Yanga yadondokea pua CAS, dabi ipo palepale

View attachment 3322041

Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam imeshindwa kwenye kesi yake ya awali iliyoifungua kwenye Mahakama ya Usuluhishi Michezoni (CAS).

Yanga SC katika kesi ya msingi ikiyoifungua dhidi ya TFF, Bodi ya Ligi na Simba SC imeomba kupewa alama 3 na mabao 3, lakini ikaiomba CAS pia izuie tarehe ya 'DABİ' isipangwe mpaka kesi ya msingi itakaposikilizwa, yani ile ya kudai alama 3 na mabao 3 kwa walichosema Simba SC waligomea mchezo wa tarehe 8 Machi, 2025.

Walalamikiwa Simba SC, TFF na Bodi ya Ligi kwenye utetezi wao walipinga Yanga SC kufungua kesi CAS na kuzivuka mamlaka za TFF za kisheria.

Kwenye hukumu CAS wamekubaliana na Simba SC, TFF na Bodi ya Ligi kwamba wao CAS hawana mamlaka ya kuzuia kupangwa kwa tarehe ya DABI, lakini pia wamekubaliana na walalamikiwa kwamba wao CAS hawana pia ya kushughulikia jambo hili kabla halijapitia kwenye mamlaka za kisheria za TFF.

Hivyo basi shauri la Yanga SC limepigwa chini na sasa TFF na BODI YA LİGİ wako huru kupanga tarehe ya DABI na itapigwa kama kawaida.

Kwa hukumu hii Yang SC wakigomea kucheza DABI itakapopangwa, maana yake ni kwamba watapokonywa alama 15, wako tayari kwa hilo? Msimamo wao ulikuwa hakuna kucheza hiyo mechi lakini walikuwa wanategemea CAS ambako wamepigwa za uso tena pamoja na lundo na mawakili walio orodheshwa huko CAS. Dabi haina kipengele, kipengele uje nacho wewe.
Ni wakati sasa yanga itafute mawakili wengine wenye uelewa mkubwa wa taaluma yao.
Hersi na jopo lake nao wajiangalie kama wanatosha kwenye nafasi zao.
Kitendo cha Hersi & co kubadilisha makocha watatu ndani ya msimu mmoja ndiyo chanzo cha timu kufanya vibaya cafcl
 
Idara ya sheria ya klabu ya Yanga inaendeshwa na kigenge cha wapigaji.
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Acheni ujinga nyie utopolo. Andaaeni mechi, safari hii mkiweka hao makomandoo wenu getini wazee wetu washindwe kuingia kutegua matunguli yenu mtatukoma
 
View attachment 3322041

Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam imeshindwa kwenye kesi yake ya awali iliyoifungua kwenye Mahakama ya Usuluhishi Michezoni (CAS).

Yanga SC katika kesi ya msingi ikiyoifungua dhidi ya TFF, Bodi ya Ligi na Simba SC imeomba kupewa alama 3 na mabao 3, lakini ikaiomba CAS pia izuie tarehe ya 'DABİ' isipangwe mpaka kesi ya msingi itakaposikilizwa, yani ile ya kudai alama 3 na mabao 3 kwa walichosema Simba SC waligomea mchezo wa tarehe 8 Machi, 2025.

Walalamikiwa Simba SC, TFF na Bodi ya Ligi kwenye utetezi wao walipinga Yanga SC kufungua kesi CAS na kuzivuka mamlaka za TFF za kisheria.

Kwenye hukumu CAS wamekubaliana na Simba SC, TFF na Bodi ya Ligi kwamba wao CAS hawana mamlaka ya kuzuia kupangwa kwa tarehe ya DABI, lakini pia wamekubaliana na walalamikiwa kwamba wao CAS hawana pia ya kushughulikia jambo hili kabla halijapitia kwenye mamlaka za kisheria za TFF.

Hivyo basi shauri la Yanga SC limepigwa chini na sasa TFF na BODI YA LİGİ wako huru kupanga tarehe ya DABI na itapigwa kama kawaida.

Kwa hukumu hii Yang SC wakigomea kucheza DABI itakapopangwa, maana yake ni kwamba watapokonywa alama 15, wako tayari kwa hilo? Msimamo wao ulikuwa hakuna kucheza hiyo mechi lakini walikuwa wanategemea CAS ambako wamepigwa za uso tena pamoja na lundo na mawakili walio orodheshwa huko CAS. Dabi haina kipengele, kipengele uje nacho wewe.
Aibu Yao since day one tuliwaambia mtunze tiketi derby IPO pale pale, ohh hatuchethi kumbafu zao
 
Back
Top Bottom