Yanga walitakiwa kutumia mbinu aliyotumia Hayati Magufuli kwenye Makinikia

Yanga walitakiwa kutumia mbinu aliyotumia Hayati Magufuli kwenye Makinikia

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Kuna uhusiano mkubwa kati ya dhuruma na upole wa kimasikini.

Masikini mtata huwa anapunguza uwezekano wa kuonewa na Matajiri. I

Yanga kama hayati Magufuli ilitakiwa walete taharuki. Wagomee match wazue balaa ambalo litaleta attention ya FIFA na dunia nzima. Wamefanya kosa baya sana kukubali kuendelea na match. Dunia ya sasa haiitaji uungwana na upole wa kimasikini ( unprincipled politeness).

Kwenye suala la Makinikia JPM alilikuza na kuleta tahaluki kubwa katika dunia ya uchimbaji dhahabu kiasi kwamba wasomi wa madini walimuona kama amechaganyikiwa.

Huwezi kudeal na tajiri sirini au kwa barua. Unatakiwa kumuanika hadharani uovu wake ili dunia yote ijue na uzingatiwe. Chochote inachokifanya sasa hakuna atakayekizingatia. Walitakiwa kugoma, na kukataa kuingia uwanjani liwalo na liwe.

Ingesaidia pia nchi Yetu kujulikana duniani, Kama Magufuli alivyoleta taharuki kwenye Tasnia ya madini hadi tukaandikwa kwenye magazeti ya ulaya.

Kelele zote zinazoendelea sasa ni ujinga na kupoteza muda wa uzalishaji kitaifa.
 
Huoni tunavyopigwa za uso na hao MiGA?wazee hawakukosea kusema hasira hasara...yawezkana kuwa wangegomea ni kupigwa ban ya miaka kumi bila kishiriki hayo mashindano....lazma kufanya risk assessment kabla ya kua jambo..japo ukwel lile ni goli...watanii wamedhulumiwa kabisa
 
Haki Huwa inapiganiwa Kwa nguvu zote na siyo kusubiri huruma za mnyonyaji.Yanga badilikeni pamoja na wa Tanzania Kwa ujumla mkatae uhuni wa ccm unavyoiharibu nchi
 
Wachezaji na benching la yanga kama waliwahi kupoa mapema
Wangekuwa wamangaa pale pangechimbika

Ova
 
Mambo ya Trilioni 360 za makinikia 😁😁😁😁😁
Alizua taharuki duniani kwa kutaja grade za kwenye makinikia ambazo ukicalculate zinakuja tons za dhahabu ambazo hakuna migodi duniani imewahi kuzalisha.

Hiyo ilikuwa ni njia ya kuiambia dunia tunaibiwa kuna kitu hakiko sawa hata kama sikijui vizuri.

Hiyo kauli ilimshusha rais wa Bartick na matokeo yake leo Tanzania kupitia kampuni ya Twiga tunashare.

Pale ilitakiwa Yanga wasimamishe mechi, waanzishe mtiti mechi iahirishwe kabisa hata wakifungiwa sawa tu. Hiyo ingechallenge udhalimu wa kiburudani CAF. Na ingeleta mapinduzi makubwa ykatika utoaji haki kimpira Afrika.
 
Huoni tunavyopigwa za uso na hao MiGA?wazee hawakukosea kusema hasira hasara...yawezkana kuwa wangegomea ni kupigwa ban ya miaka kumi bila kishiriki hayo mashindano....lazma kufanya risk assessment kabla ya kua jambo..japo ukwel lile ni goli...watanii wamedhulumiwa kabisa
Sasa hivi wanatakiwa kupimq sana. Kwanza wasome sheria kwa kina na wajue loopholes ambazo hata ukileta ubishi haufungiwi.

Namaanisha itengenezwe taaruki ambayo itafanya hiyo dhuruma iangaliwe upya au ionekane waziwaazi kwa mapana kuna dhuruma imefanyika. Sio kusubiri hadi mpira uishe. Sasa hivi hakuna anayeizungumzia ukiacha wanaYanga wachache wanaojifariji.
Watu wanafikiria nusu fainali tu.
 
Hata wewe mtumishi na wewe umeshaachana na zile sera zetu za kugeuza shavu la pili baada ya kibao cha kwanza?
Mimi nimejifunza kwa Paulo. Aliwahi kudhurumiwa haki, ila waliomdhurumu walipojua wamekosea walitaka kumtoa lupango kimya kimya, akagoma hadi sheria ifuate mkondo wake. Jamaa hawakuamini kama mtumishi angewaanzishia timbwili. Soma kitabu cha matendo ya mitume.
 
Kwani baina ya Yesu na wanafunzi wake, kumbe tushike la nani?
 
Back
Top Bottom