platozoom
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 9,424
- 11,320
Mzee MS hukuwahi kuwasikia Wazanzibar wanavyowasema Vibaya Watanganyika?! Hukuwahi kusoma mitandaoni chuki inavyoonyeshwa?The....
Huu ni ukumbi huru mtu anaweza kuweka chochote anachopenda.
Hapakuwa na haja ya kutoa maneno yasiyopendeza.
Soma habari ya bandari hapo chini:
(Hii makala nilimwandikia mtu wa mfano wako nahali fulani).
CHUKI DHIDI YA WAZANZIBARI
Nasikitika sana kila ninaposoma hapa maneno yaliyojaa chuki, dharau na kejli dhidi ya Wazanzibari.
Picha niipatayo ni kuwa wengi wanaoonyesha chuki hizi sababu kubwa ni kuwa hawajui historia iliyopelekea mapinduzi ya Zanzibar mwaka wa 1964.
Historia ya kupigania uhuru wa Zanzibar ina mengi na Rais wa TANU Mwalimu Nyerere alihusika sana kwanza katika kusaidia kuundwa kwa ASP na kisha katika kusaidia kufanya mapinduzi kuangusha serikali ya ZPPP na ZNP.
Baada ya mapinduzi ndiyo nchi hizi mbili zikaungana kufanya Tanzania hii tunayoiona hivi sasa.
Kabla ya mapinduzi Zanzibar ilikuwa nchi huru kama ilivyokuwa Tanganyika.
Kwa nini Mwalimu alisaidia kuangusha serikali iliyokuwapo madarakani?
Wakati wa kupigania uhuru wa Zanzibar kulikuwa na propaganda kubwa kuhusu historia ya utumwa ikisemwa Waafrika waliteswa na Waarabu na ni lazima Waafrika walioko Zanzibar wasaidiwe kujikomboa.
Propaganda hizi zikawa sababu kubwa ya chaguzi za Zanzibar zikawa zenye vurugu na damu kumwagika.
Lakini katika propaganda hizi suala la Uislam Zanzibar halikujitokeza na sababu kubwa halikujitokeza ni kuwa Wazanzibari wote ni Waislam.
Ilipokuwa ASP imeshindwa uchaguzi na serikali ikawa ni ya ZPPP/ ZNP uamuzi wa ASP ukawa lazima yafanyike mapinduzi na Tanganyika ikasaidia sana kuhakikisha kuwa serikali ya Zanzibar inapinduliwa.
Serikali ikaanguka na baada ya kuanguka serikali Zanzibar na Tanganyika zikaungana.
Hapakuwa na hofu yeyote hata kwa mbali kuwa Tanganyika inaungana na Zanzibar nchi ya Waislam watupu.
Wala Zanzibar haikuwa na hofu kuwa Tanganyika ina Wakristo na hawa wanaweza wakawa tatizo kwao hapo baadae.
Kwa kipindi kirefu hapakuwa na chokochoko zozote kuhusu Zanzibar na Uislam wao ndani ya muungano.
Matatizo yalitokea kwa mara ya kwanza Zanzibar ilipojiunga na OIC mwaka wa 1993.
Hiki ni kisa kirefu lakini muhimu kilichojitokeza ni kuwa Zanzibar ilitambua kuwa itastahamiliwa katika muungano pale pindi itakapojiweka mbali na Uislam na Waislam.
Hapa ndipo linapokuja tatizo la "Waarabu" na Bandari ya Dar es Salaam.
Lakini hizi ni nchi mbili zilizokuwa huru na Zanzibar haikuwa na shida ya kuungana na Tanganyika.
Leo tunasoma hapa watu wanaandika maneno makali ya kutisha kuwa Wazanzibari wafukuzwe Tanganyika.
Maneno haya hayapendezi.
Katika Jamii zetu hizi mbili Kuna baadhi kila upande huona upande mwingine kuwa hawafai. Mimi siwezi kuwa mnafiki nikatetea hawa na nikawaacha wale kwa kuwa si Watanganyika wenzangu.
Kuna Wazanzibari wanaishi vyema na Watanganyika huko Zanzibar na wapo Watanganyika wanaishi vizuri na Wazanzibari huko Zanzibar. Ndiyo maana utawapata Wazanzibari mpaka Rukwa, Mwanza au Tarime huko.
Tujitahidi kuyaona haya katika namna Bora sana kuliko kuchukua upande kila mara. Mimi nipo 40+ najitahidi nisiwe chachu ya kuwagombanisha Watu au kuwa shabiki wa upande Fulani, maana maisha haya mafupi.