Yanga vs Rivers United (0-1) | CAFCL | Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam

Yanga vs Rivers United (0-1) | CAFCL | Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam

Protect

Senior Member
Joined
Apr 4, 2020
Posts
103
Reaction score
362
UPDATES

00' Kipenga kinapulizwa kuashiria mwanzo wa mchezo na Yanga inaanza kwa kushambulia lango la Rivers, hata hivyo shuti linapaa juuu.

03' Rivers wanafika lango la Yanga, Adeyum katika jitihada za kuokoa anagongana kichwa na mchezaji wa Rivers

05' Ukwa Nelson anaingia lango la Yanga kwa kuwapunguza msururu wa mabeki, juhudi zake zinaishia hewani.

19' Almanusura Adeyum aweke goli kupitia mpira wa adhabu ndogo kuelekea lango la Rivers

20' Makambo anapiga shuti kali la chini na kutoka nje kidogo ya lango la Rivers

24' Makambo anataka goli kama alilowaweka Zanako lakini inakataa

28' Yakuba anashindwa kuandika bao la kwanza baada ya mpira kuponyoka mlinda mlango kwa kupiga kichwa fyongo

41' Rivers wanaingia kwenye lango la Yanga, shuti linatoka nje ya lango

45+2' Mpira unakwenda mapumziko

51' ⚽Moses anaiwekea Rivers bao la kwanza, Yanga 0-1 Rivers

64' Feisal Salum anapata nafasi ya kusawazisha baada ya Makambo kuuruka mpira lakini anapaisha juuu

85' Mlinda mlango anagagaa chini baada ya shuti kali kumpiga usoni katika harakati za kuokoa

90+4' Yanga wamelala nyumbani kwa kutandikwa 0-1 na Rivers United uwanja wa Mkapa Dar es Salaam, Tanzania. Wanatarajia kucheza mchezo wa marudiano nchini Nigeria.

Ili wasonge mbele wanahitaji ushindi nchini Nigeria au sare yoyote ya magoli inayozidi 1-1

=========

Screenshot_20210912-064829~3.png




Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Dar es Salaam Young Africans (Yanga) leo watashuka kwenye dimba la uwanja wa Benjamin Mkapa kupambana na timu ya Rivers United katika mechi ya kwanza ya hatua ya awali ya mashindano hayo

Baada ya mechi hii, timu hizo zitarudiana tarehe 19/09/2021 ili kuweza kupata mshindi atakayefuzu kwenye hatua inayofuata

Ungana nami nikikuletea kinachojiri katika mpambano huo

#RetunsOfChampions

Kikosi Cha Yanga

1. Diarra
2. Kibwana
3. Adeyum
4. Job
5. Mwamnyeto
6. Mukoko
7. Jesus
8. Mauya
9. Makambo
10. Feisal
11. Yacouba
 
Kila la kheri wawakilishi wetu wa Tanzania wanaocheza Leo Yanga, KMKM kwenye mechi zao
 
Yanga wanapaswa kumlazimisha kocha wao kufuta kauli ya kudai anajenga team. hiyo timu inahistoria kubwa sana. Kama hawezi wamuondoe
 
Yanga wanapaswa kumlazimisha kocha wao kufuta kauli ya kudai anajenga team. hiyo timu inahistoria kubwa sana. Kama hawezi wamuondoe
Mpira unaujua kweli wewe? Unajua ni nini maana ya kujenga timu? Je unajua ni kwanini kasema anajenga tumu?
 
Kila la Kheri Yanga, mtani msimu huu mna timu nzuri sana, naamini mtafika mbali kwenye haya mashindano na kuweka historia kwa timu za ukanda wa Afrika Mashariki.
Bado hawajawa na timu nzuri mkuu bali wana wachezaji wazuri tu.
 
Back
Top Bottom