Yanga walisha peleka mkataba wa Morrison TFF tena mkataba ambao Tff kupitia mtaalamu wao wa TMS wali uidhinisha maana TFF wanaye mtaalamu wa TMS. Yanga wakapeleka malalamiko juu ya mchezaji wao Benard Morrison kurubuniwa na Simba wakati anamkataba wa miaka miwili na wao Tff kimsingi walisha utambua.
Jambo la kushangaza wakati Tff bado hawajatoa maamuzi ya malalamiko ya Yanga, Simba wamemtangaza rasmi kwamba Benard Morrison ni mchezaji waliye msajili. Sasa wapenzi wa mpira tusubiri Tff watachukua uamuzigani juu ya swala hilo.
Endapo timu ikibainika imemrubuni mchezaji pasipo klabu yake kushirikishwa adhabu zake nikama ifuatavyo. Mchezaji atafungiwa miezi 4 au miezi 6.
Klabu iliyo fanya kosa Itapewa moja ya adhabu zifuatazo.
Onyo, fain, kushushwa madaraja mawili, kuzuiwa kufanya usajili. Kwasasa tunawasubiri Tff kwakua picha ndio linaanza.