliko walivyo sasa.

Sababu mpaka hapa walipofikia wameyajua mapungufu yao na tayari wanao ushawishi wa kumsajili mchezaji yeyote wanayemtaka kutokana uwepo wa fedha na mafanikio waliyopata.

Itakuwa muujiza kwa Yanga yetu hii kushindani na wenzetu ambao kimsingi mpaka sasa wameshatuacha mbali sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna vibabu vinavyojiita vyenye Yanga yao ndo havitaki mfumo wa kushare hisa za club. Vinanitia hasira kinoma, yaani Mimi wa kulala saa moja kisa Kilipuli.

Yaani sisi tunapigwa na Lipuli mtani anamfumua Mkongo!! Dunia haiko fair

Barafu la moto
 
Wachache sana katika hao uliowakusudia watakuelewa. Wengi wao ni wale wanaounga mkono timu yao ifungwe na Lipuli ili Simba naye afungwe na Vita.

Kila ulichokisema ni kweli na inahitaji kufikiri ili kuelewa wasiwasi wako.
 
Manji pia aliwekeza lakini hamkuweza kufua dafu kimataifa.
Kuna tatizo kubwa sana la 'Kisaikolojia' kwenye timu zetu.
Manji alizungukwa na wajanja wengi mno, Simba mtu wa kumshukuru sana ni try again huyu kwangu namuona ndio km shabiki namba 1 wa simba kwa kuweza kusimamia mabadiliko ya simba pasipo kuweka maslahi yake binafsi tena kwa kipindi kifupi mno alichoiongoza simba, Yanga tuna kila sababu kipindi hiki kumpata kiongozi mwenye mapenzi ya dhati kututoa hapa tulipo, bila hivyo itatuchukua muda sana.
 
Uzi mzuri kutoka kwa wanamichezo haswa.

Nasi simba bado tunajifunza zaidi toka kwa walio juu yetu. Kama mashabiki tunachangia mchango wetu. Tuwe na utaratibu wa kununua vifaa vinavyousiana na simba ktk maeneo husika. Mfano jezi tununue tunapoelekezwa na uongozi.
 
Fantastic one, but kuna vizee pale vikipitia uzi kama huu,kamwe havikuelewi, Vimekariri Negative tu all the time-hata kama akija mwekezaji bado vitajikusanya na kupinga kila kitu.

But all in all yawapasa wabadilike.

Sent from Nokia 7 Plus
 
Kuna vibabu vinavyojiita vyenye Yanga yao ndo havitaki mfumo wa kushare hisa za club. Vinanitia hasira kinoma, yaani Mimi wa kulala moja kisa Kilipuli!!!

Yaani sisi tunapigwa na Lipuli mtani anamfumua Mkongo!! Dunia haiko fair

Barafu la moto
mzee baba wewe siulikua mstari wambele kuitukana simba nakuishabikia As vita? Wakati mwingine msiwe mnatukana bali mjifunze kitu kwa simba kaka. Nimependa ulivyochangia leo.
 
mzee baba wewe siulikua mstari wambele kuitukana simba nakuishabikia As vita? Wakati mwingine msiwe mnatukana bali mjifunze kitu kwa simba kaka. Nimependa ulivyochangia leo.
Aisee nikweli nilishabikia As vita na hata akija nani Mimi siwezi shabikia Simba. Lakini kwa yanayoendelea kwa wenzetu natamani na sisi tufikie hatua ya kushare hisa ili tuwe watani kiukweli kweli lakini saizi mtani anatutesa balaa, kila tukiombea mabaya anatusua tu dah!!

Barafu la moto
 
Pole mtani, yatakwisha tu.

Ila badilikeni, sawa mtani?
Kuna vibabu vinavyojiita vyenye Yanga yao ndo havitaki mfumo wa kushare hisa za club. Vinanitia hasira kinoma, yaani Mimi wa kulala saa moja kisa Kilipuli!!!

Yaani sisi tunapigwa na Lipuli mtani anamfumua Mkongo!! Dunia haiko fair

Barafu la moto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom