Yanga wanastahili kufika walipo, sio miujiza bali ni investiment iliyofanyika kwa misimu 3 wakijitafuta!

Yanga wanastahili kufika walipo, sio miujiza bali ni investiment iliyofanyika kwa misimu 3 wakijitafuta!

Mtanzanias

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2021
Posts
1,747
Reaction score
3,725
Najua maumivu waliyonayo upande wa pili ni makali sana, wivu ukijumlisha na chuki vinawafanya wawe na hali mbaya sana zikiwemo stress za kujitakia.

Pamoja na hayo yote bado ukweli unaendelea kubaki vile vile ya kuwa mpira hauna cha short cut, mpira ni uwekezaji na project za maana ili upate unachokitaka. Mpira sio uchawi kusema ya kwamba ukiroga ama kuchoma uwanja moto ndio magoli yatajitumbukiza kwenye nyavu kwa kutumia nguvu za giza,

No way mpira una njia zake na ndio Yanga wameonesha hizo njia, kuna watu wasiojua mpira wanadhani mafanikio ya Yanga hii yamekuja ghafla tu kwa kupiga ramli! Yanga hii imeanza kutengenezwa misimu mitatu nyuma; kuanzia kwenye menejiment, benchi la ufundi na wachezaji.

Ni mchakato ambao ulikuwa na mabonde na milima, tulikuwa tunawashuudia wakisajiliwa kina Yikpe, Balinya, Molinga, Bigirimana, Kindoki, Youthe Rostand na wengine wengi sana ambao waliigharimu klabu mamilioni ya fedha na hakuna cha maana walichoisaidia timu.

Sasa kutoka kwenye usajili ule ndio tukaanza kuona mwanga wa wapi Yanga inakwenda baada ya mapito.

Kwa maana hiyo ubora wa Yanga ya sasa sio wa kubahatisha ni ubora aswaaa. Kuingia Nusu Fainali ya CAF hakujaja kwa bahati mbaya, bali wana kikosi bora na benchi bora la ufundi lililowafanya wafikie hapo walipofika.

Eng. Hersi wakati anakuwa Rais alikutana na changamoto ya kila aina, lakini kwa sasa nafikiri ndiye kiongozi aliyepata mafanikio kuliko kiongozi yeyote yule pale Yanga.

Kabeba makombe yote ya ndani na sasa kageukia makombe ya nje na anaweza maana sio Mhindi wa Bombay anatoa pesa kusajili quality payers na sio garasa prayers kwa bei yoyote ile.

Wananchi Hawapoi na wala Hawaboi.🙌🙌🙌🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom