Yanga wameshindwa kumbakiza Ngassa

Yanga wameshindwa kumbakiza Ngassa

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
Huyu jamaa kiukweli anaipenda sana yanga, lakini viongozi wa yanga hawakuona umuhimu wa kumthamini wakati akiwapigia magoti wamlipie deni lake crdb bank.

sasa kagoma kusain mkataba mpya na ndani ya masaa48 atatimka kwenda kuanza maisha mapya bondeni(platinum fc)swali ni jee?!!viongozi wa yanga wameshindwa kumbakiza kweli jamani?mbona timu inabomoka sasa?msuva yuko bondeni na kwa mujibu wa meneja wake anasema atafuzu majaribio.niyonzima anaenda sudan na atatimka mwezi7, sasa ngasa nae huyo!!

mbaya zaidi ngassa na niyonzima wanaondoka free!!!!hii inaniuma sana.....na haya yote ni kutokana na ubabaishaji wetu.eti ngassa kashuka kiwango na hastahili kulipiwa deni,sasa mbona mnampigia magoti leo?kila la kheri ngassa,mpira ndiyo maisha yako nakuunga mkono."wakisema wa nini kuna ambao wanasema watakupata lini"
 

Attachments

  • ngassa+aga.JPG
    ngassa+aga.JPG
    25 KB · Views: 505
Aende tu,aliondoka kwenda azam tukabeba ubingwa, we will always love ngasa thanx bye
 
Ngoja akajaribu na huko...na akope tena hao platinum fc watamlipia!
 
Aende tu,aliondoka kwenda azam tukabeba ubingwa, we will always love ngasa thanx bye

kweli mkuu yeye aende tu...kabla yake Yanga ilikuwepo na ilikuwa ikitwaa vikombe...baada yake Yanga itaendelea kuwepo!
 
namsubiri Msuva wa milioni 700 kama kweli atafikia thamani hiyo mkwara wa Hanspope umewafanya yanga waone bora akacheze nje
 
Kuna siku nilitumiwa clip ya Ngassa akiwa anahojiwa ugenini (nadhani ilikua kwenye game ya taifa stars) nilicheka sana.Ajifunze na lugha kabisa kabla ya kutimka.
Tunamshukuru kwa mchango wake, kila la kheri.
 
Dah!!!
Wabongo hatuna shukrani kabisaaa!!
 
Ngasa tutakumiss Yanga ila kwa vile unaenda bondeni tunakutakia kila lakheri kwani mpira ndo ajira yako.
Ila ungekuwa unaenda Mikia fc ungetuumiza sana wanayanga.
 
Last edited by a moderator:
kuna siku nilitumiwa clip ya ngassa akiwa anahojiwa ugenini (nadhani ilikua kwenye game ya taifa stars) nilicheka sana.ajifunze na lugha kabisa kabla ya kutimka.
Tunamshukuru kwa mchango wake, kila la kheri.

nadhani kama sikosei ilikuwa challenge ya mwaka 2007 kama sio 2008 ilifanyika rwanda na kipiindihicho aliibuka top scorer alikuwa anahojiwa na presenter wa dstv,alafu jamaa alimuhoji maswalisimple sana kama ya mtoto wa primary na alikuwa nauwezo wakujibu maneno hata mawili au matatu sema ndio ivo sasa..nadhani atakuwa amepata kitu fulani mpaka sasa naamni anaweza kucontact nawasio waswahili japo wakaelewana
 
nadhani kama sikosei ilikuwa challenge ya mwaka 2007 kama sio 2008 ilifanyika rwanda na kipiindihicho aliibuka top score alikuwa anahojiwa na presenter wa dstv,alafu jamaa alimuhoji maswalisimple sana kama ya mtoto wa primary na alikuwa nauwezo wakujibu maneno hata mawili au matatu sema ndio ivo sasa..nadhani atakuwa amepata kitu fulani mpaka sasa naamni anaweza kucontact nawasio waswahili japo wakaelewana

Hahahahaaa umetisha sana! Ndio hiyo hiyo...ze God is good it will help me!...lol
Usione ajabu kusikia kua bado mambo ni yaleyale maana kwa wachezaji wetu hawa hilo sio ajabu na wala hawaipi elimu kipaumbele.
 
