Yanga wasitarajie ushindi kutokana na kocha mpya, ubora wa wachezaji ndiyo utaibeba timu

Yanga wasitarajie ushindi kutokana na kocha mpya, ubora wa wachezaji ndiyo utaibeba timu

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
YangaSc Vs Al Hilal

NJE YA PICHI....

Kesho Yanga watakuwa uwanjani dhidi ya Al Hilal miongoni mwa mchezo ambao nafikiri utakuwa mzuri na mgumu sana kulingana na ubora na uzoefu wa timu zote mbili.

Msimu huu Al Hilal wanashiriki ligi kuu Mauritania ambako mpaka sasa wanaongoza ligi wakiwa wamecheza michezo 7, wakishinda 5 na kutoa sare 2. Wamefunga mabao 15 wakiwa wameruhusu 2 pekee. Wakati Yanga wako nafasi ya pili wakiwa wamefunga mabao 14 na kufungwa 4 kwenye michezo 10. hii inakupa tafsiri ya ubora wa vilabu vyote viwili japo kuna tofauti ya ubora wa ligi ya Mauritania na Tanzania.

Upande wa uzoefu Yanga kwa misimu miwili mfululizo wamekuwa na mwendelezo mzuri kwenye michuano ya kimataifa wakicheza fainali ya kombe la shirikisho na robo fainali ya Ligi ya mabingwa, hivyo kwa hivi karibuni uzoefu kwao haiwezi kuwa shida sana.

Hivyo hivyo kwa klabu ya AL Hilal ambao wamekuwa na kawaida ya kufuzu hatua ya makundi mara kwa mara na hata zaidi mwaka 2020 wakicheza Robo fainali ya Ligi ya mabingwa.

Tofauti ya uzoefu itakuwa upande wa makocha, Al Hilal wana faida ya kuwa na kocha Ibenge mwenye uzoefu mkubwa kwenye michuano ya kimataifa barani Afrika, ambaye tayali ameshinda ubingwa wa chani, ameshinda ubingwa wa kombe la shirikisho akiwa na Barkane lakini pia amecheza fainali ya kombe la shirikisho akiwa na AC Vita. Wakati Kocha wa Yanga Ramovic bado hana uzoefu wowote kwenye michuano hii, hivyo Yanga ndiyo timu yake ya kwanza kuanza kutengeneza uzoefu. bila shaka huu ni ugumu ambao Ramovic anaenda kukutananao kesho mbele ya Ibenge.

Kwa upande wa Ubora wa wachezaji so far Yanga wanaonekana kuwa vizuri sana. Wana muunganiko wa wachezaji wengi bora kutoka mataifa mbalimbali. Takribani wachezaji 10 wakizisaidia timu zao za Taifa kufuzu michuano ya Afcon. Ni tofauti na Al Hilal ambayo ubora wa wachezaji wake asilimia kubwa profile yao sio kubwa kulinganisha na Yanga.

Binafsi nafikiri Yanga wanatakiwa kunufaika zaidi na ubora wa wachezaji kuliko Kocha kwenye mchezo wa kesho. Kwa sababu Kocha bado mgeni na hata profile bado haimbebi sana. Hivyo wachezaji wanatakiwa kujua pamoja na kile watakachopewa na mwalimu lakini asilimia kubwa mechi ipo mabegani mwao.

yangaSc Vs Al Hilal

✍️ Nedy Mgogo
 
Back
Top Bottom