Tetesi: Yanga walitibuana na Azam sababu ya Prince Dube Sasa wanatibuana na KMC sababu ya Moallin, KMC waapa kuwaonyesha wao ni nani

Mkakataba wa huyo kocha na Yanga mmeuona? Nini kinaizuia Yanga kusajili kocha kutoka kwenye timu yoyote? Kocha kaamua yeye mwenyewe kuvunja mkataba na wakafanya makubalino na kumruhusu. Yanga anahusikaje?
Kufungwa Camera kwenye vyumba vya kubadirisha nguo sio jambo geni. Shida ni muda wa matumizi wa hizo Camera. Wachezaji wakishaingia ndani ya vyumba vya kubadirisha nguo camera zinapaswa kuzimwa na kuwashwa wakitoka kwa ajili ya usalama wa mali zilizopo na hujuma zinazowezwa kufanywa.
 
Niliona Clip ya Mayor wa Kinondoni akilalamika kuhusu kitendo walichofanya Yanga.
Aliongea kwa hisia kama baba mwenye nyumba aliyeporwa demu mpangaji
Yaani tatizo imekuwa lama suprise kwa KMC,lazima iwaume,timu zote duniani zimezoea kufukuza makocha sio kuporwa
 
Wafunge hizo camera hadi toilet, na tukiona nao wanazingua tunahama. Yanga msiione tu, ina watu kila Idara, figisu zote za mpira wa kibongo, tunazimudu.
Waje na lingine, uwanja tutajenga kwa wakati wetu, si kwa mnavyotaka. Kila timu Yanga, Yanga, wivu tu kuona ni bingwa mfululizo. Na 2024/2025 tunabeba ili timu za figisu zipasuke.
#Yangabingwa#
 
Molin hajakubaliana na kmc kuvunja mkataba na wala hawajamruhusu anataka kuondoka kihuni bila kufuata utaratibu ndio maana kmc wanalalamika.
 
 
Molin hajakubaliana na kmc kuvunja mkataba na wala hawajamruhusu anataka kuondoka kihuni bila kufuata utaratibu ndio maana kmc wanalalamika.
Kocha kaandika barua ya kuondoka kakabidhi kwa wahusika kwa mujibu wa Mh. Meya wa Halmashauri ya kinondoni. Je mnajua sababu za kuondoka kwake alizoandika? Je unaweza kuniambia kuna utaratibu gani mwingine usio wa kihuni ambao angefuata tofauti na utaratibu aliotumia? Je mnaufahamu mkataba wa kocha Moalin na Kmc mpaka mmeseme anaondoka kihuni?

Kmc wamepokea barua ya kocha kuwataarifu kuondoka. Jambo lililotakiwa ni kujibu barua yake kama anaruhusiwa au haruhusiwi kulingana na terms zilizoko kwenye mkataba badala ya kukimbilia kulalamika kwenye vyombo vya habari.
 
Notice ya mwezi mmoja yeye katoa 24 hrs notice
 
Alitakiwa atoe notice ya mwezi mmoja kabla ya kuondoka.

Yanga walitakiwa waongee na kmc kwasababu moalini bado ana mkataba na kmc.

Hakuna sababu hata moja ya maana inayoweza kufanya mkataba uvunjike.

Yanga wangewacompansate kmc chochote kitu kama wanamtaka kweli kuliko kumuiba kihuni.
 
Hivi unachoandika unakielewa kweli? Daaah hii shida kwelikweli.
Michezoni hakuna kipengele cha notice ya mwezi mmoja mkuu. Mkataba unaweza kuvunjwa wakati wowote kwa vipengele fulani kukiukwa na upande mmoja wa walioingia mkataba, kwa makubaliano ya pande mbili au kukosa utimamu wa akili wa kufanya kazi au upande mmoja kuamua kuvunja kwa sababu inazoona inafaa kuvunja.

Kwani Yanga imemtangaza huyo kocha kuwa imemsajili au tunakisia? Tuseme ni kweli anaenda Yanga Wewe unafikiri kocha wa Kmc hakuona tobo la kutokea kwenye mkataba wake? Na kama kuna sehemu Yanga wamekiuka waacheni wapigwe adhabu. Sheria si zipo? Nyinyi mnaumia nini wakati hilo linatakiwa liwape furaha kama ilivyo siku zote?

Ukisema hakuna hata sababu moja inayofanya mkataba uvunjike hapo ndio napata shida juu ya uelewa wako wa mikataba

Kuhusu kulipa ada ya uhamisho wa kocha na si fidia iko ulimwenguni kote. Kama Kmc wanahisi wana mkataba naye na Yanga wanamhitaji warudi mezani hilo jambo litakuwa sorted. Lakini vipi kama kocha wa KMC mkataba wake wa awali unaisha December akaamua kusimama kazi sasa hivi ili ajiunge January na Yanga akiwa huru? Mbinu za kivita ni nyingi mkuu msilale upande mmoja.

Vipi kama kwenye mkataba wameweka kipengele cha endapo kocha akikiuka na kuicha timu atatakiwa kulipa fidia ya pesa ndogo kama 10M kwa mfano. Na Yanga wakaahidi kumpatia pesa hiyo kisha kumpa mkataba mnono Jangwani? Atakataa? Ungekuwa wewe unakataa? Haya ni maisha fursa haziji mara mbili. Udhaifu wa mkataba ndio unatengeneza matobo ya kutokea mkuu
 
Unajua KMC ni club na ni taasisi ya serikali mikataba ya watumishi wake uko katikati,kuna wakati inaofuata sheria za mpira kuna wakati inafuata sheria za ajira za nchi yetu,
Moallin inasemekana,sina uhakika ,aliajiriwa ba manisoaa ya Kinondoni kuifundisha timu yao,bosi wake ni Mkurugenzi wa manispaa sijui neya sijui,huko huwa hakuna siasa za kimpira kama mkataba ulisema ni one month notice lazima uheshimiwe unless otherwise,Whater the case mkataba wa kazi haulazimishi mtu kubaki kazini ila fuata utaratibu
 
Nafikiri sentensi ya mwisho ndio yenye maana. Hata hivyo tumemsikia kiongozi mmojawapo anayehusika na Kmc kuwa wamepokea barua ya kocha kutaka kuondoka na yeye anasubiri majibu ya barua yake, Je hapo hajafuata utaratibu? Ili aonekane amefuata utaratibu inatakiwa afanye nini tofauti na huu?
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…