Yanga watafanya vizuri kimataifa zaidi ya simba msimu ujao

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Najua jambo hili ni ngumu kidogo kuingia masikioni mwa mashabiki wa simba.

Maana wamekariri kuwa yanga kimataifa si lolote ni kama Mbeya kwanza tu wakiwa kimataifa ila ukweli ni kwamba Yanga itashangaza watu wengi.

Wakiona wanavyo toboa anga kuingia final ya CAF.

Na ushindi mwingi wa yanga utakuwa unapatikana ugenini.

Nyumbani watakuwa wanafanya vibaya ila wakifika ugenini ndo moto una waka kweli.

Naombeni wote hii post msave kwenye simu zetu mtarudi ku comment
 
Yanga Ina kikosi kizuri, haijalishi Nyumbani Wala ugenini watafanya vizuri. Swala la kutinga nusu fainal au fainal ilo kwasasa ni kama utabiri, uhakika watafika mbali ila hatujui umbali gani.
 
Yanga Ina kikosi kizuri, haijalishi Nyumbani Wala ugenini watafanya vizuri. Swala la kutinga nusu fainal au fainal ilo kwasasa ni kama utabiri, uhakika watafika mbali ila hatujui umbaligani.
Amini ninacho kuambia
 
Inshallah
 
.... Na ushindi mwingi wa yanga utakuwa una patikana ugenini. Nyumbani watakuwa wanafanya vibaya ila wakifika ugenini ndo moto una waka kweli
Mwanzo nilidhani unachambua kisayansi, ila ulipofika hapo kwenye utabiri kwamba watakuwa wanafanya vizuri ugenini na vibaya nyumbani, imedhihirisha kwamba sio uchambuzi wa kiufundi bali unabii
 
Hilo linajulikana kulingana na namna kikosi chao klivyokamilika kila idara kwa sasa, tiyali wamewabakiza wachezaji wao wote muhimu na wameongeza quality ya wachezaji wachache wanaokuja kuongeza ubora kwenye mapungufu ya msimu uliopita, ivyo haitokuwa timu ya masikhara masikhara kama miaka iliyopita nawaona wakitinga makundi na wakitinga robo fainali ya caf champions league wala sitoshangaa kwakuwa wanayo timu yenye uwezo wa kufanya ivyo kwa sasa, Zile habari za kwamba awafanyagi vizuri kimataifa zitabaki kuwa Kama historia kuanzia msimu huu
 
kwa kujipima nguvu na masela wa Friends Rangers ya Manzese kweli mtafika mbali!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…