Yanga ya sasa ikikutana na Simba hii itafungwa goli hata 11

Muite

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
2,971
Reaction score
6,607
Nimeangalia mwenendo wa Yanga inaonyesha kiwango kinazidi kushuka kwa kasi kubwa sana, hata inaposhinda unakuta inashinda kwa kupambaaaaana kama bao la mzee, kagoli kamoja.

Hata game ile aliyocheza na Simba tuwe wa kweli maana ingechezeshwa na refa makini kama Aragija Simba ingeshinda kwa goli 3. Ona juzi kacheza na Azam kafungwa tukasingizia kuwa tulicheza pungufu. Na jana tumecheza lakini tumefungwa goli tatu, ninaamini Tabora wangekuwa makini wangefunga hata goli tano.

Kwa upande wa Simba tukiweka ushabiki pembeni ni dhahiri mwenendo wake unatisha sana, Simba tayari wameshajipata tena pakubwa kitimu na individual players, tuliwabeza kina Mukwala, Ahoua, Ateba na wenzake lakini kumbe jamaa ni moto.

SIMBA HII IKIKUTANA NA YANGA HII TUTEGEMEE MAANDAMANO PALE JANGWANI NA JENGO KUPIGWA KIBIRITI MAANA KUFUNGWA GOLI ZAIDI YA KUMI HAKUNA ATAKAYEUELEWA UONGOZI.

Halafu Yanga hebu tuacheni tabia ya visingizio vya kijinga sana. Naona tunaanza kusema tunahujumiwa, mara tunafanyiwa ushirikina, mara sijui wachezaji wanapigwa misumari, Mara sijui Kuhama uwanja wa Azam.
HUWA NINACHUKIA SANA MAWAZO YA KISHIRIKINA PALE UNAPOFELI KWA UJINGA WAKO HALAFU SABABU YA KUFELI KWAKO USINGIZIE KULOGWA AU KUHUJUMIWA.

NA HILI LA VISINGIZIO VYA KISHIRIKINA NI TANGU MIAKA MINGI HII TIMU YANGU YA YANGA NA MASHABIKI WAKE WAMEKUWA WAKILIBEBA SANA TOFAUTI NA WENZAO WA SIMBA. Simba wao mara zote wamekuwa wakiamini katika sayansi ya football, wakiona shida ni kocha watachukuwa hatua, wakiona shida ni uwezo wa wachezaji watachukuwa hatua kurekebisha. Huwezi kusikia Simba wakisema wamelogwa.

Yaani mfungwe goli 3 halafu mseme ni hujuma ya uwanja na kulogwa!!!! Wakati wote tumeona mchakamchaka tuliopelekewa na wale warina Asali.

Pia tuache kusema sijui hakuwepo Baka, Boka, Job na Yao. NAKUMBUKA MMEKUWA MKISEMA.YANGA KIKOSI KIPANA SAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAANA
 
Kinachowafanya muingie uwanjani kinyumenyume ninin kama sio uchawi, kule south mlichoma nin uwanjani, unajua sababu yakuhama uwanja wa azam complex nibaada yakuzan mnalogwa
 
Kila mechi ina uzito na mipango yake jinsi ya kuicheza usifikiri yanga iwe na mechi na simba icheze kama ilivyocheza na Tabora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…