Yanga wameliingiza jina la Morison katika mfumo wa usajili

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,420
Reaction score
18,298
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dkt. Mshindo Msolla amethibitisha kuwa wameliingiza jina la kiungo mshambuliaji Bernard Morrison katika mfumo wa usajili wa wachezaji wa klabu hiyo (Transfer Matching system) na wamepeleka katika Shirikisho la soka la Barani Afrika na Shirikisho la soka la Dunia (FIFA).

Msolla amesema kuwa Kiungo huyo ni Mchezaji wao halali na hukumu iliyotolewa na Kamati ya (TFF) haina Uhalali wowote.

Msola amesema Jumatatu watatuma shauri la mchezaji huyo shirikisho la soka Duniani FIFA na ikiwa shirikisho hilo litamuidhinisha kuwa ni mchezaji wa Yanga, basi itawalazimu Simba waende mezani wakamalizane nao.

Orodha ya wachezaji wa Kigeni yaliyoingizwa katika mfumo wa TMS: Farouk Shikalo, Mukoko Tonombe, Michael Sarpong, Tuisila Kisinda, Haruna Niyonzima, Lamine Moro, Yacouba Sogne, Carlinhos Carmo na Bernard Morrison.

HII TAARIFA MNAONAJE?
 
Yanga wapo sahihi kabisa,na huyo morrison atafungiwa
 
Nilijua tu goli la jana la BM ni lazima utopolo wataliamsha dude.Viongozi wa Yanga wanaamisha magoli ili kuwazuga mashabiki.
Nashauri BM asiwe anacheza pale Simba awekwe benchi.maana kilaatakapocheza kule jangwani bundi atakuwa anaamka.
 
Yanga wanajua hawawezi shinda. Wanachofanya hapa ni kutuliza aibu mbele ya mashabiki, kumzuia Morrison asicheze msimu huu mpaka hukumu itoke, kuendeleza mpira wa maji taka.
 
Sasa jamaa inawezekana yuko smart lakini simba kumchezesha itakwaje mbona itakuwa kama ishu ya kubahatisha
Huyu jamaa ni smart kichwan na anajua anachofanya,mshindo msolla wanatuliza tu mashabiki na kuwadanganya, km ile ishu ya simba na point 3 za kagera
 
Kama ni kweli Yanga wamepeleka kesi CAS na FIFA basi wawe na uhakika na wanacho kishtaki kuwa ni ukweli na hakuna ubabaishaji walioufanya. Pili wanasheria wa Yanga wawe wamejipanga ipasavyo maana wanapambana na Morrison, Simba na TFF kwa pamoja.

Kitendo cha kutoa taarifa hiyo kwa mashabiki wao maanake wamejipa deni kwa mashabiki wao kutaka kujua muendelezo wa kesi huko CAS na FIFA.
 
FIFA kumfungia mchezaji huwa ni ngumu sana kwa kuhofia kiwango cha mchezaji kisishuke mwisho wa siku ni Morrison kuchagua timu ya kucheza na jana kasema kuna time flani ni university of football

Rejea kwa buswita

Kwani anaeidhinisha usajili ni nani FIFA, tff, au timu husika.

Kamati ilitambua mapungufu ya mkataba ikasema inampa faida Morrison na FIFA haiko tayari kukurupusha na wanachama wake ambao ni tff,. Na yakifukuliwa sana makaburi ya mkataba huo kuna timu itacheza SDL

Atachelewa ndio mwisho wa siku atachezesha simba.
 
Haya ni mawazo yako, huyo anarudi na atakuwa anawekwa benchi mpaka awe na adabu nzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…