FARHAN JR: YANGA WAMEIKKAMATA PABAYA TFF.
.
Ukitulia vyema kabisa ukisoma kwa utuo ile taarifa ya Yanga, kwenye msimamo pale haswa msimamo namba tatu (3) wanasema:
“Kutokana na mfululizo wa uvunjifu na kushindwa kusimamia kanuni za Ligi Kuu, Klabu ya YANGA imekosa imani na Kamati ya Uendeshaji ya Ligi Kuu, chini ya Mwenyekiti wake Steven Mnguto na Katibu wa Kamati hiyo Almas Kasongo”
Kiufundi sana hapo hawana Imani hata na uchunguzi ambao utaenda kufanyika na majibu ya uchunguzi huo, kwa kifupi sana wamesukuma kete tatu za moto kuelekea TFF, hivyo majibu yoyote kutoka kwa Kamati hayatotambulika na Yanga Afrika, kifupi anayepaswa kuchunguza kaambiwa ajichunguze na kujitathmini kama anafaa kuwa Mchunguzi, ndicho kilichopo hapo.
Hapo hata ukiwaambia warudie mechi watagoma kwa kusema hawana imani na Bodi, kimsingi unawarudisha TFF mezani waone namna gani ya kutatua hili la Yanga, ukisema halipo kwenye kifungu na wao wataomba kifungu cha mechi kutochezwa, ndio akili waliyoipiga hapo.
Kesi ishakuwa ngumu hii, Shahidi anasindikizwa na escort ya Polisi na mitutu kila Kona, aliyepeleka chakula Kituoni nae kawekwa ndani na Mwanasheria anasema pesa ya kumlipa wakatumie kwa Mganga, ndio hii sasa[emoji3]
.
AMEANDIKA FARHAN JR.
Sent from my TECNO KG5j using
JamiiForums mobile app