Yanga yabanwa mbavu na Mtibwa. Yashindwa kutamba Morogoro

Habari nzuri sana hizi kwa wanaSimba...adui yako muombee njaa.
 
Point yako No.1 inashusha hadhi ya Jf kama chanzo muhimu cha taarifa. Kama huujui mpira acha wanaojua wachangie. Mimi ni shabiki wa mpira na mechi nimeiona lakini kusema penati yenye utata ni upotoshaji wa kitoto. Hata kama huwapendi hao Yanga sijui ndala kama unavyowaita sema ukweli maana kuna wengine hawajaiona hii mechi na wanaweza kukumbwa na ushabiki wako wakaamini kulikuwa na uonezi kumbe ni uchochezi wako tu.
 
Mateja FC jana walisumbua sana.. Ha ha ha ha ha.. Mjue mungu si mkata umeme
 
labda kwa sababu mimi sijui mpira.. ila kwa jinsi nilivyoona, ile haikua penati kabisa.. kwa kifupi ile ni mbeleko.. na ombi langu kwa bodi ya ligi chunguzeni hili suala.
 
Jana pia ungefungua uzi kama huu ungekuwa umetenda haki ila mapambano bado yanaendelea hongera kwa sare ya jana mtani wangu.
 
Yanga kama Man U.Sehemu ya kupandia wanaicgezea bora Ubingwa uchukuliwe na Simba.Hakuna namna
 
Na hiyo ni kwako.. Kwangu ni penati yenye utata Mkubwa saaana.. Ndugu zangu wa bodi ya ligi mchunguzeni refa wa mechi ya leo.. pia kuna mtu kama Yondani nimeshangaa anamalizaje dk 45.. ina maana refa leo red card hakuingia nayo uwanjani??!
Huyo Yondan bora na wewe umeona!
 
Sisi wa Pwani tunasema: KILICHOMPATA MAMBA NA BOKO KITAMPATA
 
Yanga akifungwa na Azam shughuri imeisha
Yaani mikia bwana,, hamjihurumii kwamba mnafungwa na vitimu vya ovyo ovyo kweli? Jana yenyewe bila mbereko mlikuwa mmeloa! Kagera kwenyewe hamchomoki, mkija kwa Mbao FC pale napo mnaacha point!!
 
Yaani mikia bwana,, hamjihurumii kwamba mnafungwa na vitimu vya ovyo ovyo kweli? Jana yenyewe bila mbereko mlikuwa mmeloa! Kagera kwenyewe hamchomoki, mkija kwa Mbao FC pale napo mnaacha point!!
Kwani nyinyi Unga Limited FC mko nafasi ya ngapi.? maana mnatia huruma kwa vile miezi sasa hamfiki juu..!
 
Hawa ndala wajifunze kupiga penat kila siku msuva anapaisha.[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwani nyinyi Unga Limited FC mko nafasi ya ngapi.? maana mnatia huruma kwa vile miezi sasa hamfiki juu..!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] .. Hii mijamaa inatia huruma kweli.
 
Hawa ndala wajifunze kupiga penat kila siku msuva anapaisha.[emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu.. Hii mijamaa uwezo wao wa kupiga penati ndo umeishia hapo. Hata kama wakimpa yule kocha wao lazima nae apaishe tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…