Nimeona niwape kidogo mbinu Yanga ili kuisaidia timu kuvuka hiyo hatua muhimu.
Kwanza nawasalimu. Mimi ni mpenzi wa mpira wa Ulaya hasa Ligi ya Uingereza katika kipindi cha miaka ya 2000 hadi 2013. Katika hiki kipindi soka la Ulaya lilikuwa sio la kisport sport. Ilikuwa ni balaa sio kama sasa hivi hakuna wachezaji wa kutisha.
Wachezaji nguli wale wa miaka hiyo sasa hivi ni makocha. Akina Zinadine Zidane, Patrick Viera, Claudi Makelele, Louis Figo, Thieri Henri, kina Inniesta na kulikuwa na beki hatari yule wa Italia, alipigwa kichwa na Zinadine Zidane,
na wachezaji wengine wengi unaweza kuongezea.
Tukirudi kwenye mada hii timu ya Fc Porto wakati inanolewa na Kocha Jose Mourinho ilikuwa ikikufunga goli moja dakika za mwanzo hurudishi mpaka mwisho dakika 90 zinakamilika, na dakika za nyongeza hurudishi. Na hata ukienda FIFA kuomba wakuongezee dakika nyingine hurudishi na hata ukiomba poo hurudishi mpaka mpira unaisha.
Sijui fomesheni aliyokuwa anatumia huyu kocha mtata na mtaalamu Jose Mourinho. Sasa ndugu zangu wa Yanga watafute video za huyo kocha alipokuwa na timu hii ya FC Porto ya Ureno itawasidia. Kifupi gemu ni rahisi sana Yanga wanatakiwa wapate goli moja tu halafu wanalilinda mpaka mwisho.
Dakika 90 zina vipindi vya dakika 15, watumie dakika 15 za mwanzo kuusoma mchezo wa adui. Wakishajua anachezaje halafu dakika 15 za pili waanze kulazimisha kupata bao huku wakizuia kwa makini. Wanaweza wakamuacha mtu mmoja mbele wakati huu wa kuusoma mchezo yaani dakika 15 za kwanza halafu baadae akabadili mbinu.
Na ikiwezekana kocha aweke viungo wakabaji wengi kipindi cha kwanza wakati wa kuusoma mchezo hawa viungo wakabaji wanasaidiana na mabeki kutoruhusu mpira kupita na hapo hapo wanacheza pasi ndefu kupeleka mbele kwa Mayele.
Winga wa pembeni wanatakiwa wawe na mbio ili kuwachosha wapizani na kuwafanya wasipande mbele. Mara nyingi kwenye hii michuano ya nyumbani na ugenini, timu ya ugenini inakuwa na uhuru sana wa kucheza kuliko timu ya nyumbani kwa sababu timu ya nyumbani wanataka kwenda mbele haraka ili kupata goli.
Na wakati huo huo wanatakiwa wazuie wasifungwe, yaani wanacheza kwa presha kwa hiyo wanakuwa na majukumu 2 kwa wakati mmoja. Yanga wanatakiwa wasiwe na presha, najua wako nyuma kwa goli la ugenini lakini wanatakiwa kucheza kitaalam zaidi kuliko kukimbia kimbia.
Dakika 15 za mwanzo kama wakimuona mpinzania hana papara za kushambulia basi watumie mwanya huo kwenda mbele kwa kasi na kuwahi kurudi nyuma. Kitu kingine ni kuwalinda wale wachezaji wao hatari kuhakikisha hawafurukuti. Ukiwaweka hao mfukoni basi umewini gemu. Kazi kwenu Yanga na kila la heri.
Mimi siyo mchambuzi wa mpira au soka bali nimeona nitoe maelekezo muhimu. Pia kama Yanga wanajiamini wanaweza wakaamua kucheza mpira wa kufunguka, yaani piga nikupige.
Nitarudi. Poleni kwa mpangilio, mimi ni mvivu wa kuandika.
Mawazo mengine yanaruhusiwa.