Yanga wanajiandaa kumpeleka Kamati ya Maadili Rais wa TFF kwa kuwatukana hadharani

Yanga wanajiandaa kumpeleka Kamati ya Maadili Rais wa TFF kwa kuwatukana hadharani

Mimi na Haji Manara wapi na wapi! Sema ukubwa wa adhabu ndiyo umechangia kumuamsha hayo mashetani yake. Na kupitia huruma ya baadhi ya Watanzania, basi umaarufu wake unazidi tu kuongezeka.

Ukweli utabakia kuwa ukweli tu! Haji Manara ni mtu mwenye mdomo mchafu anapo ongea. Na hii tabia alianza nayo alipokuwa msemaji wa Simba! na hata sasa anaiendeleza akiwa Yanga.
Nimekuelewa mkuu!
 
Manara akishashikwa pabaya anaanza kueneza propaganda ambazo zinawahusu watu wengine, Hilo swala la vinyesi amelisema ili mashabiki wa yanga wamuunge mkono na waichukulie hii kama vita yao huku kiuhalisia ni vita yakwake mwenyewe.

Huyu jamaa ukimchekea ataiharibu Sana tasnia ya mpira hapa nchini. Ni kufungia maisha tu...anachojivunia anao mambulula ambao hawajielewi hawawezi kureason wanaompa support
Ni kweli kabisa anajaribu kuwaingiza mashabiki katika mkwamo wake.
 
OUT OF TOPIC.
Nilikuwa naangalia mazoezi ya wachezaji wa Simba Sc wakiwa jim (gym), sasa Matola katika kupita pita akauona mkono wa Okrah aliekuwa anafanya tizi la ku-pull kamba kutoka juu kushusha chini[emoji23][emoji23], jamaa akadata kwa jinsi mwamba alivyojaza.

Akaushika shika akaishia kusema "AAAH[emoji15][emoji15][emoji15]"

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ila hii ya kuwaita vinyesi fc imenifedhehesha mwana Simba mie
 
Ile press aliokiri na kuomba msamaha ilikuwa ya nini
Na zile picha akiwa na hersi pamoja na karia ?
Hilo la picha mbona kalitolea ufafanuzi mkuu

Alafu press ya kuomba radhi haikuwa kuwaomba radhi kamati ya maadili bali kalia kama kakake kama raisi ya soka na akasema press ile na msamaha ule haufanyi kamati ya maadili isitende haki ama impendelee kwenye sakata lake
 
Wakuu salaam,

Uongozi wa yanga, unajiandaa kumfungulia mashitaka rais wa tff kwenye kamati ya maadili muda wowote kuanzia kesho kwa matamshi yake ya kuwatukana na kuwadhalilisha.

naisubiria kwa hamu hii kesi ili nione kama kamati ya maadili watamuadhibu boss wao/wataufyata.
Kama hii habari ni kweli,basi kumbe hawa utopolo ni kinyesi cha binadamu kweli
 
Hilo la picha mbona kalitolea ufafanuzi mkuu

Alafu press ya kuomba radhi haikuwa kuwaomba radhi kamati ya maadili bali kalia kama kakake kama raisi ya soka na akasema press ile na msamaha ule haufanyi kamati ya maadili isitende haki ama impendelee kwenye sakata lake
BAsi atulie ye si mwanaume?
 
TFF NA 'KICHEKESHO' CHA SAKATA LA HAJI MANARA

Mbali na mambo mengine katika sakata hilo, bado pia kuna mengine ambayo ni pamoja na haya yafuatayo:

(1) Katika Kanuni zote za adhabu za TFF, hakuna hata moja ya kumtoza mtu shilingi milioni 20;

(2) Katika mashtaka yale, mlalamikaji alipaswa awe Wallace Karia mwenyewe na siyo Sekretarieti ya TFF ambayo ndiyo inailipa posho zote Kamati ya Maadili, hivyo lazima itekeleze maelekezo inayoielekeza kama mwajiri.

Hapa kwa tafsiri nyingine, mlalamikaji hakuwa Karia ila Sekretarieti ya TFF ambayo haijasema inahusikaje na ugomvi wa Manara na Karia wala kuwa ina maslahi gani na malumbano hayo, hasa pale ambapo yule anayedaiwa kudhalilishwa hakulalamika.

Mwisho katika hili, kwa vile Kamati ya Maadili inalipwa posho zote za shughuli zake na Sekretarieti ya TFF zikiwemo za kusikiliza mashtaka, hapa maana yake ni kwamba yenyewe ndiyo iliyokuwa mlalamikaji, shahidi wa upande wa mashtaka na hakimu aliyetoa hukumu hiyo;

(3) Karia aliyepaswa awe ndiye shahidi mkuu wa upande wa mashtaka, kisha wengine wote wabaki kuwa mashuhuda, lakini hakuitwa wala kufika ili kutoa ushahidi wake;

(4) Kamati ya Maadili ya TFF haijasema chanzo cha Manara kufanya hivyo wala haijataja mashahidi waliofika mbele yake ili kutoa ushahidi wao dhidi ya Manara.

Hii ni kwa sababu, inawezekana Manara alikuwa anajihami au kujibu mapigo baada ya kuchkozwa, kutukanwa au kudhalilishwa kwanza na Karia; na

(5) Kwa mujibu wa Sheria za TFF, anayefikishwa katika Kamati ya Maadili kwa masuala ya soka ni kiongozi wa kuchaguliwa wa Klabu, Chama cha Soka cha ngazi yoyote, chombo cha Shirikisho la Soka au mwenye nafasi ya kuteuliwa iliyopo kwenye muundo wa Shirikisho la Kandanda Duniani au FIFA.

Nafasi ya "Mhamasishaji" kama aliyonayo Manara haipo katika muundo wa FIFA, hivyo anaweza tu kuwa ni shabiki wa Yanga ambaye hawezi kushtakiwa katika Kamati ya Maadili ya TFF ila mahakamani kama alimdhalilisha Karia.

Alipaswa ashtakiwe Kituo cha Polisi na Karia mwenyewe, kisha apelekwe mahakamani kama mtu binafsi na mlalamikaji akawe shahidi wa Jamhuri kama mtu binafsi na siyo kama Rais wa TFF.

Katika kutekeleza mfumo na muundo wa FIFA, Yanga yenyewe ina Afisa Habari wake, Hassan Bumbuli. Huyo ndiye anaweza kushtakiwa katika Kamati ya Maadili ya TFF.

Kutokana na hali hiyo na hata vinginevyo, swali linalozuka hapa ni je, tangu lini Manara ni kiongozi wa kuchaguliwa au afisa wa kuteuliwa wa Yanga kwa kuzingatia muundo wa FIFA?

Ni cha kujifunza hapa na kukishika kila mshabiki na kukipigia kelele siku zote hadi Manara atakapoachiwa huru ni wajibu ni kwa nini mashabiki au shabiki anaporusha chupa ya maji uwanjani inaazibiwa klabu na si mhusika why Manara ahukumiwe kama yeye wakati anaipigania timu.

Kesi hii tutashinda kabla ya tar.6.8.2022.Tumuombe Mungu
 
BAsi atulie ye si mwanaume?
Mwanaume sio kutulia mwanaume harakati angetulia wewe ungefahamiana wapi kama kanuni azijasajiliwa ungefahamia wapi kama wahuni wale wanaficha nakala ya hukumu

Mwanaume kupigania unacho amini kutulia n kwa wanawake na wanaume goi goi
 
Back
Top Bottom