Mkataba ulioidhinishwa na FIFA ni ule wa miezi 6 tu, na uliisha Julai 14, Kuna madirisha mawili ya kufanya transfer ya mchezaji wa kimataifa, kubwa ni hili linaloendelea na kumalizika September 10, na dogo huisha January 31. Tukirudi kwenye huo Mkataba wa March wa miaka miwili, si Mkataba halali, na unapingwa kwa vipengele vingi tu lakini muhimu zaidi vipengele viwili. Kipengele cha kwanza umeghushiwa saini ya Morrison, kipengele hiki kitawapa wakati mgumu TFF kuamua, kwani Polisi hawana mamlaka ya kusema hiyo saini ni ya Morrison au sio ya Morrison, sana sana wanaweza sema mwandiko wa saini hiyo unafanana sana na ya Morrison, kimahakama hadi upatikane ushahidi mwingine utakao thibitisha pasi na Shaka kwamba ni Morrison ndiye aliye saini fomu hizo, ushahidi wa picha au video siku hizi haukubaliki sana. Kipengele cha pili ambacho kinauua kabisa huo Mkataba na kuufanya sio halali (Invalid) ni clause moja wapo ya.mkataba huo ambapo Yanga walitakiwa kumaliza malipo ya signing fee ndani ya mwezi moja, lakini Yanga walimwingizia pesa kwenye account mwezi Julai, hivyo tayari Yanga walikiuka masharti ya Mkataba ña kuufanya void (Batili) na inasemekana Morrison aliiamuru benki yake irudishe hizo pesa kwa Yanga. Tayari imekula kwa Yanga, Morrison atakipiga Msimbazi msimu ujao.