Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo Duniani (CAS) imeitupilia mbali rasmi kesi iliyofunguliwa na Klabu ya Young Africans Sports Club (Yanga SC) dhidi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), na Klabu ya Simba SC.
Katika uamuzi uliotolewa tarehe 1 Mei 2025, Naibu Rais wa Divisheni ya Rufaa ya CAS, Elisabeth Steiner, alieleza kuwa CAS haina mamlaka ya kisheria kushughulikia shauri hilo lenye kumbukumbu namba 2025/A/11298. Kwa mujibu wa taarifa hiyo rasmi, kesi hiyo imeondolewa kabisa kutoka kwenye orodha ya mashauri ya CAS.
CAS imesisitiza kuwa uamuzi huo umetolewa bila gharama zozote za ziada kwa pande zote, isipokuwa ada ya ofisi ya CAF 1,000 (sawa na takriban shilingi milioni 2.7 za Kitanzania) ambayo tayari imelipwa na Yanga SC na haitarudishwa.
Uamuzi huu unamaliza rasmi mvutano wa kisheria kati ya Yanga SC na vyombo hivyo vya soka Tanzania, ambao ulifikishwa CAS kwa lengo la kutafuta haki nje ya mipaka ya nchi.
Huu ni mwendelezo wa hatua mbalimbali za kisheria zinazochukuliwa na vilabu vikubwa nchini katika kudai haki zao, lakini pia unatoa fundisho kuhusu upeo wa mamlaka ya CAS na masharti ya kupokea mashauri kutoka mataifa mbalimbali.
Yanga Nyuma Mwiko 😀😀