YANGA yakasirishwa na SIMBA SC, kumsajili BM33, watoa tamko

Tff wanavyo nakala ya mikataba yote ya wachezaji, uyo Morrison Tff ndio walio mwidhinisha kua mchezaji wa Yanga na iyo mikataba yote na nakala wanazo.

Iwemiezi 6 au miaka 2 Sasa tusubiri tuone je! Tff wata usajiili mkataba mpya wa Morrison.
 
Uchebe alisema Simba haiwezi kuendelea kwakua kuna watu un educated, Ismail Aden Lage akiwa mweyekiti wa Simba alisema Simba ni Mbumbumbu mimi ninasema Simba bado ni mbumbumbu ila sasa wapo kwenye daraja la pekeyao ni next level .
Unakuwa kama mgeni kwenye Usajili wa bongo.
Mara ngapi Signature zimekuwa forged?
Si ni hawahawa GSM walisema wamemsign pappy?
Saiv hajasign tena
 
Mkataba ulioidhinishwa na FIFA ni ule wa miezi 6 tu, na uliisha Julai 14, Kuna madirisha mawili ya kufanya transfer ya mchezaji wa kimataifa, kubwa ni hili linaloendelea na kumalizika September 10, na dogo huisha January 31. Tukirudi kwenye huo Mkataba wa March wa miaka miwili, si Mkataba halali, na unapingwa kwa vipengele vingi tu lakini muhimu zaidi vipengele viwili. Kipengele cha kwanza umeghushiwa saini ya Morrison, kipengele hiki kitawapa wakati mgumu TFF kuamua, kwani Polisi hawana mamlaka ya kusema hiyo saini ni ya Morrison au sio ya Morrison, sana sana wanaweza sema mwandiko wa saini hiyo unafanana sana na ya Morrison, kimahakama hadi upatikane ushahidi mwingine utakao thibitisha pasi na Shaka kwamba ni Morrison ndiye aliye saini fomu hizo, ushahidi wa picha au video siku hizi haukubaliki sana. Kipengele cha pili ambacho kinauua kabisa huo Mkataba na kuufanya sio halali (Invalid) ni clause moja wapo ya.mkataba huo ambapo Yanga walitakiwa kumaliza malipo ya signing fee ndani ya mwezi moja, lakini Yanga walimwingizia pesa kwenye account mwezi Julai, hivyo tayari Yanga walikiuka masharti ya Mkataba Γ±a kuufanya void (Batili) na inasemekana Morrison aliiamuru benki yake irudishe hizo pesa kwa Yanga. Tayari imekula kwa Yanga, Morrison atakipiga Msimbazi msimu ujao.
 
Luc Eymael akasema Yanga ni
1. Un educated
2. Nyani
3. Mbwa

We unaona hayo matusi ni sawa?we unaona hayo ni sawa?isitakw watu tuseme maneno mengine hatukupanga.inaumiza sana.

Uchebe alisema Simba haiwezi kuendelea kwakua kuna watu un educated, Ismail Aden Lage akiwa mweyekiti wa Simba alisema Simba ni Mbumbumbu mimi ninasema Simba bado ni mbumbumbu ila sasa wapo kwenye daraja la pekeyao ni next level .
 
Mbona wewe umeumia sana ?why umeumia hivi? Sisi yanga tunafahamu uhuni wa GSM acha yatupate. Wewe unajiita simba na wakati ni yanga mwenzetu na sema tu we ni yanga nyani au mbwa. Luc Eymael. Gsm washenzi wameforge mkataba tunajua sisi tulio ndani



Yanga kusema kuwa Morisson ana mkataba hadi 2022, ni tosha uwa usajili wa mizengwe
Shame on Senzo, Mo Dewji na Simba
 
Yanga wamewafukuza wachezaji makini na kumuacha morisson huku wakijua kawaleta utovu wa nidhamu kumbe lengo lao ni kumblock tu simba wasimchukue hahahaa.
 
Nachoseza kusema tu ni kwamba Yanga hususani mashabiki uangalieni uongozi wenu vizuri, kunatatizo kubwa sana. Msiishie kulaani na kulalamika tu ila jaribuni kuhoji uongozi wenu kwann wanakua na Mambo ya magumashi na ikiwezekana muwawajibishe. Anakubali mpira wa bongo magumashi nyingi lakini naiona Simba mbele ya Yanga kwa weledi. Kwann uongozi uongee uongo kuhusu usajili wa morisoni, hapo tu ndio penye swali la maana.
 
Tukiacha ushabiki wa Simba na Yanga mimi binafsi nadhani viongozi wa Simba walihitajika kutumia busara tu ya kawaida wangesubiri mpaka jumatatu ndio wamtangaze Morison kuwa mchezaji wao baada ya TFF kutoa uamuzi wake. Sielewi ni kwanini viongozi wa Simba wameshindwa kuwa na subira katika jambo hili dogo . Na ni nini kimewapa jeuri hiyo viongozi wa Simba ili hali mchezaji bado hukumu yake haijatolewa na TFF/ Polisi au hiyo hukumu imeshavuja? Je katika hali ya uswahili kama huu wapenzi wa mpira nchini waendelee kuamini kuwa Simba inaendeshwa kisasa? Viongozi wa Simba wamejiandaaje iwapo hukumu ikitokea kuwa Yanga wameshinda kesi dhidi ya Morison?

Yote kwa yote ukweli lazima usemwe kuwa Morisoni ni bonge la mchezaji ndani ya uwanja lakini nje ya uwanja jamaa ni "comedian" bab kubwa hata "makomediani" wenye fani yao wanazima fegi. Lakini napata mashaka sana na nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa zile komedi zote alizofanya Morison akiwa Yanga ilikuwa tu ni kwa sababu alikuwa ana ugomvi binafsi na viongozi waYanga na si tabia yake. Tabia ni kama ngozi haifichiki je viongozi wa Simba wamejiandaa vipi kukabiliana na vituko vya huyu mchezaji iwapo ataanza "ukomedian" wake pale Simba?

Mwisho nikiangalia kote Morison alikopita kuna sehemu moja au mbili hivi alikuwa na matatizo ya mikataba. Kwa hiyo hii sio kesi ya kwanza kuhusiana na mkataba wake wa kazi. Je GSM hawakuliona hili mapema na iwapo walilijua hili mapema je walichukua hatua gani? Je nao Simba hawalijui hili na kama wanalijua wamechukua tahadhari gani isije wakawa wahanga wa kuingizwa "king" na mtukutu Morison?
Jumatatu sio mbali nadhani ndio muda tutakapoanza kuona mwanga wa hili suala na majibu mengi sana wanaojiuliza wapenzi wa soka nchini yataanza kupata majibu baada ya TFF/ Polisi kutoa taarifa ya uchunguzi na maamuzi ya hili sakata. Na pia itakuwa fursa nzuri sana ya kuanza kumwelewa huyu mwamba wa Ghana maana mpaka sasa sidhani kama kuna mpenda soka nchini anayeweza kusimama mahali na kumwelezea huyu jamaa ni mtu wa nama gani kutoka na vitendo vyake anavyovifanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…