Yanga yakwepa fedheha kwa Simba, yajitoa CECAFA Kagame Cup

Lupweko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
23,566
Reaction score
24,891
Taarifa zinaeleza kuwa uongozi wa klabu ya Yanga umewaandikia barua TFF kuwaomba kujitoa katika mashindano ya Kagame CUP yanayotarajiwa kuanza June 28 mpaka Julai 13 2018 jijini Dar es Salaam.

Sababu za msinngi zilizofikia Yanga kuandika barua hiyo ni kufanya maandalizi ya michunao ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo watacheza na Gor Mahia FC ya Kenya, Julai 18 jijini Nairobi.

Kutokana na muingiliano wa ratiba ya KAGAME na CAF, Yanga wameona ni vema kuwapatia wachezaji wao mapumziko ili kuwapa fursa ya kujiandaa vizuri kuelekea mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya tatu baada ya kucheza na USM Alger pia Rayon Sports ya Rwanda.

Taarifa hizo zinazoelezwa kutoka Yanga kupitia viongozi wa Kamati ya Utendaji wa klabu hiyo, wameazimia kufanya maamuzi hayo ili kuepuka kubanwa na muingiliano wa ratiba hiyo ambayo imekuwa si rafiki kwao.

Kufuatia kuandika barua hiyo ya kuomba kujiondoa, Yanga wanakuwa wameikwepa Simba kwenye mashindano ambapo walikuwa wamepangwa pamoja na mabingwa hao wa Ligi Kuu Vodacom.

Simba na Yanga zimepangwa pamoja kwenye kundi C ambapo kuna timu zingine ambazo ni Dakadaha ya Somalia pamoja na St. George kutoka Ethiopia.

Chanzo: Salehe Jembe
 

Attachments

  • upload_2018-6-8_9-42-51.png
    27.7 KB · Views: 73
Yanga wakijitoa basi ntawadharau,hao Goro Mahia watakaocheza nao,wao hawashiriki Haya mashindano?.Michuano inaisha tare 13,yanga wanacheza tare 17 na goro mahia siku nne za mapumziko wanazo kama wakiingia fainali.

Suala wanalolikwepa yanga nikukutana na Simba,kwa sababu wanahofu wakifungwa hali ya hewa itachafuka.Nachowashauri CECAFA wawafungie yanga kushiriki mashindano haya kwa muda miaka 2 au 3,kama watakuwa wamejitoa ili mwakani wapate muda mzuri wakupumzika maana hawatokuwa kwenye mashindano yoyote ya kimataifa.
 
Yanga ina ɓifu na musonye toka kipindi cha maximo ..We unamsikiliza saleh jemɓe simɓa damu...
 
Vyuraaaaaaaa!!!!!
Sasahivi mnadabu sana.. Nakumbuka simba pamoja na matatizo yanayojitokeza lakn haijawahi kujitoa kwenye mashindano kisa et kuiogopa yanga
2014 yanga ilitaka kupeleka timu B na baadhi ya wachezaj wa kikosi A mashindanoni chin ƴa maximo ..musonye akachomoa ..umeshasahau
 
uchambuzi wako unaonesha hujui kitu juu ya yanga na cecafa. ukweli ni kuwa yanga hawataki kushiriki kombe hili tangu zamani kama unakumbuka mwaka 2014 walipeleka kikosi b cecafa wakakataa. kinachoonekana kombe hili lina mvuto likichezwa tz na washiriki lazima wawaweke simba na yanga ili wapate mashabiki wengi uwanjani. na kuhusu kuwekwa kundi moja simba na yanga hii ni mbinu ya cecafa kuvuna pesa za viingilio mapema kwenye mechi ya watani. na kwa taarifa yako lile kundi A zitapita timu tatu mshindi wa kwanza,wa pili na wa tatu atapita kama best looser wa kundi sasa hapo yanga atakosaje kupita. ujue kwanza mpira wa bongo kabla hujaeleza lolote.
 
