Yanga wamekopi mifumo ya siasa za nchi hii 100%Simba mkiwachekea watawachafua sana

Yanga wamekopi mifumo ya siasa za nchi hii 100%Simba mkiwachekea watawachafua sana

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,333
Reaction score
5,845
Sio jambo la ajabu kwenye siasa za nchi hii kuona mambo machafu ama meusi yakifanywa na upande wenye nguvu kisha zikatengenezwa propaganda ili washindani wao ndio wachafuke.

Huu mfumo timu ya yanga imeukopi kwa asilimia mia moja na kuuleta kwenye mpira wa Tanzania tangu uongozi wa sasa kuwepo madarakani.

Tulishuhudia hawa jamaa wakikimbia uwanja wa Azam kisa camera za Azam kunasa picha zilizoonesha mabomba ya sindano katika chumba walichotumia yanga.

Katika hali isiyo ya kawaida,timu hii ilipofungwa goli 2 kipindi cha kwanza,walienda kwenye "jumba la maajabu" kwa visingizio kuwa kuna dawa wamepuliziwa na mpinzani wao ( Simba) kwenye chumba cha kupumzikia.Lakini hata hivyo walirudi uwanjani na uwezo tofauti na wa mwanzo huenda ni kwa sababu walitumia mbinu ile waliyozoea kuitumia.

Leo msemaji anaposti picha yenye utata ili kuanzisha mjadala wa kuichafua Simba kwa kuposti bomba la sindano kuashiria eti Simba walienda SA kuchoma dawa za kuongeza nguvu!

Hii tabia wanayo wao na ushahidi ulikuwepo baada ya zile picha za kule Azam complex.
Lakini sasa wanataka kuipakazia Simba wakijua Simba wapo kwenye furaha watapuuza kujibu tuhuma hizi

Mi nawaambia Simba waache kupuuza hizi tuhuma kwani zinachafua brand ya Simba.Ikibidi wote wanaojaribu kufanya hivi,Simba iwachukulie hatua,wakathibitishe wanachokieneza.Vinginevyo hata ligi hii mnaichafua sana kisa yanga kufungwa.

Yanga hii imekuwa ikiponea chupu chupu kufungwa na Simba rejea kule Aman ambapo walikuwa na shot on target moja tu kwa dk 90.

Rejea mechi ya Geita gold walivyoponea chupu chupu kwa msaada wa mwamuzi walishinda mechi ile.

Yanga acheni siasa chafu kwenye soka chezeni mpira.Tabia ya kujinasbisha na chama cha siasa "kisichoshindwa" ni mambo ya hovyo sana
 
Viongozi waliopo Simba wanqchojua ni kugombania madaraka sio ynga tu kuna mwamuzi aliwahi kuandika kwenye gazeti la mwanaspoti kuwa Simba ilihonga mchezaji wa yanga lakini wao wamekaa kimya bila kujali brand ya timu inachafuliwa.
 
Yaani hili povu ni kwa ajili ya picha tu na hakuna tamko lolote....pole sana!
 
Umeandika porojo kama vile unawaambia watoto wa chekechea..
Kama ushahidi unao wa Azam umeshindwa nini wewe kuuweka hapa?
 
Kuna mtangazaji kipindi cha michezo RFA anasisitiza kuna tatizo kubwa kwa wachezaji wa ligi yetu kutumia madawa ya kusisimua misuli.
Tena yeye amesema zaidi ya 50% wanatumia madawa.
Viongozi wa TFF msipomtaka huyu mtangazaji kuthibitisha,nitawashangaa sana.
Hii nchi ndiyo inaandaa Afcon,halafu mnaruhusu waandishi kuzusha hii propaganda kisa yanga amefungwa,mtakuwa watu wa ajabu sana
 
Simba iwachukulie hatua,wakathibitishe wanachokieneza.Vinginevyo hata ligi hii mnaichafua sana kisa yanga kufungwa.
Mahaba yamezidi uwezo wa kuchanganua mambo.
Ali Kamwe hajataja timu wala taasisi yeyote au mtu binafsi yeyote kwenye Ile picha. Sasa hao viongozi wako wa Simba waamshtaki Ali Kamwe kwa ushahidi gani kaichafua timu yenu?
 
20260221_140351.jpg
 
Back
Top Bottom