Yanga vs Rivers United (0-1) | CAFCL | Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam

Yanga vs Rivers United (0-1) | CAFCL | Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam

Mkuu Kwa kiwango hiki mnachokionyesha leo,ugenini mnaenda Kula goli zaidi ya 3..jamaa wanatawala gemu Kama wapo kwao
Uko sahihi kabisa. Wachezaji wetu wamezoea kucheza na kelele za mashabiki. Leo Fei Toto siyo yule wa siku zote! Mukoko tangu alipo tuchomesha kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho, ameendelea kuwa yule yule!

Zawadi Mauya ni homa za vipindi! Anyway, labda vijana wanaweza kubadilika. Ila kwa hizi dk 45 za kwanza, nakubali tumecheza mpira wa kawaida sana ukilinganisha na wapinzani wetu.
 
Hivi Sukule la Taifa, limanara halijapata namba kucheza, naona silisikii kabsa, namsikia tu moloko, na makambo
Haji alikuwa anabebwa na ubora wa Simba.
Hii Yanga inaenda kutolewa round ya awali na mdomo wa Haji utakosa mvuto. Mwisho wa siku tutamsikia na kauli mbiu yake 'Mabingwa wa Mapinduzi cup, wamerejea kule walipopazoea- Mchangani'
 
Tupo vibanda umiza hapa tunaangalia mechi ya yanga vs river united. Kwa kweli yanga ni timu ya kawaida sana labda wabadilike kipindi cha pili .haina muunganiko mzuri mbele. Hawa wapinzani wao ni timu ndogo sana sijui wamefikaje champion league ni level tu ya ruvu shooting, gwambina, mbeya kwanza, singida united....nipo na wanazi wa yanga hapa wanaishangaa timu yao kuona hadi sasa hakun hata goli wala mpango wa goli. Labda tuangalie kipindi cha pili.

Yanga mna kazi ya ziada kwa timu hii.
 
Back
Top Bottom