Yanga waache kujipendekeza Zanzibar?

Yanga waache kujipendekeza Zanzibar?

Sijui Kuna uhusiano gani ukiwa Kolo na kuandika pumba Jf , wewe cheki nyuzi zao jinsi zilivyo za kiduwanzi..
 
Muasisi wa Yanga Mzee Karume ni mzinzibari hivyo Yanga kucheza Zanzibar ni kumuenzi , ni jambo zuri sana.

Yanga angalieni mchezaji striker mwenye uchu wa kufunga anaitwa LOKALE anacheza AFC Leopards ya Kenya. Huyu ni figher ana sifa za kucheza Yanga one day.
Yaani wewe ndo Bure kabisa. Yanga imeanzishwa mwaka 1935 huyo karume alikuwa na influence Gani huku Tanganyika? Unaelewa maana ya muasisi kweli?
 
Tukisema Maandamano mnaitukana CHADEMA saiv mnaanza Kubweka weka..haya yote source ni CCM.
 
Muasisi wa Yanga Mzee Karume ni mzinzibari hivyo Yanga kucheza Zanzibar ni kumuenzi , ni jambo zuri sana.

Yanga angalieni mchezaji striker mwenye uchu wa kufunga anaitwa LOKALE anacheza AFC Leopards ya Kenya. Huyu ni figher ana sifa za kucheza Yanga one day.
Karume ameiasisi vipi Yanga?
 
Hakuna timu inayojua kujipendekeza duniani kama Yanga. Kitendo cha kupelekea mechi Zanzibar ni dalili zote za shobo na kujipendekeza kwa Wazenji.

Nasubiria mapovu, nipo mtaa wa Lindanda hapa napata gahawa
Uko sahihi, siku hizi ni mtindo wa uchawa tu, kuanzia viongozi mpaka taasisi zote
 
Yaani wewe ndo Bure kabisa. Yanga imeanzishwa mwaka 1935 huyo karume alikuwa na influence Gani huku Tanganyika? Unaelewa maana ya muasisi kweli?
Influence ya AFRICAN ASSOCIATION.
CCM ni zao la ASP na TANU.
ASP ni zao la SHIRAZI ASSOCIATION na AFRICAN ASSOCIATION .
TANU ni zao la AFRICAN ASSOCIATION.
YANGA imesajiliwa 1935 lakini imeanzishwa 1926 kutoka na vuvuvugu la AFRICAN ASSOCIATION.
Kumbuka KARUME alizaliwa 1905, alimzidi NYERERE miaka 17.
Usichokijua ni kwamba maingiliano ya Watanganyika na Wanzibari hayakuanza 1964 yalikuwepo enzi na enzi, Muungano umekuja kuimarisha zaidi tu.
Nimekutafunia vya kutosha mengine tafuta mwenyewe.
 
Fuatilia Mpira ndugu. Nenda Jangwani pale watakupa majibu.
Kuliko kunitaka nifunge safari kwenda Jangwani kutoka huku nilipo ambapo mimi na wewe hatujui ni wapi, kuna shida gani wewe ukijibu hapa kwa faida ya wengi tujue ni namna gani gani Karume alishiriki kwenye uasisi wa Klabu ya Yanga mwaka 1935, wakati uasisi wa Yanga uliendana na harakati za Uhuru wa Tanganyika na ndiyo chanzo cha wengine kujitenga ndani na Yanga na kuanzisha timu yao ya Queens, ambayo baadaye ikaitwa Sunderland kabla ya mwishoni mwa miaka ya 60 kubadilishwa tena jina na Mwanachama wa Yanga alipoamuru iachane na jina la Sunderland kwa kuwa walipewa na wakoloni na iitwe Simba.
Ni vipi Karume alishiriki kuiasisi Klabu ya Yanga halafu hatajwi popote kwenye harakati za Uhuru wa Tanganyika.
 
Kikwete ni Rais mstaafu kupitia CCM ambaye ni mwanachama wa Yanga inayodhaminiwa na swahiba wake GSM mwenye ukaribu na Hangaya.
 
Back
Top Bottom