Yanga wameharakisha mno kumtafuta mjenga uwanja

Yanga wameharakisha mno kumtafuta mjenga uwanja

Kujitolea bila makubaliano maalumu kwa anaejitolea kuweka wazi anataka nini kunaweza kuleta mgogoro baadae atakapotaka compensation ya kujitolea kwake. Nia njema inawezekana kabisa ikatendeka kwa kufuata utaratibu.

Kesi ya mudi na simba ipo hivi hivi. Jamaa alianza kutoa mzigo kabla ya makubaliano
Kwenye hizo timu wengi hujitolea tu. Hata wananchama huchangia chochote.

Mashabiki na wanachama wa hizo timu hawafanyi biashara.
 
Kwenye hizo timu wengi hujitolea tu. Hata wananchama huchangia chochote.

Mashabiki na wanachama wa hizo timu hawafanyi biashara.
Ingekuwa ni kujitolea pasipo maslahi hakika wangeshabwaga manyanga muda mrefu sana. Au ni lazima wangeharakisha mchakato wa mabadiliko ili mzigo majukumu yabebwe na wengi. Katiba ya Yanga tayari lakini imeishia kwa kutekeleza kipengele kimoja tu cha raisi wa timu lakini vipengele vyote vilivyobakia hawavitaki kuvikamilisha kwa wakati.

Yanga kuwa kampuni bado, thamani ya Yanga bado, wawekezaji zaidi ya mmoja na mgawanyo wa hisa bado lakini yote wanayafanya kwa kuchelewa ili GSM iendelelee kuwepo ndani ya Yanga. Kuna namna hawa watu wanapata maslahi kwenye biashara zao na upande wa serikali. Ndio maana Mo Dewji anatangaza kupata hasara ila swala la kung'atuka hataki.
 
Mpaka sasa GSM hajawa mwekezaji bali mdhamini na mfadhili.
Amekuwaje mwekezaji wakati mchakato wa uwekezaji haujakamilika?
Kumbuka ukikamilika wanatakiwa wawekezaji watatu au zaidi kwa mujibu wa katiba mpya.
Unaweza kuniambia GSM amewekeza asilimia ngapi na hicho kiasi ni shilingi ngapi?
Hapa umepotosha kwa kutojua au kwa makusudi.
Simba pekee ndiyo mwekezaji ameshanunua hisa 49% tayari.
Hakuna ishu ya wawekezaji kuwa watatu
 
Hakuna ishu ya wawekezaji kuwa watatu
Kisheria na kimfumo wa uwekezaji kwenye klabu ya Young Africans SC (Yanga), muundo uliopendekezwa na mamlaka za soka na serikali nchini Tanzania una mambo mawili muhimu:

1) Idadi ya wawekezaji

Uwekezaji wa asilimia 49% ya hisa haupaswi kumilikiwa na mtu mmoja pekee; unatakiwa kugawanywa kwa angalau wawekezaji watatu ili kuzuia kuhodhi klabu na mtu mmoja.


👉 Hivyo, kisheria/sera ya mabadiliko ya umiliki wa klabu:

Wawekezaji wa chini kabisa: 3

Lengo: kulinda maslahi ya wanachama na kuzuia mtu mmoja kudhibiti klabu.

2) Mgawanyo wa umiliki wa klabu

Muundo wa kisasa wa Yanga unaweka:

51% kwa wanachama/mashabiki wa klabu

49% kwa wawekezaji binafsi
Hii inalenga kuongeza fedha na ufanisi huku wanachama wakibaki na umiliki wa juu wa klabu.

✅ Hitimisho:

Kisheria/kimfumo, uwekezaji Yanga hauwezi kumilikiwa na mtu mmoja; unatakiwa kuwa na angalau wawekezaji watatu kugawana asilimia 49 ya hisa.

Wanachama wanabaki na asilimia 51, hivyo wanaendelea kuwa na udhibiti mkuu wa klabu
 
Ingekuwa ni kujitolea pasipo maslahi hakika wangeshabwaga manyanga muda mrefu sana. Au ni lazima wangeharakisha mchakato wa mabadiliko ili mzigo majukumu yabebwe na wengi. Katiba ya Yanga tayari lakini imeishia kwa kutekeleza kipengele kimoja tu cha raisi wa timu lakini vipengele vyote vilivyobakia hawavitaki kuvikamilisha kwa wakati.

Yanga kuwa kampuni bado, thamani ya Yanga bado, wawekezaji zaidi ya mmoja na mgawanyo wa hisa bado lakini yote wanayafanya kwa kuchelewa ili GSM iendelelee kuwepo ndani ya Yanga. Kuna namna hawa watu wanapata maslahi kwenye biashara zao na upande wa serikali. Ndio maana Mo Dewji anatangaza kupata hasara ila swala la kung'atuka hataki.
Yule jamaa wa Geita aliyetoa ng'ombe alipata nini??

Mashabiki wanaochanga pesa kila siku wanapata nini?

Wanachama wanaolipa ada kila mwezi anapata nini?
 
Back
Top Bottom