Kumanina zao Yanga isiposhuka daraja mwaka unaokuja then TFF itakuwa haijatenda haki. Hii timu kwa kweli ipo ila ni kama imekufa vile.
 
Yanga ina ɓifu na musonye toka kipindi cha maximo ..We unamsikiliza saleh jemɓe simɓa damu...
Kwa hiyo ukiwa na bifu na mtendaji mmoja (tena wa kuajiriwa tu), ndio sababu ya kujitoa kwenye mashindano? Nchi ngapi zilikuwa zinatofautiana na Sepp Blatter wa FIFA? Ulishawahi kusikia zimejitoa kushiriki kombe la dunia? Hiyo sio sababu, kikubwa hapo ni kuikimbia Simba, kama ilivyofanya kule Nakuru kwenye SportPesa
 
Kumanina zao Yanga isiposhuka daraja mwaka unaokuja then TFF itakuwa haijatenda haki. Hii timu kwa kweli ipo ila ni kama imekufa vile.
matusi ya nini mkuu wengine hatuwezagi kuvumilia hayo madude utachafua hali ya hewa hapa.
 
Hapo ndio naamini viongozi wengi wa Yanga kichwani hakuna kitu!!! Utamuogopaje mpinzani wako hata kabla ya kuingia ulingoni huo ni udhaifu wa hali ya juu sana.YANGA wangeweza kutumia mechi hiyo kujiingizia kipato kwani kwasasa wamefulia na mashabiki wao hata kwenda uwanjani wanaona aibu, pili kama YANGA wangebahatika hata kutoa draw na SIMBA kwenye mechi ya KAGAME au kushinda basi club ingekuwa na furaha na amani na mashabiki wangekuwa na furaha kama wamechukua ubingwa na hata kama wangefungwa bado wangekuwa na kisingizio kuwa timu yao bado wanaisuka upya.Wanachokwepa sasa hivi watakuja kufungwa na simba wakati wa ligi mwakani na mashabiki hawatawavumilia tena.YANGA wanasema wanataka kujiandaa na mechi yao na GORMAHIA wakati GORMAHIA watakuwepo kagame kushiriki mashindano hayo hayo.Hivi mbona kagera sugar hawakuogopa kucheza na simba mbele ya magufuli na umati ule wa mashabiki wa samba na wakaweza kuwafunga simba.Au yanga sasa sio levo moja na simba ipo levo na JKU!
 
Kama hawataki kushiriki kwa nini wasiandike barua kujulisha uongozi wa CECAFA kuwa yanga hawatoshiriki mashindano haya mpaka pale sababu zao za msingi zitatuliwe,na waziweke hizo sababu wazi ili tuone kama zinaingia akilini?.

Kama kukutanishwa Simba na Yanga nimbinu yakuvuna pesa tatizo ni nini?,mbona sioni Simba wakilalamika kupangwa na Yanga lakini yanga ndio wanalalamika?.
 
Ni namba mkuu, Yanga wanajua wakiwa kwenye hali kama waliyonayo sasa mara nyingi wanafungwa magoli kuanzia 4, 5, 6 + Kwa siasa za Simba na Yanga ni bora kujiweka kando kuliko kubebeshwa mzigo kama huo. Yanga mna bahati maana Simba ingevunja rekodi zake zote za idadi ya magoli ilizojiwekea dhidi yenu
 
Tuwe wa kweli ...Simba kwa timu gani waifunge Yanga NNE...dakika 180 Kenya mnashindwa kupata hata goli moja..timu yenu ya kawaida sana msijipe moyo...Yanga msimu mbaya wanakaa chini tarehe kumi Mwenyekiti Manji anarudi kundini picha LA kutisha linaanza
 
Wawafungie tu mashindano yenyewe hayana tofauti na bonanza
 
nilikuwa natafuta mahali walipoikacha Simba sijapaona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…