Yanga yakung'utwa 2-1 huu ni mwanzo tu

Yanga yakung'utwa 2-1 huu ni mwanzo tu

View attachment 1915355

FT Yanga 1 - 2 Zanaco

Soka sio kipompipompi, soka sio makelele midomo mirefu..Soka ni mipango. Huu ni mwanzo tu. Nawaambia kabla ya TPL kuanza mtakuwa nje CAFCL.

Kwa wale wasiofahamu ni kwamba leo Yanga imecheza mechi 3. Under 20 wamechezea kichapo kitamu. Yanga Princes wametoa droo. Utopolo wenyewe wamechezea cha kulalia.

Kifupi TPL imeisha cha msingi ni kuandaa lawama tu kwa TFF.
KAPUMBU mtu mbadi...awapiga uto goli la mbali...wahaha uwanja mzima..!aamua kuwafuata na kuwajaza akishangilia alivyowapiga goli..
 
Wamefanya makosa wangemwingiza winga aliyebuma akafukuzwa wao wakamwona anawafaa wakamsajili kwa dau la mara Kumi na tano ya alichokua anapokea namaanisha hajiiii.
 
Simba mnachonga sana wakati na nyie walewale tu, ebu tuacheni na siku yetu muhimu bana, tumefungwa sawa ila siyo mbaya next time tutaua mtu[emoji23]

Krismasi ni krismasi tu hata pilau ikiungua bado sherehe iko palepale
 
Yanga waliwaalika zanaco waje kwenye bononza ona sasa zanaco wamekuja kucheza mechi walitofautina lugha hawa
 
Simba mnachonga sana wakati na nyie walewale tu, ebu tuacheni na siku yetu muhimu bana, tumefungwa sawa ila siyo mbaya next time tutaua mtu😂
Mtawafunga Wanigeria? Thubutuuu.

Ndio,kwa Mkapa mnaweza mkajitutumua.Ila kule machinjioni Surulele mtaliwa kiboga na ndo mtakatupwa nje ya CAFCL.

Nyinyi si mliona ni rahisi Simba ilipowapiga wale Wanageria?Mnafikiri nanyi mtaweza? Simba ilipoifunga Nkana mkasema Simba imecheza na timu ya kichovu.Leo Zanaco wamewafanya nini? NA NINAKWAMBIA HATA HAO NKANA WANGEWAGONGENI VIZURI TU.
 
Back
Top Bottom