Kuna siku nilitumiwa clip ya Ngassa akiwa anahojiwa ugenini (nadhani ilikua kwenye game ya taifa stars) nilicheka sana.Ajifunze na lugha kabisa kabla ya kutimka.
Tunamshukuru kwa mchango wake, kila la kheri.
kwani anakwenda kufundisha lugha?!! lugha ya ki mpira sio ki vile sana, pole pole tu ataelewa huko huko, Yaani afauru majaribio ashindwe kwenda kisa lugha?!!
 
kwani anakwenda kufundisha lugha?!! lugha ya ki mpira sio ki vile sana, pole pole tu ataelewa huko huko, Yaani afauru majaribio ashindwe kwenda kisa lugha?!!

Nimeongelea umuhimu wa kujifunza lugha tu.Mbona kuna wachezaji kibao tena maarufu na lugha ilikua/bado inawapiga chenga?
Kama sikosei nakumbuka Sir. Alex Furgerson aliwahi kusema kua Vidic alikua anampa shida sana kwenye kuelewana maana alikua hajui kiingereza vizuri.
Ndio maana nikakumbushia na hilo suala la lugha kwa Ngassa.
 
binafsi Kiroho safi nlikuwa natamani aondoke YANGA akajaribu na changamoto zingine sehemu nyingine maana amecheza timu zote tatu kubwa Za hapa...kila lakheri ngasa Mungu akutangulie na kila jema liwe lako
 
Yanga mlipieni hizo 45M abaki kucheza bure, anaipenda sana Yanga. Mwenzake Msuva mwenye damu ya Msimbazi ana mkataba bado lakini ametoroka kwenda kufanya majaribio, huyo Ngasa hana mkataba lakini bado anaiwaza Yanga iliyomsababishia deni hilo. Lakini aliwahi kusema asipoifunga Simba atazichoma moto nyumba zake tatu, sasa si auze tu nyumba moja alipe deni?
 
Yanga mlipieni hizo 45M abaki kucheza bure, anaipenda sana Yanga. Mwenzake Msuva mwenye damu ya Msimbazi ana mkataba bado lakini ametoroka kwenda kufanya majaribio, huyo Ngasa hana mkataba lakini bado anaiwaza Yanga iliyomsababishia deni hilo. Lakini aliwahi kusema asipoifunga Simba atazichoma moto nyumba zake tatu, sasa si auze tu nyumba moja alipe deni?
Hiyo hoja yA kulipiwa deni haijawahi kuingia akilini kwangu
 
Tatizo hana meneja na kichwani hamna kitu, hata ukimuuliza dola moja kwa sasa ni shilingi ngapi hajui. Hata deni la sasa lilitokana na kutoelewa kwake mkataba wake na Simba, akasema alidhani amepewa gari la milioni 30 kwa ajili ya kusaini mwaka ule, kumbe ilikuwa kwa ajili ya mwaka mwingine mmoja zaidi. Matokeo yake akaamriwa kurudisha 30M plus 15M za usumbufu. Yanga wakamdhamini mkopo wa benki ambao ni dhahiri nao una riba, hebu jaribu kufikiria riba ya mkopo wa sh. milioni 45 itakuwa kiasi gani! Sasa kwa akili yake akadhani kudhaminiwa ndio kulipiwa. Kuja kushtuka anakatwa kwenye mshahara. Kuja kushtuka zaidi akakuta kumbe hata anazokatwa hazipelekwi benki kulipia mkopo, kuna mjanja anajengea nyumba yake! Benki nayo haina dogo, ikaongeza riba kwa kucheleweshewa marejesho. Dogo akachanganyikiwa akaenda kupumzika Tanga!

Akina Muro wakamwambia tulia tutakusaidia kulipa, dogo akaongeza bidii uwanjani na kiwango kikapanda. Anakuja kwenye kumalizia mkataba hao hao akina Jenny Muro wakamwambia tunakupa milioni 70 katika mkataba mpya, kati ya hizo 45M zilipe mkopo na 25M ndio hela yako

Dogo akashtuka, sasa ameamua kwenda bondeni mwenyewe, tena bila meneja wala mkalimani wa mikataba, wala hata kujua dola moja inabadilishwaje! Huyo ndio dogo ambaye ana wake kadhaa!
 
Back
Top Bottom