Yanga waliingia uwanjani kwa kuidharau Simba

Smt016

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2016
Posts
3,012
Reaction score
4,300
Mechi ya jana imeamulia na saikolojia ya wachezaji, nyuso za wachezaji wa Simba walikuwa na shauku kubwa sana ya kudhihirisha kitu mbele ya wapenzi wa mpira wa miguu ulimwenguni kutokana na kukosolewa kwao kuwa ni kikosi kibovu huku Yanga kwavile wanaongoza ligi na wamepoteza mechi moja tu wakiaminika kuwa ni bora zaidi. Hali ya kujiamini na kuchukulia mazoea ikaingia kwa mashabiki, wachezaji hadi benchi la ufundi.

Simba walijiandaa sana kiakili kwa hali ya juu hivyo ikawa ni rahisi kwa kuwa ndani ya mchezo katika game plan yao. Yanga kipindi chote cha kwanza walipoteana kabisa, akili zao zilikuwa hazijatulia, halafu wakawa wana mambo mengi mno uwanjani wakati wachezaji wa Simba walikuwa ni kwenda direct na kwa haraka golini kwa Yanga. Kutokana na kuwa na utulivu makosa kwa wacheza wa Simba yakawa ni machache kulinganisha na Yanga waliopotea mchezoni. Kilichowakuta leo ni kama surprise, na yote hiyo ni kutokana na kutokuheshimu mpinzani wako.

Kama hii mentality itabadilika, basi kule kwa Rivers Yanga itapigwa goli nyingi sana. Maana saivi kila mtu anamuonea Simba huruma huku wakijiona wao wapo semi, ila mambo yanaweza kwenda tofauti.

Mwisho namalizia kwa kusema, Yanga msimu ujao ubingwa wa NBC mnapaswa mjipange sana. Ukiangalia kikosi cha Simba kinahitaji tu kiungo mkabaji basi. Ila Yanga inahtaji wapishi wa magoli haswa na namba tisa ambaye asubiri nafasi kumi ndio apate goli moja.
Mods naomba msiunganishe uzi, hii ni tahadhari kuelekea mechi dhidi ya Rivers.
 
Simba bwana, ushindi kiduchu, kelele miingi!
Game za yanga ndo huwa ushindi kiduchu goli moja tu ila kwa simba 7,5,4,3,2,1.
Atleast ihefu walipokuja kwa mkapa walikaza wakafungwa 1. Ila nyie mmeshindwa kabisa kukaza mmepigwa kama wengine tu.
 
Na zile za Baleke zingeingia sijui Nabi angesemaje
Nimekasikiliza kale kazee ni kajinga kama mashabiki wa utopolo tu, yaani kaliingia kamejiamini sana ndo madhara yake haya, pia hayuko professional kabisa ni kama anamchukulia poa kocha wa simba while makocha wote huwa wanawaheshimu wapinzani.

Mashabiki wa yanga wamemjaza sana yule mzee na ndiyo maana kamechanganyikiwa baada ya kufungwa na soka safi lililopigwa na mnyama.

Ajifunze kuheshimu wapinzani, and this will happen the same kwa rivers united kitendo cha kushangilia kupangwa na wale jamaa ni cha ajabu sana.
 
Mtoa mada vp umedata?
Mechi ni ya leo au ya Jana?[emoji4]
 
Like it or Not......
Yanga hachukui Ubingwa.
Atafungwa na Singida away, ata draw na Mbeya City........
Baada ya hapo habari zinakuwa Nyingine kabisa.
Sijui ni nani kawahakikishia kuwa wao ni Mabingwa.
Naona ata kocha wao anasema Wao ni mabingwa.
 
Hiiiiiiiiiiiiii
In magu's voice
 
Like it or Not......
Yanga hachukui Ubingwa.
Atafungwa na Singida away, ata draw na Mbeya City........
Baada ya hapo habari zinakuwa Nyingine kabisa.
Sijui ni nani kawahakikishia kuwa wao ni Mabingwa.
Naona ata kocha wao anasema Wao ni mabingwa.
I can see it
 
Nimekasikiliza kale kazee ni kajinga kama mashabiki wa utopolo tu, yaani kaliingia kamejiamini sana ndo madhara yake haya, pia hayuko professional kabisa ni kama anamchukulia poa kocha wa simba while makocha wote huwa wanawaheshimu wapinzani.

Mashabiki wa yanga wamemjaza sana yule mzee na ndiyo maana kamechanganyikiwa baada ya kufungwa na soka safi lililopigwa na mnyama.

Ajifunze kuheshimu wapinzani, and this will happen the same kwa rivers united kitendo cha kushangilia kupangwa na wale jamaa ni cha ajabu sana.
 
Hawasikiagi hao mkuu yaani wako kama kenge ambae kusikia kwake mpaka damu itoke masikioni.
 
Mechi ya jana imeamulia na saikolojia ya wachezaji, nyuso za wachezaji wa Simba walikuwa na shauku kubwa sana ya kudhihirisha kitu mbele ya wapenzi wa mpira wa miguu ulimwenguni kutokana na kukosolewa kwao kuwa ni kikosi kibovu huku Yanga kwavile wanaongoza ligi na wamepoteza mechi moja tu wakiaminika kuwa ni bora zaidi. Hali ya kujiamini na kuchukulia mazoea ikaingia kwa mashabiki, wachezaji hadi benchi la ufundi.

Simba walijiandaa sana kiakili kwa hali ya juu hivyo ikawa ni rahisi kwa kuwa ndani ya mchezo katika game plan yao. Yanga kipindi chote cha kwanza walipoteana kabisa, akili zao zilikuwa hazijatulia, halafu wakawa wana mambo mengi mno uwanjani wakati wachezaji wa Simba walikuwa ni kwenda direct na kwa haraka golini kwa Yanga. Kutokana na kuwa na utulivu makosa kwa wacheza wa Simba yakawa ni machache kulinganisha na Yanga waliopotea mchezoni. Kilichowakuta leo ni kama surprise, na yote hiyo ni kutokana na kutokuheshimu mpinzani wako.

Kama hii mentality itabadilika, basi kule kwa Rivers Yanga itapigwa goli nyingi sana. Maana saivi kila mtu anamuonea Simba huruma huku wakijiona wao wapo semi, ila mambo yanaweza kwenda tofauti.

Mwisho namalizia kwa kusema, Yanga msimu ujao ubingwa wa NBC mnapaswa mjipange sana. Ukiangalia kikosi cha Simba kinahitaji tu kiungo mkabaji basi. Ila Yanga inahtaji wapishi wa magoli haswa na namba tisa ambaye asubiri nafasi kumi ndio apate goli moja.
Mods naomba msiunganishe uzi, hii ni tahadhari kuelekea mechi dhidi ya Rivers.
unajua timu yako ikishinda utasema kila aina ya maneno
 
Back
Top Bottom